Dkt. Faustine Ndugulile agusia kuhusu matumizi ya fake account. Serikali kuja na sheria ya kulinda faragha

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Feb 26, 2018
2,490
3,534
Habari wadau..!

Leo kwenye mahojiano ya Waziri Dkt. Faustine Ndugulile akiwa kwenye mahojiano katika kipindi cha dakika 45 kinachoendeshwa na mtangazaji Farhia Middle wa ITV amegusia kuhusu suala la fake akaunti a.k.a fake ID maana kuna watu wanatamba sana as if wapo pinguni hawawezi kukamatwa pasipo kujua mkono wa Serikali ni kama mkono wa Mungu popote upo.

Kwa hili nadhani siku za Kigogo zinahesabika ,maana mkuu ndio kwanza ana siku mia moja katika wizara kabla hazijafika 100 zingine story za Kigogo zitakuwa zimekwisha na wale wanaotukana tukana wakulu na kueneza uzushi watanyooshwa kisawa sawa na kusambaratishwa wao na genge lao😂😂😂

----
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia Habari, Dkt. Faustine Ndugulile amesema wizara yake inatarajia kuunda Sheria ya Kulinda faragha za wanaotumia mawasiliano.

‘Data Protection Act’ itakuwa sheria kubwa ambayo ikitokea mtu anahitaji taarifa za mtumiaji basi kunakuwa na utaratibu maalumu wa kuzipata

Sheria itaeleza taarifa ambazo zinaweza kutolewa na taarifa ambazo hazipaswi kutolewa. Waziri Ndugulile amesema watafanya hayo ili kuhakikisha wanalinda faragha ya mtumiaji wa TEHAMA.

Dkt. Ndugulile amesema hii mitandao na ‘Apps’ ambazo watu wanatumia bure hukusanya taarifa na huwa zinauzwa kwenye makampuni ya biashara.


=========

MWANDISHI: Sio kweli kwamba (Wizara) imeanzishwa kwa ajili ya kubana mitandao ya kijamii?

WAZIRI NDUGULILE: Kusudio letu sisi kuu sio kwenda kudhibiti mitandao, ndio maana nasema Wizara yetu sisi ni pana ambayo ni Wizara wezeshi, inawezesha taasisi nyingine.

MWANDISHI: Hapa umezungumzia kuhusiana na suala zima la kuboreshwa mawasiliano lakini tunaona suala la gharama za mawasiliano ni kilio cha watu wengi sana nchini Tanzania, pengine tatizo ni nini hasa?

WAZIRI NDUGULILE: Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha tunaboresha mawasiliano na ukiangalia nianzie labda katika hizi simu za mikononi, utakumbuka tulivyoanza ulikuwa ukipokea simu unachajiwa na ukipiga simu unachajiwa lakini gharama ya kupiga kutoka mtandao mmoja kwenda mtandao mwengine ilikuwa ni gharama juu sana.

Gharama zimekuwa zinaendelea kushuka taratibu kutoka huko zilipokuwa, sasa hivi zimeshuka sana. Mfano sasa hivi gharama ya kupiga simu kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine imeshuka mpaka shilingi 2.

Lakini najua moja ya kilio kikubwa imekuwa vifurushi na nashukuru ndani ya hizi siku 100 tumeweza kutibu huo ugonjwa.

Tarehe 2 mwezi huu tumetoa tamko kupitia TCRA ya hatua ambazo tumezichukua na nichukue fursa hii kuwajulisha watanzania kwamba changamoto nyingi zilizokuwa kwenye vifurushi tumeweza kuzitibu na lazma upate ruhusa ya TCRA
  1. Hakukuwa na bei elekezi ya vifurushi, makampuni ya simu yalikuwa yanaamua tu, sasa hivi tumekuja na bei elekezi
  2. Upandishaji holela nao tumeudhibiti, sasa hivi ukipandisha kifurushi hautapandisha tena mpaka baada ya miezi 3
MWANDISHI: Suala la uhuru wa mitandao ukoje hasa mheshimiwa Waziri hapa kuna tafsiri imekuwa tofauti, kuna watu wanaona kama uhuru wa watu kutumia mitandao kidogo imekuwa ngumu nchini Tanzania kwasababu ukiandika taarifa ambayo inakosoa labda Serikali, utachukuliwa hatua, utaambiwa wewe ni mchochezi ama unafunguliwa kesi ya matumizi mabaya ya mitandao, hili likoje hasa mheshimiwa waziri!

