Kuhusu ACT - Wazalendo kuunga mkono Serikali, acha leo niteme nyongo

Makonyeza

Member
Feb 2, 2020
67
248
(Tunafanya Siasa tusiyoijua)

Nimeona na kusoma sehemu kadhaa makada na mashabiki wa chama cha Chadema wakilaani taarifa inayokinasibu chama cha ACT wazalendo kuunga mkono juhudi za serikali katika miradi mbalimbali ya kimaendeleo.

Na niliiona nongwa hii tangu siku ya sherehe za mapinduzi ambapo bendera za chama cha ACT zilionekana zikipepea uwanja wa Aman kuashiria USHIRIKI wao katika sherehe zile za kuadhimisha mapinduzi matukufu.

Ninaiita Nongwa kwa sababu ushiriki wao haukuandikwa au kupokelewa wala kutafsiriwa vizuri na wenzao wa Chadema.
Hii ndio ilinipa wasiwasi na kujiuliza, hivi hii fani ya Siasa tunayojinasibu kuishiriki tunaijua kweli au ni wahanga tu wa mkumbo bila kujua maana, athari wala hatima yetu kwa kufuata tusilolijua.

ACT ni chama huru cha Siasa kilicho na Sera zake, katiba yake, Itikadi zake, vikao vyake, maamuzi yake, malengo yake na viongozi wake kama ilivyo kwa vyama vingine vya Siasa ikiwemo Chadema.

Lakini zaidi kwa sasa ACT sio tu chama cha Siasa cha Upinzani, bali pia ni sehemu ya serikali kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar ikishiriki kuongoza nchi na kuendesha serikali kwa kuwa sehemu ya serikali hiyo ya Umoja wa kitaifa, na ushahidi wa hilo ni ukweli kwamba baadhi ya mawaziri wa serikali ya Zanzibar wametoka ACT-Wazalendo.

Sasa katika mantiki hiyo hivi ni vipi unaweza kutarajia au hata kuwaza tu kwamba eti ACT wasishiriki shughuli za kiserikali ilhali na wao ni sehemu ya hiyo serikali? Tena shughuli zenyewe ni maazimisho tu ya kumbukizi za kihistoria?

Hivi ni kwa sababu ACT kashiriki sherehe za mapinduzi leo tumuite majina ya kihuni, mara chama cha michongo, mara ooooh kiongozi wao fulani msaliti, hii hapana!

ACT ni sehemu ya serikali, hivi unatarajia viongozi wake washupaze mishipa ya shingo kupinga na kulaani kila linalofanywa na serikali hata kama ni zuri? hii pia HAPANA.

Tamko la kiongozi wa ACT kwamba wataiunga mkono serikali katika juhudi zake za kusimamia miradi ya kimaendeleo, ni tamko mujarabu kabisa na ndicho hasa wanachotakiwa kukifanya kwa sasa lakini bila kusahau kofia yao ya Upinzani kwa kukosoa na kuelekeza penye umuhimu wa kufanya hivyo.

Naomba niwakumbushe wenzangu wa Chadema, kuwa chama cha Upinzani haimaanishi Sasa kuwa na kibali cha kulaani na kupinga kila kinachofanywa au kusemwa na serikali, kama kinachotakiwa kufanywa kikifanyika kwa faida ya taifa kwanini basi pia usitoe tamko la kuunga mkono mwenendo huo mzuri ili kuchochea mazuri mengine kufanyika?

Yaani namaanisha mwanao ni mtundu sana na kila leo unamchapa kwa utundu wake, hivi siku akifanya lolote zuri basi kwa nini usimpigie makofi kumpongeza ili kumjengea kijiamini na kutenda uyapendayo? Sijui naeleweka!?

Kikatiba, kazi ya chama cha Upinzani ni pamoja na kuikosoa na kuishauri serikali, tunaelewa kukosoa tu, vipi serikali ikifanya vizuri, hatupaswi kuipa kongole ili iendelee kufanya vizuri?

ACT katoka ubavuni mwa Chadema, haileti taswira nzuri kwa Chadema kupoteza muda kumuandama ACT na viongozi wake ilhali kila mmoja ana shughuli zake za kufanya, ebu kwa sasa kila mtu ashinde MECHI zake halafu mwisho wa msimu tutahesabu mwenye alama nyingi.

