Kuhatarisha usalama wa Taifa? Give me a Break!

Ni imani yangu kuwa inawezekana serikali ya Kikwete ingekuwa inafanya vizuri kama ingekuwa sikivu na kuwajibika kwa wananchi bila ya kutiwa kiburi na Usalama wa Taifa na kufuata porojo za propaganda za Usalama wa Taifa.

Usalam wa taifa wangekuwa wanafanya kazi ya kusaidia rais basi wangefanya lolote lile mapacha watatu waondolwe hata kama rais alikuwa hataki.

Inawezekana breking news za UWT zinamfikia Lowassa hata kabla JK hajajua.
 
Wakuu... Amani iwe kwenu!!
Nimekuwa nikijiuliza kwa nini mara nyingi serikali inafanya makosa mengi na makubwa dhidi ya sheria? Nikagundua hatimaye kuwa tatizo kubwa la nchi hii ni kule kuongozwa na Usalama wa Taifa.

Tatizo utamaduni wetu wa kitanzania ni kufanya kazi kwa kuogopana. Huwa hatuweki sheria mbele au huwa hatuweki taratibu za kazi mbele bali huwa tunatanguliza mtu mbele halafu ndiyo mtu anafanya kazi kitu ambacho nchi nyingi zilizoendelea mtu huwa hatambuliki ila ni mfumo uliopo ndiyo humtofautisha mtu na kumtendea kadri mfumo unavyotaka.

Mfano, polisi anapotekeleza jukumu lake huku akiogopa asipomfurahisha mkuu wake basi atahamishwa kituo au hatapanda cheo, mtu kama huyu utategemea asiuwe mtanzania kwa ajili ya kumfurahisha Said Mwema au JK?

Ukweli watanzania tunahitaji tubadilike, turudie ule umoja na uungwana wa mtanzania ulioenziwa na Mwl, kwani kwa sasa serikali (polisi) ndiyo wanaoonekana kuwa wauwaji namba moja wa watanzania kuzidi hata majambazi. Ila kuna usemi Dhambi humfuata mtu, mfano aliyekuwa rais wa Misri.
 
siku chama tofauti na magamba kikichukua dola kitapata tabu sana kwa sababu hawa jamaa wamesha chakachuliwa na chama cha magamba.Magamba wataenda nao na kazi ya usalama wa taifa kuwa hatarini
 
"Nendeni nchi jirani au kwingine mkaangalie, mimi niliwahi kuingizwa ndani mchana kwenda kulala kutokana na hali mbaya ya usalama. Hapa kwetu Idara inafanya kazi kubwa, nchi imetulia," alizidi kuikingia kifua na kuwararua wakosoaji.

Katika kuonyesha jinsi idara hiyo inavyofanya kazi kwa ufanisi, Ngonyani alitaka Serikali kuongezea mishahara watumishi wa TISS na kuongeza, "hawa vijana tunashinda nao hapa hadi saa 4:00 usiku wanaangalia usalama halafu tunawasema hawafanyi kazi!"

"Tena nasema waongezewe mishara, vijana wanafanya kazi nzuri na kubwa ya kulinda nchi. Tunapaswa kuwapa nguvu siyo kuwalaumu siyo sahihi hata kidogo," alisisitiza Ngonyani (Maji Marefu)

Nionavyo:
Ikiwa jambo limesemwa na upinzani kwao ni Ovu hata kama kuna chembe za ukweli. Lakini likianzishwa na Mwenzao hata kama nikulisha sumu nchi watashangilia, Nakumbuka walivyomkingia kifua Chenge kwa Umoja wa maslahi ya Chama chao.

Nafika mbali zaidi BAE wanapokataa kuirudishia chenji serikali kwa harufu ya ufisadi serikalini Bunge limethibisha kwamba kweli serikali ni Mafisadi kwa kumkingia kifua Chenge ilhali ushahidi uko wazi.

HONGERENI USALAMA WA TAIFA KWA KULINDA AMANI YETU.
 
mkuu kama unakataa basi usingizi umekulevya!

Wewe Ndumbayeye ni mpuuzi kama Maji Marefu na wajinga wenzio wa CCM. Kazi ya kulinda ulinzi na usalama sio ya Usalama wa Taifa bali Jeshi la polisi. Huwa nakasirika kuona watu wasiojua lolote wakiropoka bila mpangilio.

Kwasababu tu jina ni Usalama wa Taifa haimaanishi wanajukumu la kulinda watu na mali zao. Kazi yao kikatiba ni kulinda mali asili za nchi. Wangetakiwa kuwa wa kwanza kuweka surveillance kwa wezi wa EPA, Richmond, Kagoda nk kwasababu ule ni uhujumu uchumi unaoangukia moja kwa moja kwao. Hata umeme kukatika hovyo ni treason ambayo tayari wangetafuta chanzo cha hilo tatizo na sio kuwakatikia viuno CCM kwenye kila jambo.

