Kuhusu mahindi, nchi hii ina viongozi wa namna gani?

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,553
41,060
Kuna mambo yanatokea nchi hii, mpaka unajiuliza nchi ina laana gani hata ishindwe kuwapata viongozi wenye upeo wa kuyaona matatizo, kuyatafakari, na kisha kuyatafutia ufumbuzi sahihi.

Viongozi wa nchi hii mara nyingi wanatatua matatizo kwa kutengeneza matatizo makubwa zaidi!

Baadhi ya wananchi wamekuwa wanalalamika sana juu ya kupanda sana kwa bei za vyakula. Viongozi walistahili kulitafutia suluhisho tatizo hili bila ya kutengeneza tatizo kubwa zaidi.

Hawa viongozi wa Serikali, walivyo watu wa ajabu, wakiwa hawajaandaa utaratibu wowote wa soko la mazao ya wakulima, wakasema mazao ya chakula hayataruhusiwa kupelekwa nje ya nchi. Kilichofuatia, viongozi wale wajinga, wa ngazi ya chini wakaanza utekelezaji wa tamko hilo mara moja wakati wala haikutangazwa zuio hilo litaanza lini, na wala hawakusema wale wafanyabiashara ambao tayari walikuwa wamenunua mazao kwaajili ya kupeleka nje, wapeleke wapi hayo mazao.

Kilichotokea baada ya hapo, malori yaliyokuwa yanapeleka mahindi nchini Kenya yakasimamishwa mpakani na kuambiwa wauze mahindi hayo nchini, lakini hawaambiwi wakauze kwa nani. Viongozi hawa ambao mimi nawaita wajinga, hawajui kuwa soko huwa linatafutwa na likishapatikana linalindwa.

Toka wakati huo, wanunuzi wote wakubwa wa mahindi wamepotea. Wakulima wanahangaika wakauze wapi mazao, na wengi wao wana mikopo ya mabenki na wameanza kufuatwa ili walipe. Wanunuzi wachache ambao wanaendelea kununua, wananunua kwa bei ya chini kupindukia.

Jana, nimeambiwa mkoani Ruvuma na Njombe, maeneo ya vijijini bei ya gunia moja la mahindi la kilo 100 limeshuka toka sh. 75,000 mpaka sh. 25,000. Fikiria gunia la mahindi kununuliwa kwa sh. 25,000. Yaani magunia 10 ndiyo mkulima apate sh. 250,000. Kila unayeongea naye anasema kwa bei hiyo hakuna haja ya kulima. Labda walime kwaajili ya chakula chao tu na siyo kwaajili ya kuuza.

Huu ujinga uliofanywa wa kuzuia uuzwaji wa mahindi nje, wakati utaratibu wa kuyanunua mazao hayo ndani ya nchi haujaandaliwa, utazidi kuua kilimo.

Kwa bei hizo za mahindi, hata yale matrilioni anayotumia Bashe eti kuandaa mashamba kwaajili ya vijana, hakuna mtu atakayeenda kulima. Kwenda kulima, maana yake umechagua umaskini wa kutupwa.

Kuwa kiongozi inamaanisha kuwa na uwezo wa kuona mbali. Yaani kuyaona matatizo kabla hayajatokea, na kuyatafutia ufumbuzi kabla ya madhari hayajatokea, lakini hapa nchini petu, hicho kitu hakipo. Viongozi hawaoni mbali, wanafanya vitu bila ya kufikiria nini kitatokea kwa kufanya maamuzi fulani.

Tumetoka kwenye kilio cha bei ya chakula, sasa tunaingia kwenye kilio cha mkulima mazao yake kukosa soko na kununuliwa kwa bei ya kutupwa.

Tunataka tutoke kwenye tatizo la uduni wa huduma za bandari, tuingie kwenye tatizo la kuporwa rasilimali ya bandari. Yaani hatuna uwezo wa kutatua tatizo bila ya kutengeneza tatizo jingine.
 
Miaka kadhaa toka Bashe awe waziri amesimamia msimamo wake wa kuruhusu soko huria la mahindi. Wote mnajua namna alivyokuwa anashambuliwa humu kwamba anajifanya mjuaji kuachia mahindi yauzwe nje ya nchi.

Sasa wametest tu kile watu walikuwa wanalilia, watu hao hao wanalia tena afungue mipaka.

Tuwe wavumilivu, hadi tar 1 kama tulivyo ahidiwa. Tukate leseni kabisa na tax clearance iwepo mkononi.
 
TANZANIA NCHI ISIYOISHA MAZINGAOMBWE
 
Nadhani matukio mengi sana yanayotengenezwa kipindi hiki ni juhudi kuu ya kuhamisha watu waache kujadili issue ya Bandari.
Jiulize, huu ni mwezi wa 6 kipindi ambacho ndio mahindi mapya yametoka mashambani muda si mrefu.
Ilikuaje wakakomaa mahindi yakauzwa nje mwezi wa 10,11,12 ambapo sio kipindi cha mavune waje wabadirike leo.
Ni nguvu kubwa sana ya kuunda matukio ili mjadala wa watu uhame. Mbaya zaidi matukio mengine yanaumiza watu .
 
Itoshe kusema tu shauri Yao hao wakulima. Nakumbuka kunakipindi nasafiri, tulipofika maeneo Fulani tukaluta bwawa chafu sana mifugo, binadamu Wana share maji bsi mjadala ukaanza inakuwaje ile hali wakati kilomita 50 mbele upo mto kwanini serekali isiwapelekee maji safi. Kwangu Mimi mjadala ule uliitimishwa na kauli ya mchangiaji mmoja aliyesema shauri yao coz wamerizika na ile hali ilimradi yeye akitaka hata maji ya chupa anapata, kwao siku wakizinduka na kujua ilikuwa n hali Yao watadai.
 
Wananchi brother kijijini wameaminishwa maendeleo ni hisani ya watawala na siyo haki yao ya msingi sababu mtu akili yote ipo shambani hivyo usiwalaumu
 
Nadhani matukio mengi sana yanayotengenezwa kipindi hiki ni juhudi kuu ya kuhamisha watu waache kujadili issue ya Bandari.
Jiulize, huu ni mwezi wa 6 kipindi ambacho ndio mahindi mapya yametoka mashambani muda si mrefu.
Ilikuaje wakakomaa mahindi yakauzwa nje mwezi wa 10,11,12 ambapo sio kipindi cha mavuno waje wabadirike leo.
Ni nguvu kubwa sana ya kuunda matukio ili mjadala wa watu uhame. Mbaya zaidi matukio mengine yanaumiza watu .
 
Spika amesema wakauze NFRA na bashe kakazia kama wanauza kwa bei hiyo eti wamejitakia wenyewe ila hii nchi wanahitaji tufanye kunji hakuna namna
 
Miaka kadhaa toka Bashe awe waziri amesimamia msimamo wake wa kuruhusu soko huria la mahindi. Wote mnajua namna alivyokuwa anashambuliwa humu kwamba anajifanya mjuaji kuachia mahindi yauzwe nje ya nchi.

Sasa wametest tu kile watu walikuwa wanalilia, watu hao hao wanalia tena afungue mipaka.

Tuwe wavumilivu, hadi tar 1 kama tulivyo ahidiwa. Tukate leseni kabisa na tax clearance iwepo mkononi.
Majitu kwenye hii nchi hayaeleweki yaani,wamelia saana kuhusu bei ya mazao kuwa juu baada ya mipaka kuwa wazi. Serikali ikifunga mipaka pia mnalalamika,, sometimes nashindwa hata kuelewa tunataka nini hasa. Kuongoza ni kazi ngumu mnoo
 
Back
Top Bottom