_20220123_100206.JPG
 
Kijana kutoka zambarau umekula?
Kuna takataka nyingine hii ulishawahi andika usisahau kuisoma
👇🏿
 
ACT wazalendo ni tawi la CCM.

Waasisi:

Kitila Mkumbo..........................CCM.

RIP Anna Mghwira....................CCM

Mgwamba............................CCM

Zitto Kabwe............ Tawini ( kama Lipuli kwa Simba)
 
Wana haki ya kumfollow yoyote as long as hawavunji sheria na taratibu za nchi...
 
(Tunafanya Siasa tusiyoijua)

Nimeona na kusoma sehemu kadhaa makada na mashabiki wa chama cha Chadema wakilaani taarifa inayokinasibu chama cha ACT wazalendo kuunga mkono juhudi za serikali katika miradi mbalimbali ya kimaendeleo.

Na niliiona nongwa hii tangu siku ya sherehe za mapinduzi ambapo bendera za chama cha ACT zilionekana zikipepea uwanja wa Aman kuashiria USHIRIKI wao katika sherehe zile za kuadhimisha mapinduzi matukufu.

Ninaiita Nongwa kwa sababu ushiriki wao haukuandikwa au kupokelewa wala kutafsiriwa vizuri na wenzao wa Chadema.
Hii ndio ilinipa wasiwasi na kujiuliza, hivi hii fani ya Siasa tunayojinasibu kuishiriki tunaijua kweli au ni wahanga tu wa mkumbo bila kujua maana, athari wala hatima yetu kwa kufuata tusilolijua.

ACT ni chama huru cha Siasa kilicho na Sera zake, katiba yake, Itikadi zake, vikao vyake, maamuzi yake, malengo yake na viongozi wake kama ilivyo kwa vyama vingine vya Siasa ikiwemo Chadema.

Lakini zaidi kwa sasa ACT sio tu chama cha Siasa cha Upinzani, bali pia ni sehemu ya serikali kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar ikishiriki kuongoza nchi na kuendesha serikali kwa kuwa sehemu ya serikali hiyo ya Umoja wa kitaifa, na ushahidi wa hilo ni ukweli kwamba baadhi ya mawaziri wa serikali ya Zanzibar wametoka ACT-Wazalendo.

Sasa katika mantiki hiyo hivi ni vipi unaweza kutarajia au hata kuwaza tu kwamba eti ACT wasishiriki shughuli za kiserikali ilhali na wao ni sehemu ya hiyo serikali? Tena shughuli zenyewe ni maazimisho tu ya kumbukizi za kihistoria?

Hivi ni kwa sababu ACT kashiriki sherehe za mapinduzi leo tumuite majina ya kihuni, mara chama cha michongo, mara ooooh kiongozi wao fulani msaliti, hii hapana!

ACT ni sehemu ya serikali, hivi unatarajia viongozi wake washupaze mishipa ya shingo kupinga na kulaani kila linalofanywa na serikali hata kama ni zuri? hii pia HAPANA.

Tamko la kiongozi wa ACT kwamba wataiunga mkono serikali katika juhudi zake za kusimamia miradi ya kimaendeleo, ni tamko mujarabu kabisa na ndicho hasa wanachotakiwa kukifanya kwa sasa lakini bila kusahau kofia yao ya Upinzani kwa kukosoa na kuelekeza penye umuhimu wa kufanya hivyo.

Naomba niwakumbushe wenzangu wa Chadema, kuwa chama cha Upinzani haimaanishi Sasa kuwa na kibali cha kulaani na kupinga kila kinachofanywa au kusemwa na serikali, kama kinachotakiwa kufanywa kikifanyika kwa faida ya taifa kwanini basi pia usitoe tamko la kuunga mkono mwenendo huo mzuri ili kuchochea mazuri mengine kufanyika?

Yaani namaanisha mwanao ni mtundu sana na kila leo unamchapa kwa utundu wake, hivi siku akifanya lolote zuri basi kwa nini usimpigie makofi kumpongeza ili kumjengea kijiamini na kutenda uyapendayo? Sijui naeleweka!?

Kikatiba, kazi ya chama cha Upinzani ni pamoja na kuikosoa na kuishauri serikali, tunaelewa kukosoa tu, vipi serikali ikifanya vizuri, hatupaswi kuipa kongole ili iendelee kufanya vizuri?

ACT katoka ubavuni mwa Chadema, haileti taswira nzuri kwa Chadema kupoteza muda kumuandama ACT na viongozi wake ilhali kila mmoja ana shughuli zake za kufanya, ebu kwa sasa kila mtu ashinde MECHI zake halafu mwisho wa msimu tutahesabu mwenye alama nyingi.

View attachment 2092469
🚮🚮
 
Zitto hana tofauti na Prof Lipumba angalia siasa zake na kila aina ya vurugu anazozifanya kwenye chama anachoingia au chama Cha upinzani dhidi ya CCM ndio utamuekewa huyu mfia dini ni mbaguzi na mvurugaji na mwisho wake ni Kama wa Lipumba.
 
(Tunafanya Siasa tusiyoijua)

Nimeona na kusoma sehemu kadhaa makada na mashabiki wa chama cha Chadema wakilaani taarifa inayokinasibu chama cha ACT wazalendo kuunga mkono juhudi za serikali katika miradi mbalimbali ya kimaendeleo..................

View attachment 2092469
Hapa mwenye Nyongo ni Makonyeza kwa sababu
1. ACT kwa utashi wao wameona wajisalimishe umateka kwa CCM. Kwa sababu ni chama kinachoongozwa na watu wazima wenye elimu ya kutosha HAKUNA SHIDA. Ni haki yao.
2. CHADEMA wameona ACT ya watu wazima wenye elimu kujisalimisha mateka kwa CCM kuna ukakasi, ni msimamo wao. HAKUNA SHIDA.
Wote hawana nyongo mwenye nyongo ni MAKONYEZA.
 
(Tunafanya Siasa tusiyoijua)

Nimeona na kusoma sehemu kadhaa makada na mashabiki wa chama cha Chadema wakilaani taarifa inayokinasibu chama cha ACT wazalendo kuunga mkono juhudi za serikali katika miradi mbalimbali ya kimaendeleo.

Na niliiona nongwa hii tangu siku ya sherehe za mapinduzi ambapo bendera za chama cha ACT zilionekana zikipepea uwanja wa Aman kuashiria USHIRIKI wao katika sherehe zile za kuadhimisha mapinduzi matukufu.

Ninaiita Nongwa kwa sababu ushiriki wao haukuandikwa au kupokelewa wala kutafsiriwa vizuri na wenzao wa Chadema.
Hii ndio ilinipa wasiwasi na kujiuliza, hivi hii fani ya Siasa tunayojinasibu kuishiriki tunaijua kweli au ni wahanga tu wa mkumbo bila kujua maana, athari wala hatima yetu kwa kufuata tusilolijua.

ACT ni chama huru cha Siasa kilicho na Sera zake, katiba yake, Itikadi zake, vikao vyake, maamuzi yake, malengo yake na viongozi wake kama ilivyo kwa vyama vingine vya Siasa ikiwemo Chadema.

Lakini zaidi kwa sasa ACT sio tu chama cha Siasa cha Upinzani, bali pia ni sehemu ya serikali kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar ikishiriki kuongoza nchi na kuendesha serikali kwa kuwa sehemu ya serikali hiyo ya Umoja wa kitaifa, na ushahidi wa hilo ni ukweli kwamba baadhi ya mawaziri wa serikali ya Zanzibar wametoka ACT-Wazalendo.

Sasa katika mantiki hiyo hivi ni vipi unaweza kutarajia au hata kuwaza tu kwamba eti ACT wasishiriki shughuli za kiserikali ilhali na wao ni sehemu ya hiyo serikali? Tena shughuli zenyewe ni maazimisho tu ya kumbukizi za kihistoria?

Hivi ni kwa sababu ACT kashiriki sherehe za mapinduzi leo tumuite majina ya kihuni, mara chama cha michongo, mara ooooh kiongozi wao fulani msaliti, hii hapana!

ACT ni sehemu ya serikali, hivi unatarajia viongozi wake washupaze mishipa ya shingo kupinga na kulaani kila linalofanywa na serikali hata kama ni zuri? hii pia HAPANA.

Tamko la kiongozi wa ACT kwamba wataiunga mkono serikali katika juhudi zake za kusimamia miradi ya kimaendeleo, ni tamko mujarabu kabisa na ndicho hasa wanachotakiwa kukifanya kwa sasa lakini bila kusahau kofia yao ya Upinzani kwa kukosoa na kuelekeza penye umuhimu wa kufanya hivyo.

