-Mufti ni cheo cha uongozi wa dini kuongoza waumini kwa kutoa ufafanuzi na maamuzi yanayoendana na sheria za dini,ila ni cheo chenye mipaka.
Mathalan hapa Tanzania Mufti yeye hajihusishi na mengine isipokua dini tu,na yeye wala sio kiongozi wa juu kuliko wote hata nchi ingekua ya kiislam kiongozi mkuu angekua Amiirul Muuminiim na sio Mufti.
-Kwa shia ama waajemi Ayatollah ni sawa na kusema AMIIRUL MUUMINIIM kiongozi wa kiislam ambaye anatawala KIDINI NA KISIASA. Yeye ni top leader katika ngazi zote za KIDINI NA KISIASA. Anatoa ufafanuzi na maamuzi katika ngazi ya sheria za kidini na kisiasa na yeye ndiye kiongozi mkubwa kuliko wote ikiwemo rais anaripoti kwake.