SoC02 Kuinua uchumi wa taifa na kukabiliana na ukosefu wa ajira kwa kuwekeza katika maeneo ya Teknolojia, Viwanda na Kilimo

Stories of Change - 2022 Competition

BRV

New Member
Apr 7, 2022
2
1
Kuandaa vijana kwa manufaa ya taifa katika nyanja kuu tatu tekinolojia, kilimo na viwanda ili kukuza uchumi wa taifa na raia wake.

Hoja kuu, kutokana na ongezeko la watanzania wengi wanaomaliza Elimu ya msingi na sekondari na kuelekea kuwa na wahitimu wengi wanamaliza na taifa kushindwa kuwamudu Basi ni wakati wa serikali kujitanua kutokana na mabadiriko ya kiulimwengu.

Serikali kupitia balozi zetu zilizopo mataifa mbalimbali hasa yaliyofanikiwa katika ngazi ya tekinolojia, kilimo na viwanda ni Wakati wa kuchambua ni nchi gani tuombe kutokana na lengo letu tuchukue vijana kadhaa waende katika taifa Hilo wakajifunze kwa vitendo katika eneo husika Tena siyo kwa kuangalia ufaulu Bali kuwekeza katika nguvu kazi kutokana na mazingira ya nchi yetu.

Watakaoenda maeneo hayo lazima watii na kufuata maelekezo yatolewayo kwani hiyo inakuwa ni ajenda na Sera ya taifa, tukifanya hivyo kwa miaka mitano(5) tutakuwa tumepata sampuli ya watakaokuja kuwa wafundishi wa wengine.

Kama taifa litafanikiwa hapo kwa kuwa tutakuwa tumewekeza katika tekinolojia, viwanda na kilimo Basi tutatatua tatizo kubwa la wakosefu wa ajira, tutazuia kujitokeza kwa vikundi nyang'anyi katika taifa, tutaacha kuagiza baadhi ya bidhaa nje ya nchi, tutakuwa soko la viwanda vikubwa duniani kwa kutoa marighafi ya kutosha kutokana na kilimo, tutakuwa na uwezo wa kusambaza Aina ya tekinolojia katika nchi yetu na zingine afrika, tutakuwa chachu ya mabadiriko katika nchi nyingi.

Tutajibu changamoto ya watanzania na waafrika wengi wanaokimbia afrika kwa kuenda kutafuta maisha nje ya nchi, tutatibu donda la vijana wengi kutojihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya ambao husukumwa na ugumu wa maisha na ukosefu wa ajira

Imeandaliwa na;
Sinto
 
Back
Top Bottom