Kwa maoni yangu, Makampuni haya hususan mbabe wa wababe Vodacom, huwezi kuyapa lawama wala Waziri wa Mawasiliano.. kwanini? kwasababu wangekuwa wamefanya kinyume na Serikali inavyotaka wangeshapigwa faini au hata kufukuzwa nchini! lakini kwa upande wa Ndugulile kama angekuwa ni yeye mtaabishaji aliyeleta GB 2 kwa tsh 10,000 (kumi elfu) huyu nae angeshafukuzwa uwaziri wake!
Kama mpaka leo makampuni hayajashusha vifurushi vyao, kama mpaka leo bado Ndugulile yuko ofisini kwake maana yake ni moja tu, kuwa mambo haya yana baraka zote na wenye mamlaka ya nchi hii
Hivyo nitoe rai kwa watanzania wenzangu ukimuona kobe juu ya mti huna haja ya kujiuliza maswali mengi ni kuwa yupo aliyempandisha hapo alipo
Kwa maana yoyote ile nchi hii ilikusudiwa kabisa kufanya mazungumzo na malaika washuke kutoka mbinguni ili waifunge mitandao.. nadhani malaika aligoma ndio ikabidi itumike plan B, na amini amini nawaambia isingekuwa Mungu kuingilia kati gb 1 ingeuzwa kwa shilingi 15,000-20,000! na msingefanya chochote.
Nawatakia mfungo mwema