Naomba niwakumbushe wenzangu wa Chadema, kuwa chama cha Upinzani haimaanishi Sasa kuwa na kibali cha kulaani na kupinga kila kinachofanywa au kusemwa na serikali, kama kinachotakiwa kufanywa kikifanyika kwa faida ya taifa kwanini basi pia usitoe tamko la kuunga mkono mwenendo huo mzuri ili kuchochea mazuri mengine kufanyika?

Yaani namaanisha mwanao ni mtundu sana na kila leo unamchapa kwa utundu wake, hivi siku akifanya lolote zuri basi kwa nini usimpigie makofi kumpongeza ili kumjengea kijiamini na kutenda uyapendayo? Sijui naeleweka!?

Kikatiba, kazi ya chama cha Upinzani ni pamoja na kuikosoa na kuishauri serikali, tunaelewa kukosoa tu, vipi serikali ikifanya vizuri, hatupaswi kuipa kongole ili iendelee kufanya vizuri?

ACT katoka ubavuni mwa Chadema, haileti taswira nzuri kwa Chadema kupoteza muda kumuandama ACT na viongozi wake ilhali kila mmoja ana shughuli zake za kufanya, ebu kwa sasa kila mtu ashinde MECHI zake halafu mwisho wa msimu tutahesabu mwenye alama nyingi.

View attachment 2092469
Sio kila wakati unakaa mbali na adui yako., inabidi ukae naye umzoee kutimiza malengo yako ndivyo ilivyo kwenye siasa., Chadema wana theory za kizamani sana ambazo sasa zimepitwa na wakati, bado wanaamini kushika dola kutokana na hali waliyonayo tunasema ni ujinga uliopindukia.,

Zitto alikuwa hivyo hivyo lakini alipounganisha chama na Zanzibar amefumbuka macho na kuona siasa hasa za Tanzania vipi zinatakiwa ziendeshwe., Maalim Seif alikuwa mwanasiasa ambaye karibu 90% alifanikiwa kisiasa, leo hakuna mzanzibari mahali asiyejielewa ni kutokana na juhudi zake kisiasa chadema walijifunza siasa toka zanzibar, lakini kuna mahalai wamekuwa wakiachwa pande kubwa sana kutokana na ujuaji wao na sasa ndio inawa-cost.

Naamini Zitto atakuwa mwanasiasa mkubwa zaid huko tanganyika baada ya anguko la chadema linavyoendelea hivi sasa., Ni ujinga wa hali ya juu kwa nchi kama Tanzania kutegemea utawaongoza wananchi kupitia youtube na twitter kama anavyofanya yule mtu belgium na canada., maalim alipata madhila mengi sana lakini alirudi zanzibar kuungana na wananchi liwalo na liwe.,

Chadema wanataka wapewe nchi kwenye kisahani cha chai., Chama kishakufa mwenyekiti wao yuko ndani wameshindwa kutoka huko waliko kuja kumsaidia mwenyekiti wao wa juu zaidi kwenye chama ni ishara kwamba Chadema imefeli kwenye mapambano.

Zitto ni ginious,
 
(Tunafanya Siasa tusiyoijua)

Nimeona na kusoma sehemu kadhaa makada na mashabiki wa chama cha Chadema wakilaani taarifa inayokinasibu chama cha ACT wazalendo kuunga mkono juhudi za serikali katika miradi mbalimbali ya kimaendeleo.

Na niliiona nongwa hii tangu siku ya sherehe za mapinduzi ambapo bendera za chama cha ACT zilionekana zikipepea uwanja wa Aman kuashiria USHIRIKI wao katika sherehe zile za kuadhimisha mapinduzi matukufu.

Ninaiita Nongwa kwa sababu ushiriki wao haukuandikwa au kupokelewa wala kutafsiriwa vizuri na wenzao wa Chadema.
Hii ndio ilinipa wasiwasi na kujiuliza, hivi hii fani ya Siasa tunayojinasibu kuishiriki tunaijua kweli au ni wahanga tu wa mkumbo bila kujua maana, athari wala hatima yetu kwa kufuata tusilolijua.

ACT ni chama huru cha Siasa kilicho na Sera zake, katiba yake, Itikadi zake, vikao vyake, maamuzi yake, malengo yake na viongozi wake kama ilivyo kwa vyama vingine vya Siasa ikiwemo Chadema.

Lakini zaidi kwa sasa ACT sio tu chama cha Siasa cha Upinzani, bali pia ni sehemu ya serikali kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar ikishiriki kuongoza nchi na kuendesha serikali kwa kuwa sehemu ya serikali hiyo ya Umoja wa kitaifa, na ushahidi wa hilo ni ukweli kwamba baadhi ya mawaziri wa serikali ya Zanzibar wametoka ACT-Wazalendo.

Sasa katika mantiki hiyo hivi ni vipi unaweza kutarajia au hata kuwaza tu kwamba eti ACT wasishiriki shughuli za kiserikali ilhali na wao ni sehemu ya hiyo serikali? Tena shughuli zenyewe ni maazimisho tu ya kumbukizi za kihistoria?

Hivi ni kwa sababu ACT kashiriki sherehe za mapinduzi leo tumuite majina ya kihuni, mara chama cha michongo, mara ooooh kiongozi wao fulani msaliti, hii hapana!

ACT ni sehemu ya serikali, hivi unatarajia viongozi wake washupaze mishipa ya shingo kupinga na kulaani kila linalofanywa na serikali hata kama ni zuri? hii pia HAPANA.

Tamko la kiongozi wa ACT kwamba wataiunga mkono serikali katika juhudi zake za kusimamia miradi ya kimaendeleo, ni tamko mujarabu kabisa na ndicho hasa wanachotakiwa kukifanya kwa sasa lakini bila kusahau kofia yao ya Upinzani kwa kukosoa na kuelekeza penye umuhimu wa kufanya hivyo.

Naomba niwakumbushe wenzangu wa Chadema, kuwa chama cha Upinzani haimaanishi Sasa kuwa na kibali cha kulaani na kupinga kila kinachofanywa au kusemwa na serikali, kama kinachotakiwa kufanywa kikifanyika kwa faida ya taifa kwanini basi pia usitoe tamko la kuunga mkono mwenendo huo mzuri ili kuchochea mazuri mengine kufanyika?

Yaani namaanisha mwanao ni mtundu sana na kila leo unamchapa kwa utundu wake, hivi siku akifanya lolote zuri basi kwa nini usimpigie makofi kumpongeza ili kumjengea kijiamini na kutenda uyapendayo? Sijui naeleweka!?

Kikatiba, kazi ya chama cha Upinzani ni pamoja na kuikosoa na kuishauri serikali, tunaelewa kukosoa tu, vipi serikali ikifanya vizuri, hatupaswi kuipa kongole ili iendelee kufanya vizuri?

ACT katoka ubavuni mwa Chadema, haileti taswira nzuri kwa Chadema kupoteza muda kumuandama ACT na viongozi wake ilhali kila mmoja ana shughuli zake za kufanya, ebu kwa sasa kila mtu ashinde MECHI zake halafu mwisho wa msimu tutahesabu mwenye alama nyingi.

View attachment 2092469

Kuunda serikali gani?. ACT Wana Wizara tatu tu, na Makamu wa Kwanza wa Rais, ambaye anapangiwa kazi na Rais wa Zanzibar Mh Mwinyi. Wakati wenzao wa CCM wamekamata Wizara zote zilizobaki na nafasi ya Makamu wa pili wa Rais ambaye ana hadhi ya waziri mkuu. Nyie endeleeni kujikomba kwa serikali iliyowatandika na kuwaibia Kura kwenye uchaguzi. Ninachojiuliza wapemba waliwezaje kukubali kujiuza kwa Zitto?. Ngoja aendelee kuwalambisha miguu kwa CCM .
 
ACT siyo chama cha upinzani, ni chama tawala ni sehemu ya serikali ya Tanzania Visiwani. CHADEMA ni chama cha upinzani haipo serikalini, hivyo kwa maoni yangu, kama wanavyoinanga CCM, kadhalika kwa ACT.
 
(Tunafanya Siasa tusiyoijua)

Nimeona na kusoma sehemu kadhaa makada na mashabiki wa chama cha Chadema wakilaani taarifa inayokinasibu chama cha ACT wazalendo kuunga mkono juhudi za serikali katika miradi mbalimbali ya kimaendeleo.

Na niliiona nongwa hii tangu siku ya sherehe za mapinduzi ambapo bendera za chama cha ACT zilionekana zikipepea uwanja wa Aman kuashiria USHIRIKI wao katika sherehe zile za kuadhimisha mapinduzi matukufu.