WAZIRI NDUGULILE: Niseme hivi, uhuru wa mtu kujieleza umeainishwa katika Katiba na sheria zetu za nchi lakini uhuru huo nao una mipaka yake, sisi ambacho tumekiona kwasasa kama Serikali ni matumizi mabaya, sisi kama Serikali hatumzuii mtu kutukosoa, tukosoe kwamba muelekeo wa Wizara hii ya Mawasiliano na Teknolojia ya habari hamuendi sawa sawa, ngeweza mkafanya hiki, mkafinya hiki na mkifanya hiki mnaweza mkaenda vizuri zaidi.

Hio inaitwa 'objective' lakini unapokuja kuanza kunikosoa kwa kunidhalilisha mimi utu wangu na vitu vingine, hapo sasa umepitiliza mipaka ile ya wewe uhuru wako wa habari na kujieleza.

Shida hii ya mtandao ni kubwa kwasababu sasa hivi mtu yeyote ambae anaweza akafungua account ya mtandao wowote anaweza akapost vyovyote na sasa hivi kumezuka tabia kwamba vitu vinavyotisha, vinavyodhalilisha inasaidia wewe kupata watu wengi wanaokufuatilia kwenye mtandao na wengine wanatumia njia hiyo kwa wao kutengeneza hela kwasababu kutumia mitandao unaweza ukatengeneza hela ukiwa na wafuasi wengi.

Kwa hiyo mtu anatengeneza habari za kuzusha tu, za uchochezi tu, mambo kama hayo na ama kudhalilisha ama kutukana watu tu ili sasa watu wengi wawe wanakwenda kwenye mitandao yake.

Katika mitandao hiyo, sasa hivi kila mtu amekuwa mwandishi wa habari, kuna nyinyi ambao ni taaluma yenu lakini na mimi kwa sababu nikishafungua akaunti yangu naweza nikapost chochote, nikatoa mawazo yangu katika jambo lolote.

Huo uhuru sisi kama nchi tumeutoa lakini lazima tuhakikishe kwamba uhuru huu nao unazingatia miiko, maadili na tamaduni zetu kama Watanzania.

Lakini wengine wanafungua akaunti kazi yao ni kutukana tu, kuanzia asubuhi mpaka jioni ni kutukana na kudhalilisha watu, sasa hiyo sisi kama Serikali ni lazma tuchukue hatua na tunaendelea kuchukua hatua kuhakikisha kwamba tabia kama tunazidhiiti.

Wizara hii haijaanzishwa kuwa polisi wa mitandao

MWANDISHI: Mheshimiwa Waziri katika makosa ya kimtandao, kuna watu wanafungua akaunti hawatumii majina yao halisi, inamaana Serikali kuwapata watu hawa, haina uwezo huo?

WAZIRI NDUGULILE: Sio kwamba hatuna uwezo, tunao, ni kazi kubwa kwasababu mtu naingia pale anatumia jina sio la kwake halisi, anasajili akaunti anaanza kukashfu na kutukana watu. Sio kwamba tunashindwa kuwapata, tunawabaini na wengine tumeanza kuwachukulia hatua wale ambao tunaweza kuwafikia na tuna njia zetu siwezi kuzisema hapa, tunaweza tukawafikia na kuweza kuwabaini hata kwa hiyo fake account yake tunaweza tukabaini huyu mtu ni nani, yuko wapi na pale tunaweza tukachukua hatua, kuna wengine wako ndani ya nchi na wengine wako nje ya nchi.
 
.......

.... hawawezi kukamatwa pasipo kujua mkono wa serikali ni kama mkono wa Mungu popote upo .

.....

Aisee, baadhi ya wanasiasa wa Tanzania siku hizi wanamfananisha Mungu na vitu vingine!!!!

Kuna wengine wanaambiwa wana roho kama ya Yesu, wengine wanasema Dunia siyo ya Mungu.

Sent from my HTC U12 life using JamiiForums mobile app
 
Utazuiaje fake ID? means tukitaka kujiandikisha kwenye mitandao mfano JF lazima twende ofisi zao na vitambulisho vyetu vya uraia?
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Teknolojia haina mbabe, nadhani waziri ana mambo mengi sana ya msingi ya kufanya kuliko kuhangaika na fake ids za social networks.

Tena kwenye ulimwengu wa mambo ya computer n.k angepaacha kabisa maana ni kiza kinene.
Mwacheni ajaribu kabla hajafukuzwa kazi
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom