Kuhusu BAE.... Panya hula yamini!

wamekula bwana...halafu hawa panya wanapendana kweli..hivi ulimsikia yule panya mkubwa alivyosema juzi? yaani alibadilika kabisa na lile karatasi lililokuwa na maandishi lilikosewa na kuwa hakuna panya mwenzake aliyekula ghalani!!
nilistuka kwli maana panya huyu mkubwa hakuwa na haya...aliongea kwa kujiamini huku akichezesha mkia wake hata masikio yake kuna moja lilikuwa linacheza cheza nadhani alkuwa anasikiliza kama wale mifugo wengine aliokuwa anaongea nao walikuwa wanapiga kelele..

lakini ukimwangalia vizuri kwenye vidole vyake huyu panya mkubwa bado kuna masalia ya chakula ghalani, kuna vi punje punje kwenye mikono alinawa lakini hakutaka...yaani we acha tu...panya hawa!!!
 
Beti Moja:
Panya hawakamatani, na pia hawatajani,
Ati nani kala nini, kala wapi na kwanini,
Panya daima makini, watajane kiwe nini?
Wanapokula ghalani, panya hula na yamini!

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)

Hawa panya hatari sana, wanataka hata kumla paka
 
Bunge lilihamasika sana kwenda kudai ile chenji ya rada...mbona kila kitu kiko kimya? Hii ndio Tanzania tunayoijenga ambayo haitaki wakubwa wawe accountable kwa wananchi.
 
Wamwambie panya mwenzao Membe afute kauli yake kwamba anawajua walionufaika na pesa ya rada. Yana mwisho haya hata kama hayatafanana na yale yanayotokea kule Uarabuni. Na wala wasidhani kuwa kuyafunikafunika hivi kutafanya yasahaulike.
 
Beti Moja:
Panya hawakamatani, na pia hawatajani,
Ati nani kala nini, kala wapi na kwanini,
Panya daima makini, watajane kiwe nini?
Wanapokula ghalani, panya hula na yamini!

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)

Wanajua kabisa wakiinga kwenye MTEGO wa kuwataja wata OPEN A PANDORA BOX!

Kati yao (CCM) hakuna aliye salama. Kama wanashindwa kuwataja wabunge wa CDM wanaotuhumiwa kula rushwa, kweli wataweza kuwataja WENZAO WA CCM. (ref kesi ya TL na wabunge wala rushwa).
 
hakika nawaambieni kwa utaratibu huu hii nchi haipo mikono salama na hata siku moja tusitegemee nchi hii kupata maendeleo kutoka katika mikono ya mapanya haya. hati nini? hakuna aliyehusika kuiba fedha za rada kutoka selikalini? ebo! kwa hiyo ni selikali ya uingereza ikaingia pale bot na kujiidhinishia fedha yetu kwenye mradi wa kifisadi? wakati gavana anawaangalia tu, waziri anawaangalia tu na mwanasheria mkuu anaangalia tu haya si matusi? hata kama hawausiki kitendo cha kujiachia uchi mpaka mtu anakuja kwenye hazina yako na kujiidhinishia fedha hiyo yatosha kukuwajibisha ya kwamba tuliweka mapoyoyo kulinda hadhina yetu! sasa usalama wa taifa hili upo wapi? upo kwa ajili ya kinakubenea na ulimboka? yaani fedha ya kutosha ya nchi ianibiwa hakuna aliyejua ila aliyeiba baba yake anagundua anamwambia mwanae hapana rudisha ulikotoa mwanae anakomaa baba anaamua kuchukua kwa nguvu kilichoibiwa anakuja kwako anakwambia mwanangu kwa kushirikiana na mwanao wamekuibia hiki sasa najua wewe jirani yangu masikini hawa watoto walichofanya si cha kiungwana chako hiki hapa. ukatai kwa kusema mimi sijaibiwa unakipokea kisha unanunu vitabu, watoto wengine wanakuuliza sasa baba sisi tunaishi kwa wasi wasi tueleze ni nani katika sisi watoto aliyeshirikiana na mtoto wa tajiri kuiba chetu? unasema hakuna! huu ni upumbavu kwa hiyo mtoto wa yule tajiri aliingia chumbani kwetu akatuibia? ati tunausalama wa taifa! napinga napinga napinga mambo haya hayakubaliki ni another type of silly season, 2015 mbali mno tukifika na watu hawa tutakuwa nyaka nyaka!
 
