Kuhusu BAE.... Panya hula yamini!

Iko siku atatokea Paka na sio pakashume tena na yote yatamwaga hadharani. Yaani bado hamshangai ajali ya kuua wale mabint wa Mwanza waliopelekewa ajali ndani ya Bodaboda pale karibu na St Peter's Mahakama imemuona Mh. na kosa la kuua na adhabu ni 700,000/= na huruhusiwi kuhoji wala kukata rufaa itakuwa hiyo Rada?
Nchi hiii ina wenyewe na itajengwa na wenye MOYO tu, sijui km tutafika
 

Attachments

  • LOWASSA CHENGE.jpg
    LOWASSA CHENGE.jpg
    18 KB · Views: 40
Wanajua kabisa wakiinga kwenye MTEGO wa kuwataja wata OPEN A PANDORA BOX!

Kati yao (CCM) hakuna aliye salama. Kama wanashindwa kuwataja wabunge wa CDM wanaotuhumiwa kula rushwa, kweli wataweza kuwataja WENZAO WA CCM. (ref kesi ya TL na wabunge wala rushwa).

Mwisho wa siku watatajana tu tena kwa details wakidhani adhabu itategemea nani kala sana. Chezea holly spirit wewe....Muda unakuja na sasa upo kila mtu atamkana ndugu yake ili aiokoe nafsi yake!
 
panya wa siku hizi wajanja sana, ukiwategea mtego wanautegua kisha wanatafuna wanachokikuta, walitegua mtego wa azimio la arusha,
 
utafikiri wale Panya waliotaka kutumaliza kule Lushoto kwa kuzalisha viroboto vilivyosababisha ugonjwa wa TAUNI.
 
Panya wote washakula kiapo cha kutotajana nani aliyekula au aliyekwapua chakula ghalani
japo kila mmoja alipata kipisi cha chakula toka ghalani kamwe hawatatajana
panya mkubwa kashasema wote wako safi hakuna aloiyeiba so wala tusishangae panya wanavyolindana
 
Nimependa mashairi ya leo JF!kumbe Mzee Mwanakijiji una wenzio wengi wanaweza kutunga mashairi,
Nawapa Big Up" Ila sumu ya kuwamaliza hawa panya wasiotaka kutajana tunaikaanga na ikiwa tayari
tutawalisha,haitakuwa kama ilie ya mzee wa Mbeya ambayo India wanaweza kuitoa mwilini.
 
Mie naombea Malawi wakomae na ziwa, ili hawa panya tuone watafanyaje especially where are they going to finance the dispute, nadhani kama itatokea noma lazima watarudi tu tukae pamoja ili tuungane.
 
Umoja wa panya ni dhahiri ndiyo maana wanaongezeka badala ya kupungua. Ole wako ujifanye wewe ni Donald julius Mathew basi panya watahakikisha unajinyonga ili waendelee kula vizuri. Uzuri wa panya ni mmoja tu Mungu kawanyima utashi hivyo kuwa ni vigumu kuona knachokuja mbele yao!
 
Beti Moja:
Panya hawakamatani, na pia hawatajani,
Ati nani kala nini, kala wapi na kwanini,
Panya daima makini, watajane kiwe nini?
Wanapokula ghalani, panya hula na yamini!

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)


Hapa nadhani unaonglea mijipanya iliyoko kwenye makorido ya wizara na ofisi zingine nyeti za serikali yetu, hii wala haifi kwa mitego na dawa hizi za kawaida, hii inahitaji mbinu mpya. Nadhani inakaribia itapatikana muda si mrefu
 
Chikawe ni lazima atatetea ufisadi kwani yeye ni mmoja wao; juzi juzi amenunua nyumba kule Lushoto kwa pesa za wizi na kama anabisha aeleze hizo $ 800,000 alizolipa alizipata wapi?

Yikes!! panya mwingine..
 
Back
Top Bottom