Kuimarika kwa shillingi ya Tanzania dhidi ya shillingi ya Kenya

koryo1952

JF-Expert Member
Mar 7, 2023
380
763
Hii ni habari njema sana.

Shillingi ya Tanzania imeimarika sana dhidi ya shillingi ya Kenya. Miezi michache iliyopita shilingi moja ya kKenya ilikuwa ikibadilishwa kwa shillingi 22 ya Kitanzania.

Leo hii shillingi moja ya Kenya inabadilishwa kwa shillingi 15.52 ya Kitanzania. Hii ni hatua kubwa sana na ni neema kwa Watanzania. Sasa tuje kwenye athari yake kwa bidhaa za Kitanzania.

Leo hii sementi inayotoka Kenya na wengi tayari wamefungua godowns hapa Mwanza inauzwa mpaka shillingi 17,000 kwa mfuko fedha za Kitanzania na wakati sementi ya Tanzania inauzwa mpaka shillingi 24,000 kwa mfuko fedha za Kitanzania. Mwanza Huduma ndiye msambazaji mkuu wa sementi ya Tanzania Kanda ya Ziwa na wengineo wengi.

Biashara ya sementi ya Tanzania sasa imedoda kwake. Jinsi fedha ya Tanzania inavyozidi kuimarika bidhaa za Tanzania zitakosa wateja kwa sababu ya bei kubwa. Wenye viwanda vya Tanzania, Serikali, TRA angalieni suala hili kwa ajili ya kupunguza kodi ili bidhaa za Tanzania ziuzike.

Njoo Mwanza Sementi ya Kenya ndo inayotawala kwa sasa pamoja na kuwa haina ubora kwa ya Tanzania lakini mteja anaangalia sana tofauti ya bei.
 
Screenshot_20231221_203407_Chrome.jpg

Mama anaisafishA nchi...
 
Kipindi Cha mkapa shilingi ya Kenya iliporomoka mpaka kufika 1ksh=9.something Tshs nakumbuka kipindi hiko maduka ya tz wakawa hawapokei hela ya Kenya ilishuka sana thamani, nilikua nakaa mpakani na kipindi hicho kabla haijaporomoka ukipeleka hela ya Kenya dukani wanaichukua bila shida wanakupa exchange rate ya 1ksh=10tshs....

Ila kipindi hicho pesa yetu ilikua na nguvu maana dollar tulikua tunachange kwa 1usd=1100 tshs
 
Hapo TRA anatakiwa kuhakikisha bidhaa za Kenya zinapigwa kodi ya maana ili zinapoingia huku kwenye soko letu kuwe na urari au mizania na bidhaa za ndani.

Lasivo, kuporomoka kwa fedha ya Kenya kutaumiza viwanda vya Tanzania maana bidhaa zake zitakuwa expensive dhidi ya bidhaa za kenya.
 
Kasome upya uchumi
 
Hiyo si njia nzuri kwa mwananchi anaye hitaji bidhaa ,ni kumuumiza
 
Hii ni habari njema sana.

Shillingi ya Tanzania imeimarika sana dhidi ya shillingi ya Kenya. Miezi michache iliyopita shilingi moja ya kKenya ilikuwa ikibadilishwa kwa shillingi 22 ya Kitanzania.

Leo hii shillingi moja ya Kenya inabadilishwa kwa shillingi 15.52 ya Kitanzania. Hii ni hatua kubwa sana na ni neema kwa Watanzania. Sasa tuje kwenye athari yake kwa bidhaa za Kitanzania.

Leo hii sementi inayotoka Kenya na wengi tayari wamefungua godowns hapa Mwanza inauzwa mpaka shillingi 17,000 kwa mfuko fedha za Kitanzania na wakati sementi ya Tanzania inauzwa mpaka shillingi 24,000 kwa mfuko fedha za Kitanzania. Mwanza Huduma ndiye msambazaji mkuu wa sementi ya Tanzania Kanda ya Ziwa na wengineo wengi.

Biashara ya sementi ya Tanzania sasa imedoda kwake. Jinsi fedha ya Tanzania inavyozidi kuimarika bidhaa za Tanzania zitakosa wateja kwa sababu ya bei kubwa. Wenye viwanda vya Tanzania, Serikali, TRA angalieni suala hili kwa ajili ya kupunguza kodi ili bidhaa za Tanzania ziuzike.

Njoo Mwanza Sementi ya Kenya ndo inayotawala kwa sasa pamoja na kuwa haina ubora kwa ya Tanzania lakini mteja anaangalia sana tofauti ya bei.
Fafanua viziri mzee .
Umeinunua hiyo ksh au umiuza?

Maana mimi 29.12 nilinunua ksh kwa tsh. Kwa rate ya ksh 1 kwa tsh 25.

Tarehe 7.1 nikauza ksh 1 kwa tsh 14. Sasa naomba ufafanuzi ingawa inawezekana.
 
Back
Top Bottom