Kuhusu vifurushi vya simu asilaumiwe Waziri Ndugulile au makampuni ya simu bali Serikali

Hofu-less

JF-Expert Member
May 19, 2014
520
1,031
Kwa maoni yangu, Makampuni haya hususan mbabe wa wababe Vodacom, huwezi kuyapa lawama wala Waziri wa Mawasiliano.. kwanini? kwasababu wangekuwa wamefanya kinyume na Serikali inavyotaka wangeshapigwa faini au hata kufukuzwa nchini! lakini kwa upande wa Ndugulile kama angekuwa ni yeye mtaabishaji aliyeleta GB 2 kwa tsh 10,000 (kumi elfu) huyu nae angeshafukuzwa uwaziri wake!

Kama mpaka leo makampuni hayajashusha vifurushi vyao, kama mpaka leo bado Ndugulile yuko ofisini kwake maana yake ni moja tu, kuwa mambo haya yana baraka zote na wenye mamlaka ya nchi hii

Hivyo nitoe rai kwa watanzania wenzangu ukimuona kobe juu ya mti huna haja ya kujiuliza maswali mengi ni kuwa yupo aliyempandisha hapo alipo

Kwa maana yoyote ile nchi hii ilikusudiwa kabisa kufanya mazungumzo na malaika washuke kutoka mbinguni ili waifunge mitandao.. nadhani malaika aligoma ndio ikabidi itumike plan B, na amini amini nawaambia isingekuwa Mungu kuingilia kati gb 1 ingeuzwa kwa shilingi 15,000-20,000! na msingefanya chochote.

Nawatakia mfungo mwema
 
Ndugu Waziri Ndungulile!

Ulijiweka msitari wa mbele kuja na utaratibu kubadili viwango vya bei za vifurushi vya simu huku ukituamonisha kuwa bei za hivyo vifurushi zitakuwa nafuu. Wananchi tukafurahi, Kumbe nyuma ya mazungumzo yako hayo kuna nia ovu ya kupandisha bei ya vifurushi, kitu kilichozaa taharuki kwa wananchi.

Tunamshukuru Mheshimiwa rais Samia kwa kuingilia kati na kuagiza kuwa bei zirudi kama zamani.

Wakati mheshimiwa rais anazungumza haya wewe uko kimya, hujaomba msamaha kwa umma kwa kutusababishia adha hii kubwa, na cha ajabu bado uko ofisini mpsaka leo! —Je unataka sisi wananchi tuendelee kukuamini kuwa upo kwa ajili ya best interest zetu?

Sasa cha ajabu zaidi, Baada hata ya agizo la raisi, wewe inafahamu kuwa kuna baadhi ya makampuni yametii agizo, ila kuna ambayo mpaka leo hii bado yamegoma—Wewe waziri hujatoa tamko lolote kuhusu hili, na cha ajabu umeshindwa kuhakikisha makampuni haya yanatekeleza agizo la serikali. Kwa udhaifu huu ulioonywsha wa kushindwa

1. Kusimamia agizo la rais
2. Kushindwa kusimamia best Interest za umma

Je unajiona bado una uhalali wa kuebdelea kuwa waziri wa Mawasiliano?

Hakuna excuse hapa kuwa eti Vodavom haijarudisha bei za vifurushi vya zamani kwa sababu wanafanya mchakato, mbona Airtel wameweza kubadiliksha fasta ndani ya siku mbili tu tangu tangazo la serikali kutaka bei za vifurushi zirudi kama zamani?

Ndungulile, kama wewe ni muungwana, achia ngazi, huwezi kuwa muungwana halafu usimamie vitu viwili tofauti kwa muda mmoja, wakati huo uko kimya kuzungumzia madhila ya bei kubwa ya vifurushi wanayokumbana nayo wananchi lakini wakati huohuo unashindwa kuenforce agizo la raisi
 
Jjamaa alituahidi kushusha gharama za vifurushi kumbe alimaanisha kinyume chake by the way yeye sio muhanga wa bei za vifurushi kama sisi
 
Kuna usanii mkubwa sana kwenye agizo la rais Samia.

Inakuwaje agizo la raisi linapuuzwa, je tutamheshimu vipi kwa ahadi zake nyingine na maagizo atakayotoa?
 
Back
Top Bottom