Kuingiza siasa kwenye elimu ni kitu kibaya sana. Sioni kama kuna umuhimu wowote wa kuanzisha somo la Historia ya Tanzania

Tumefikia mahali pabaya sana kwenye hii Nchi! Yaani mawazo na akili ya mtu mmoja tu imegeuka kuwa ni mawazo ya watu milioni 55!!!

Hakuna utafiti ulio fanyika! Ni suala tu la mtu mmoja kulala usiku, na alipoamka asubuhi akaja na wazo la kuanzisha "somo la historia ya Tanzania"
(Colonial Education)
.

Ndugu bora angemka na kuwaza hili jambo alilichomeka kwenye hotuba wizara ikalibeba na kuwa agizo
 
Nasubiri hiyo mihitsari (syllabus) na vitabu vitakavyotoka na historia zilizosheheni sifa za tangu kuzaliwa Jiwe na mapambano yake dhidi ya mabeberu akipewa sifa ya uzalendo uliotukuka.
 
Mnapiga kelele weee na kuchambua facts tupu lakani leo hii mkiambiwa ingieni barabarani mnalala ndani asa sijui izi kelele zinawasaidia nini!!
 
Kwa hiyo mwanafunzi kuijua historia ya taifa lake hakuna faida yoyote kwa hiyo mwanafunzi?

Kweli dunia msongamano.
Una uhakika wanafunzi hawasomi hilo somo la historia kuanzia elimu ya msingi mpaka chuo kikuu?

Hili somo jipya la historia la huyu bosi wako litakuwa na jipya lipi?

Unadhani uzalendo unakuja tu kirahisi kwa kusoma somo darasani, au utaletwa na Viongozi Waadilifu na wenye maono ya mbali ya kuwafanya wananchi wenzao walio wengi kuishi maisha bora kama wanayoishi wao?
 
Hongera sana kwa kuniwahi kuandika uzi huu , hii nchi hata maombi yamedunda , hivi ni kipi ambacho somo la historia lililopo kimekosekana ?
Asante dada pongezi zako nimezipokea, kiukweli ni jambo la kushangaza kidogo kwa sababu karibia vitu vyote vinavyohusiana na historia ya nchi hii kuanzia chimbuko la tanganyika, harakati za kusaka uhuru, kupata uhuru hadi hapa tulipo vyote wanafunzi wanafundishwa. sasa sijui ni vitu gani vimekosekana na kama hivyo vilivyokosekana vina umuhimu, kwanini visiongezewe tu katika mitaala ya sasa kuliko kuanzisha somo jipya?
 
Dada tulia matoto yako yafundishwe nchi ilipotoka, ilipo na inapoenda
Mpaka sasa watoto wanafundishwa historia ya Tanzania kwenye somo la maarifa ya jamii, uraia na historia. Ni kipi kinachokosekana/hakifundishwi katika masomo hayo hadi tufikie uamzi wa kuanzisha historia ya tanzania kuwa somo linalojitegemea?
 
Hapo lengo sio historia bali ni interest binafsi za mtu mmoja.

Yani mzee anataka yeye ndie aandikwe wanafunzi wawe wana msoma kwenye kitabu.

Sasa ole wake waziri asichore picha yake kwenye book cover au kwenye hicho kitabu yule mzee asifanywe kuwa maina character ndo watamjua yeye nani.
 
Huu uzi umenikumbusha Burundi.Watoto wa shule za msingi walifikishwa mahakamani kwa kosa la kuchora chora na kuchana chana vitabu vilivyokuwa vimejaa picha za dekteta Nkurunziza.Hata dikteta Magufuli anataka ajaze vitabu hivyo vya historia picha zake na za mke wake.
 
Back
Top Bottom