Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,251
- 44,586
Na. M. M. Mwanakijiji
Nilipata nafasi siku hizi mbili tatu kukutana na watu muhimu sana kwenye sakata la mauaji ya Oktoba 29-Novemba... Kitu ambacho sikuwa nimejua kwa undani ni kwa kiasi gani hawa jamaa wa ICC wako up to date na yanayoendelea Tanzania. Leo nimeweza kutembelea ICC na kuweza kueleweshwa vizuri kabisa kuhusu utendaji kazi wao na kwanini "Tanzanian Case" iko interesting kwao na inaweza kuwa ni ya kipekee (unique) hasa kutokana na uwepo mkubwa wa ushahidi wa "social media".
Hawa jamaa wana kitengo kabisa cha kukusanya "digital evidence" (yaani ushahidi wa kikompyuta) wa matukio, na mambo ambayo wanayafanyia uchunguzi. Kwa mujibu wa jamaa mmoja (Mfaransa) kesi ya Tanzania inaenda kujaribu (to test) ni jinsi gani ushahidi wa kidigitally unaweza kutumika kuwakuta watu na hatia. Kwa maelezo yake kesi ya Rwanda ilitegemea sana ushahidi wa kawaida wa wahusika wakuu - nani aliona nini, wapi na kwa vipi na hivyo kutegemea ushahidi wa wengi kuweza kuwakuta watu ama wana hatia au hawana hatia. Hilo ni moja.
Lakini la pili ni jinsi gani kesi ya Tanzania iko "unique" kwa sababu matukio yaliyotajwa kutukia Oktoba/Novemba yanaweza kurudiwa tena. Huyu bwana amedokeza kuwa tofauti na ile ya Rwanda ambapo matukio makubwa ya mauaji ya wingi yalitokea kwa mfululizo kwa karibu siku 100. Kwa hiyo mambo yanavyoenda kutokea kuanzia leo wanayaangalia kwa karibu sana kuona ni jinsi gani wahusika wa Oktoba/Novemba wanaweza kurudia tena.
La mwisho na ndilo lilinipa interest ya mimi kufunga safari hii ndefu ni jinsi gani hadi hivi sasa imeonekana hakuna mahakama au vyombo vyovyote vya uhalifu Tanzania vimeonesha nia, uwezo, sababu na matakwa ya kuchunguza mauaji, ubakaji, ulawiti ambao unadaiwa kufanywa na vyombo vya dola. NIlikuwa na swali moja ambalo nilitaka hasa ufafanuzi wake "je kama waandamanaji wanavunja miundo mbinu na kuharibu mali mbalimbali je inahalalisha vyombo vya dola kuua waandamanaji hao hadi majumbani kwao". Alicheka kwa kama kejeli na kunijibu "not in international system of criminal justice and probably not in any national form of justice". Nikaelewa.
Hata hivyo, uwezekano mwingine ambao unaangaliwa hasa kulingana na kinachoenda kutokea ni uwezekano wa kuanzishwa Special Tribunal for Tanzania (STT). Mahakama Maalumu kama hii ndiyo iliyosimamia kesi za kina Milosevic na zile za Rwanda (iliyokuwa inakaa Arusha). Hili inawezekana ndiyo ikawa njia ya haraka ya kuwashughulikia wahusika wa mauaji Tanzania.
Kama nilivyodokeza siku mbili tatu - kama wamejiandaa kuua na wengine wamejiandaa kuwafunga. Yaani, kuna watu wanachukulia hili kwa userious kweli. Mmoja wa jamaa niliokutana nao Mhispania huyu anasema kuwa kati ya vitu ambavyo hawakuvifikiria ni kuwa inawezekana Arusha ikaja kutumika kusikiliza kesi za mauaji ya Oktoba; kwa maneno yake "an incredible example of poetic justice".
Haki ya wananchi kuipinga na kuikataa serikali yao iachwe tu...mengine haya tutaelewana tu.
Huu ni wimbo wa kusindikiza salamu hizi: