Makonyeza
Member
- Feb 2, 2020
- 69
- 252
(Tunafanya Siasa tusiyoijua)
Nimeona na kusoma sehemu kadhaa makada na mashabiki wa chama cha Chadema wakilaani taarifa inayokinasibu chama cha ACT wazalendo kuunga mkono juhudi za serikali katika miradi mbalimbali ya kimaendeleo.
Na niliiona nongwa hii tangu siku ya sherehe za mapinduzi ambapo bendera za chama cha ACT zilionekana zikipepea uwanja wa Aman kuashiria USHIRIKI wao katika sherehe zile za kuadhimisha mapinduzi matukufu.
Ninaiita Nongwa kwa sababu ushiriki wao haukuandikwa au kupokelewa wala kutafsiriwa vizuri na wenzao wa Chadema.
Hii ndio ilinipa wasiwasi na kujiuliza, hivi hii fani ya Siasa tunayojinasibu kuishiriki tunaijua kweli au ni wahanga tu wa mkumbo bila kujua maana, athari wala hatima yetu kwa kufuata tusilolijua.
ACT ni chama huru cha Siasa kilicho na Sera zake, katiba yake, Itikadi zake, vikao vyake, maamuzi yake, malengo yake na viongozi wake kama ilivyo kwa vyama vingine vya Siasa ikiwemo Chadema.
Lakini zaidi kwa sasa ACT sio tu chama cha Siasa cha Upinzani, bali pia ni sehemu ya serikali kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar ikishiriki kuongoza nchi na kuendesha serikali kwa kuwa sehemu ya serikali hiyo ya Umoja wa kitaifa, na ushahidi wa hilo ni ukweli kwamba baadhi ya mawaziri wa serikali ya Zanzibar wametoka ACT-Wazalendo.
Sasa katika mantiki hiyo hivi ni vipi unaweza kutarajia au hata kuwaza tu kwamba eti ACT wasishiriki shughuli za kiserikali ilhali na wao ni sehemu ya hiyo serikali? Tena shughuli zenyewe ni maazimisho tu ya kumbukizi za kihistoria?
Hivi ni kwa sababu ACT kashiriki sherehe za mapinduzi leo tumuite majina ya kihuni, mara chama cha michongo, mara ooooh kiongozi wao fulani msaliti, hii hapana!
ACT ni sehemu ya serikali, hivi unatarajia viongozi wake washupaze mishipa ya shingo kupinga na kulaani kila linalofanywa na serikali hata kama ni zuri? hii pia HAPANA.
Tamko la kiongozi wa ACT kwamba wataiunga mkono serikali katika juhudi zake za kusimamia miradi ya kimaendeleo, ni tamko mujarabu kabisa na ndicho hasa wanachotakiwa kukifanya kwa sasa lakini bila kusahau kofia yao ya Upinzani kwa kukosoa na kuelekeza penye umuhimu wa kufanya hivyo.
Naomba niwakumbushe wenzangu wa Chadema, kuwa chama cha Upinzani haimaanishi Sasa kuwa na kibali cha kulaani na kupinga kila kinachofanywa au kusemwa na serikali, kama kinachotakiwa kufanywa kikifanyika kwa faida ya taifa kwanini basi pia usitoe tamko la kuunga mkono mwenendo huo mzuri ili kuchochea mazuri mengine kufanyika?
Yaani namaanisha mwanao ni mtundu sana na kila leo unamchapa kwa utundu wake, hivi siku akifanya lolote zuri basi kwa nini usimpigie makofi kumpongeza ili kumjengea kijiamini na kutenda uyapendayo? Sijui naeleweka!?
Kikatiba, kazi ya chama cha Upinzani ni pamoja na kuikosoa na kuishauri serikali, tunaelewa kukosoa tu, vipi serikali ikifanya vizuri, hatupaswi kuipa kongole ili iendelee kufanya vizuri?
ACT katoka ubavuni mwa Chadema, haileti taswira nzuri kwa Chadema kupoteza muda kumuandama ACT na viongozi wake ilhali kila mmoja ana shughuli zake za kufanya, ebu kwa sasa kila mtu ashinde MECHI zake halafu mwisho wa msimu tutahesabu mwenye alama nyingi.