Kuibiwa kwenye Daladala

Watu wengi wanaoibiwa simu kwenye daladala mara nyingi huwa wameweka earphone.

Lilikua funzo lile, ila kosa langu siku hiyo nlikua nimebeba na hela katika mfuko Mwingine kwaiyo akili yangu nilizingatia hela zaidi ya simu
 
Haa ha...na alieibaa hukumuonaa

Kuna jamaa nilimuona nikamuhisi maana alikua kama ameishika kwa nyuma hivi, ila mimj Sasa ile akili ya haraka haraka kujua kua nimepigwa yaani Kama nilipagawa fulani hivi, ile nasema nimfatilie tayari kashapotea gizani vichochoroni zamanii
 
ha ha haah daah huu uzi nimecheka sana,nahisi utakuwa mrefu sana,sibanduki,ngoja nijibanze hapa nicheke niongeze siku za kuishi,ila huyo aliyeibiwa na kuwekewa mche wa sabuni katisha kuliko wote!
Sio Mche, kipande tu
 
Haaaaa vipi jamaa walikuwa wako njemaaa ? Vipi huku toa nakoz?
 
Mimi ilibaki kidogo teja anichomolee simu huku nagombania daladala maeneo ya mwenge. Machale yalinicheza kugeuka nyuma naona mtu kachomeka vidole kwenye mkoba nilimkata jicho alivyozuga nikabaki kucheka.
Muhindi unagombania daladala
 
Wanaume ndo mnaongoza kuibiwa sababu mnajiamini kupitiliza

Na ushamba wangu wa jiji lakini nilinusurika sikuibiwa kabisa, kwanini nyie wenyeji??????

Kuna siku kariakoo mida ya kumi na moja jioni tunasukumana kupanda daladala ebwana eh kuna jamaa anasisitiza tuwe makini na simu zetu kumbe ndo jizi nageuka hivi nakuta mkono wake kauzamisha katika pochi yangu nikasema we kaka umeniibia hapo gari ishaanza kuondoka sasa mi mguu mmoja upo garini mwingine unaning'inia chini kama nimedandia flani hivi

Wakati huo nimeshahamaki na kasimu kangu kapya kabisa kalikuwa na wiki tu nimekanunua laki nne

Nikafanikiwa kuzama ndani salamu ya kwanza kukagua kama imo .......nikaikuta huku abiria wengine wakinipongeza kuponea katika tundu la sindano

Ila nina uhakika kabisa nisingeikuta kingenikuta kama cha huyo paka hapo mi ningelia kabisa sio kuvunga na kamasi wangeziona wadau hahahahaha kibaka alinitukana siku hiyo.......wooooooooiii
 
Haa ha ha...Aaha mzee hawakuwa na silaha maana??
 
Machalii wakakuingiza mjini...duuh Ofisii ilikuelewaa kweli?!!
 
Ukaamua utoe sadakaa walet...haa ah
 
Laki NNE ingesepa kiutani utanii...
 
Mie huo mchezo nlitaka kufanyiwa pale karikoo kwenye ghorofa la wachina, teja kaja na smartphone matata sana nikaitamani tukakubaliana nimpe elfu 40,lkn machale yakanicheza kwamba hapa huenda ana wenzake nikitoa tu hela naitiwa mwizi akafu nanyanganywa cm na hela nmetoa.

Mm nikamzidi ujanja nikamwambia twende nikakupie hela kule kwenye jengo la mwalimu nyerere kule ilala

Yani kutoka karikoo hadi ilala ili tukalipane kwamba kule hawezi kuzingua maana kama ana wenzie wamejibanza sehemu hawatupati. Kusikia hivyo akasema wewe huna nia nayo nikamwambia kwaheri bwana.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…