Ninaiita Nongwa kwa sababu ushiriki wao haukuandikwa au kupokelewa wala kutafsiriwa vizuri na wenzao wa Chadema.
Hii ndio ilinipa wasiwasi na kujiuliza, hivi hii fani ya Siasa tunayojinasibu kuishiriki tunaijua kweli au ni wahanga tu wa mkumbo bila kujua maana, athari wala hatima yetu kwa kufuata tusilolijua.

ACT ni chama huru cha Siasa kilicho na Sera zake, katiba yake, Itikadi zake, vikao vyake, maamuzi yake, malengo yake na viongozi wake kama ilivyo kwa vyama vingine vya Siasa ikiwemo Chadema.

Lakini zaidi kwa sasa ACT sio tu chama cha Siasa cha Upinzani, bali pia ni sehemu ya serikali kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar ikishiriki kuongoza nchi na kuendesha serikali kwa kuwa sehemu ya serikali hiyo ya Umoja wa kitaifa, na ushahidi wa hilo ni ukweli kwamba baadhi ya mawaziri wa serikali ya Zanzibar wametoka ACT-Wazalendo.

Sasa katika mantiki hiyo hivi ni vipi unaweza kutarajia au hata kuwaza tu kwamba eti ACT wasishiriki shughuli za kiserikali ilhali na wao ni sehemu ya hiyo serikali? Tena shughuli zenyewe ni maazimisho tu ya kumbukizi za kihistoria?

Hivi ni kwa sababu ACT kashiriki sherehe za mapinduzi leo tumuite majina ya kihuni, mara chama cha michongo, mara ooooh kiongozi wao fulani msaliti, hii hapana!

ACT ni sehemu ya serikali, hivi unatarajia viongozi wake washupaze mishipa ya shingo kupinga na kulaani kila linalofanywa na serikali hata kama ni zuri? hii pia HAPANA.

Tamko la kiongozi wa ACT kwamba wataiunga mkono serikali katika juhudi zake za kusimamia miradi ya kimaendeleo, ni tamko mujarabu kabisa na ndicho hasa wanachotakiwa kukifanya kwa sasa lakini bila kusahau kofia yao ya Upinzani kwa kukosoa na kuelekeza penye umuhimu wa kufanya hivyo.

Naomba niwakumbushe wenzangu wa Chadema, kuwa chama cha Upinzani haimaanishi Sasa kuwa na kibali cha kulaani na kupinga kila kinachofanywa au kusemwa na serikali, kama kinachotakiwa kufanywa kikifanyika kwa faida ya taifa kwanini basi pia usitoe tamko la kuunga mkono mwenendo huo mzuri ili kuchochea mazuri mengine kufanyika?

Yaani namaanisha mwanao ni mtundu sana na kila leo unamchapa kwa utundu wake, hivi siku akifanya lolote zuri basi kwa nini usimpigie makofi kumpongeza ili kumjengea kijiamini na kutenda uyapendayo? Sijui naeleweka!?

Kikatiba, kazi ya chama cha Upinzani ni pamoja na kuikosoa na kuishauri serikali, tunaelewa kukosoa tu, vipi serikali ikifanya vizuri, hatupaswi kuipa kongole ili iendelee kufanya vizuri?

ACT katoka ubavuni mwa Chadema, haileti taswira nzuri kwa Chadema kupoteza muda kumuandama ACT na viongozi wake ilhali kila mmoja ana shughuli zake za kufanya, ebu kwa sasa kila mtu ashinde MECHI zake halafu mwisho wa msimu tutahesabu mwenye alama nyingi.

View attachment 2092469
Ni kweli ACT Wazalendo ni sehemu ya serikali ya Zanzibar na kwa muktadha huo serikali ya Muungano. Kwa dhana hiyo pana Bwana Zito yuko sahihi kabisa kuweka wazi wao wataiunga mkono serikali kwa yale mazuri ya kimaendeleo. Kama ndivyo ilivyo, staili yao ya ukosoaji itatofautiana sana na vyama vingine kama Chadema. Hilo liko wazi na halina mjadala.

Na kama wataendesha sivyo mambo yao ya kisiasa wenye dhamana ya kuwakosoa au kuwazondoa ni wanachama wao na sio vyama vingine vya upinzani. Act wako huru kufanya mambo yao bila kujali kama yatawafurahisha wengine. Hiyo ni haki yao, wavumiliwe tu. Wachamama wao ndio wenye kuamua, wengine hayawahusu labda itakapofika siku ya kuanzisha Ukawa mwingine. Vinginevyo vyama vingine kuweni wapole tu.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom