Kuhusu AI contents kwenye Mitandao ya kijamii

Kuhusu AI contents kwenye Mitandao ya kijamii

kaangalie I raised a giant mermaid page ya magical vibes

nililia kama mbwa🤣🤣🤣presha muda wote Joanah
 
Angalia usichelewe au kubaki nyuma sana. Siku zote kwenye safari angalia mnaelekea wapi.
Dunia inaelekea huko usikokutaka.
 
Unakimbia dunia inapoelekea haya wewe baki hapo hapo tukakukuta huoni hata Yanga sasa hivi nyimbo zao zote za hamasa ni AI nachotaka kwambia mabadiliko huwa hayakataliwa ni kuungana nayo kama kuongeza ubunifu IA inafanya jinsi unavyotaka prompt yako ipoje so kama unaona vitu vya AI vinakaosoro boresha wewe AI inarahisisha mambo ila bado inatuitaji sisi binadamu halisi tuikontroo kwa kuipa maelekezo ukiipa maelekezo ovyo inakupa kitu cha ovyo ukiipa maelekezo bora inakupa kitu bora, changamka mzee usilale

Mawakili wenyewe waliozoea tuandikisha mikataba ya mauziano za mali sijui kuandaa avidaviti sijui nini kwa beinza ajabu sijui toa laki tano sijuo laki na nusu kwa sasa wanaisoma namba AI inamaliza kazi tunaenda stationary tunaprint kwa legal paper kisha tunaenda mahakama zetu za serikali kugonga mhuri kwa elfu tano tu dadeki yani buku 5 dadeki unapewa na risiti EFD show imeisha kwaiyo sasa wachague na wao wandae hizo nyaraka na wagonge mhuri kwa elfu tano au wamuachie AI haaa haaa
 
Nishaacha kitambo sana matumizi ya mitandao ya kijamii hasa Tiktok,fb and the likes. kama ni kupata habari basi jf ni mkombozi wangu! ile mitandao imejaa upumbavu mwingi.
 
Salaam Wandugu,

Kuna jambo kuhusu AI contents naliona kwa upande wangu binafsi kadri siku zinavyoenda ndio nazidi kuzikwepa, nitaweka mifano;

Nikiwa naperuzi Mitandao ya kijamii ikatokea nakutana na video ambayo imetengenezwa kwa AI huwa na skip haraka sana bila kupoteza muda.

Pia kutokana na kukua kwa matumizi ya AI wafanyabiashara wengi wameanza kutumia kutengeneza posters za matangazo ya biashara zao, kiukweli nyingi naona zina distractions, unaweza kutamani kusoma kilichoandikwa ila unaona kabisa huu mzigo wa AI unajikuta unaruka chap, naona kama zinakosa uhalisia, sijui kwa wengine mnalionaje hili jambo.

Karibuni.
Ni swala la muda tu, huwezi kukimbia AI
 
Me post zangu zote natumia AI, na nnapata wateja, nafkiri kila mtu ana choices zake, lakini ulimwengu ww sasa AI itaendelea kutumika sana, watu wanataka mambo marahisi

Siku hizi wafanya biashara hadi whatsapp wanaweka settings za AI, inakujibu vizuri mpaka mwisho, watu wanaokoa muda
 
Nishaacha kitambo sana matumizi ya mitandao ya kijamii hasa Tiktok,fb and the likes. kama ni kupata habari basi jf ni mkombozi wangu! ile mitandao imejaa upumbavu mwingi.
Wengine tunatumia kwasababu ya biashara, asilimia 70 ni kwasababu ya biashara, hiyo 30 ndio mengineyo.
 
Me post zangu zote natumia AI, na nnapata wateja, nafkiri kila mtu ana choices zake, lakini ulimwengu ww sasa AI itaendelea kutumika sana, watu wanataka mambo marahisi

Siku hizi wafanya biashara hadi whatsapp wanaweka settings za AI, inakujibu vizuri mpaka mwisho, watu wanaokoa muda
Sijasema haina faida, inajulikana inarahisisha kazi kwa asilimia kubwa,
Ila kitendo cha kuingia B2B sites unakutana na AI agent huwa naambia niunganishwe na mtu pumzi😁
 
Haya unayolalamika hapa umeyaandika mwenyewe kweli au umetumia ChatGPT kukusaidia? Maana siku hizi nyie mnaolalamikia AI ndio huwa mnatumia AI hiyo hiyo kulalamika!
 
Back
Top Bottom