I am saddened by the fact that a man who seemed hard working and principled has turned out to be just another promiscuous politician, and of dubious integrity. [/COLOR][/SIZE][/FONT]
Ndugu Moshi,
Sababu hizi ndizo zinazoifanya Tanzania kila leo inarudi nyuma na wala si kwenda mbele.
Sababu hizi ndo zinawafanya watanzania hodari kama ninyi mkimbie nchi na kwenda kuendeleza nchi za watu wengine!
Sababu hizi ndizo miaka nenda rudi, tangia tupate uhuru zimekuwa zinakwamisha nchi yetu kwenda mbele, na pia zimekuwa zina "frustrate" wanamapinduzi wengi kama ninyi na wengi wengi tusomao maoni yao humu kwenye JF kuwa msitake kabisa kujihusisha na siasa za nchi yetu ambazo zimeoza na zinatoa wadudu!
Sababu hizi ndo zimenifanya niache hata kusoma magazeti yetu hususa ya kisiasa, au kufuatilia maamuzi ya serikali yetu. Sababu hizi ndizo ambazo zimesababisha Jambo Forums, pamoja na Forums nyingi zilizotangulia kabla ya hii kuwa maarufu, kwani tunatoa hasira zetu huku tumefichama!
Tangia tupate uhuru tumekuwa tunaletewa sababu nyingi na tofauti ambazo zinafanya tusiendelee, tatizo ni kuwa wengi wazitoazo ni walewale, kutokana na ujinga wa Watanzania tumekuwa tunazikubali, au zikiwa recycled sisi tunaamini kuwa ni sababu mpya! Leo waziri wa elimu anakwambia matokea ya darasa la saba ati mazuri kwani asilimia 70 wameenda sekondari! Je, mwaka 2008 bado unamzuia kijana wa miaka 13 au 14 aisendelee na shule ya sekondari kwa kumwambia ati amefeli?
Viongozi wetu wengi ndiyo wamekuwa makaburu kuliko wale makaburu wa kusini mwa afrika na sisi bado tumekaa kimya tu.
Leo hii jiji la Dar ati bado halina maji ya bomba, na wizara ya maji na nishati ipo na mawaziri wake! Its a JOKE, a BIG JOKE! Tuna wizara ya madini, ila madini yetu hata kusafishwa yanasafishiwa nje ya nchi (eg S.Africa). Tuna wizara ya mawasiliano na uchukuzi shirika letu la ndege ni nyanya!, mabasi ya abiria yanaua mamia ya abiria kila mwaka! Tuna Wizara ya Afya- Kipindupindu kimepiga kambi nchini! Tuna wizara na mawaziri wa mambo ya ndani na sheria, kile leo askari wetu wanakamtwa wakiwa majambazi au wamekodisha silaha zao kwa majambazi!
Samahanini waungwana, hasira ndizo zinazoandika sasa wala siyo mimi na nitaachia hapa! Bungeni ni kama Sinema za vikaragosi- tunaambiwa ati tuna vyama vingi!