Na juzi juzi panya kajifungua kakimbilia Ghalani Tanesco Nguzo kutoka Mufindi zimepigwa Chata la kwa Ntabo Mbeki. Panya wakajisahau wakaingia Ghalani CDM wakaliwa na paka wa huko
 
Beti Moja:
Panya hawakamatani, na pia hawatajani,
Ati nani kala nini, kala wapi na kwanini,
Panya daima makini, watajane kiwe nini?
Wanapokula ghalani, panya hula na yamini!
Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)

Mkuu kisu hata kikiwa kikali sana hakijikati chenyewe! Panya tuchukuwe hatua!
 
Linaongelewa sasa hivi bungeni. Myika anaibana serikali lakini Chikawe anaendelea kusisitiza hakuna ushahidi na mashahidi wa bAE na SFO hawawezi kupatikana. Anasema mtu yeyote mwenye ushahidi awe wa ndani au nje aupeleke immediately na uwe credible na serikali itashughulikia immediately.
 
Linaongelewa sasa hivi bungeni. Myika anaibana serikali lakini Chikawe anaendelea kusisitiza hakuna ushahidi na mashahidi wa bAE na SFO hawawezi kupatikana. Anasema mtu yeyote mwenye ushahidi awe wa ndani au nje aupeleke immediately na uwe credible na serikali itashughulikia immediately.
nilisikia tu habari za Mh. Chikawe kusema kuwa hakuna aliyehusika kwa Tanzania lakini sikuamini bali kama ameendelea kusisitiza, ni dhahiri kuna kitu kinakaribia kutokea kwa nchi hii na hawa watawala watajutia uongo wao.
Kwa maana mwanzoni labda hawakujua lakini walipoambiwa ukweli huo ni bora wangelikaa kimya kuliko kuukataa huku wakijua.
Wasisahau kuwa walikula viapo na hiyo inawabind hata na vizazi vyao vitakavyofuata!

 
Beti Moja:
Panya hawakamatani, na pia hawatajani,
Ati nani kala nini, kala wapi na kwanini,
Panya daima makini, watajane kiwe nini?
Wanapokula ghalani, panya hula na yamini!

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)

Dawa ya hawa panya ni kuwachoma mishikaki!!
 
nilisikia tu habari za Mh. Chikawe kusema kuwa hakuna aliyehusika kwa Tanzania lakini sikuamini bali kama ameendelea kusisitiza, ni dhahiri kuna kitu kinakaribia kutokea kwa nchi hii na hawa watawala watajutia uongo wao.
Kwa maana mwanzoni labda hawakujua lakini walipoambiwa ukweli huo ni bora wangelikaa kimya kuliko kuukataa huku wakijua.
Wasisahau kuwa walikula viapo na hiyo inawabind hata na vizazi vyao vitakavyofuata!


Chikawe ni lazima atatetea ufisadi kwani yeye ni mmoja wao; juzi juzi amenunua nyumba kule Lushoto kwa pesa za wizi na kama anabisha aeleze hizo $ 800,000 alizolipa alizipata wapi?
 
Hawa mawaziri ndio wanaotutia umaskini, Membe anasema atawataja anawajua ni waziri, Chikawe anae wajua atutajie, polisi wanashuhudia , wananchi wanashuhudia Rais yupo, Takukuru wapo, Hii nchi ya ajabu kupata kutokea utafikiri wanaigiza kumbe ndivyo ilivyo
 
Mwambieni Mnyika amwambie Chikawe amfikishe Chenge mahakamani aeleze jinsi alivyojipatia zile dola milioni moja zilizokutwa kule visiwa vya Jersey. Ushahidi wanao wanaotuhumiwa.
 
Panya hawa ni wajanja, paka kavaa kengele,
Panya mekuwa kiranja, paka napiga kelele,
Panya anakula mkwanja, paka naota upele,
Panya hula yamini.

Umoja wao hatari, wenye ghala mashakani,
Mejiandaa kwa shari, urithi wetu mnadani,
Hakika hii kamari, paka hoi taabani,
Panya hula yamini.
 
Back
Top Bottom