CCM nyie wapumbavu sana. ngoja nirudi bongo nichukue kadi ya CHADEMA na kuwaanzishia zogo la hoja. Mtanikoma nikirudi huko mwakani. Nyie ngojeni.
 
Maji marefu pale alikuwa akiufurahisha umm,aligeuza Bunge kijiwe tuuuu,hakuna la maana aliloongea,sasa kama aliambiwa alale mapema????watu wanahoj inakuwaje UHUJUMU UCHUMI umekithiri wakati wao UWT wapo??????,
Profesa Maji Marefu kumbe anaitwa Ngonyani? Ndo maana akili yake kama mbili 2.
 
Background yake inafanya nisimshangae sana. Maisha yake yote alikuwa anapiga ramli tu, can anything useful come out of that person? He is short sighted, kwa mtazamo wake mfupi anadhani taifa kuwa salama ni yeye kuwa na uwezo wa kuzunguka mjini bila kuulizwa ulizwa.

Hajui usalama wa taifa unapaswa kuhakikisha nchi inakuwa salama leo, na kuondoa uwezekano wa nchi kutokuwa na usalama siku za usoni. Tunalalamikia hili la pili, Future ya nchi iko rehani.
 
Mswada ukianzishwa na CCM wa kulisha watoto wote sumu chini ya miaka mitano utapita
 
"Nendeni nchi jirani au kwingine mkaangalie, mimi niliwahi kuingizwa ndani mchana kwenda kulala kutokana na hali mbaya ya usalama. Hapa kwetu Idara inafanya kazi kubwa, nchi imetulia," alizidi kuikingia kifua na kuwararua wakosoaji.

Katika kuonyesha jinsi idara hiyo inavyofanya kazi kwa ufanisi, Ngonyani alitaka Serikali kuongezea mishahara watumishi wa TISS na kuongeza, "hawa vijana tunashinda nao hapa hadi saa 4:00 usiku wanaangalia usalama halafu tunawasema hawafanyi kazi!"

"Tena nasema waongezewe mishara, vijana wanafanya kazi nzuri na kubwa ya kulinda nchi. Tunapaswa kuwapa nguvu siyo kuwalaumu siyo sahihi hata kidogo," alisisitiza Ngonyani (Maji Marefu)

Nionavyo:
Ikiwa jambo limesemwa na upinzani kwao ni Ovu hata kama kuna chembe za ukweli. Lakini likianzishwa na Mwenzao hata kama nikulisha sumu nchi watashangilia, Nakumbuka walivyomkingia kifua Chenge kwa Umoja wa maslahi ya Chama chao.

Nafika mbali zaidi BAE wanapokataa kuirudishia chenji serikali kwa harufu ya ufisadi serikalini Bunge limethibisha kwamba kweli serikali ni Mafisadi kwa kumkingia kifua Chenge ilhali ushahidi uko wazi.

HONGERENI USALAMA WA TAIFA KWA KULINDA AMANI YETU.
Binafsi namheshimu kuwa ni kiongozi aliyechaguliwa na wananchi wa jimbo lake pasipo kujali kiwango cha elimu ya dunia, bali uwezo wake kwa uwakilishi kwa wanajimbo lake.Pia ni mtaalamu wa mambo ya jadi,ambayo pia yana nafasi yake kwenye jamii ya kiafrika na mchango wake kwa waafrika ambao ni utamaduni wetu wa kiafrika ambao unaheshimika kwa ndani [Private] wakati nje [Public] wanaukebehi,haswa wasomi wenye malengo ya upotoshaji,na ambao ni wateja wakuu wa sekta hii.

Ni aibu kwa jamii haswa wanaoitwa waastaarabu [Civilized] kusema ni washiriki wa jadi hiyo,yani mambo ya kijadi.Na kwa kuwa ni mambo ambayo jamii imekuwa ikiyakwamisha kiuwazi na hivyo kuyapa kipaumbele kibinafsi na kuweka kinga kuwa si jambo la kufahamika kwa jamii kwa upana wake na mchango wake katika KUDIDIMIZA MAENDELEO YA TAIFA HILI.

Kwa upande wake DK Ngonyani aka Maji Marefu ni Mtaalamu kwenye fani yake ya JADI ambayo mimi kwenye upande huo sina ujuzi wowote na uelewa wa mambo yake, Tunafahamu uwepo wa mambo ya JADI kuwa yamekuwepo toka vizazi na uenda uwepo wake utaendelea kuwepo kututambulisha kuwa ndio moja ya uthibitisho kuwa tu Waafrika.Kwa waliopata kufika Nchi ya HAITI mambo hayo yako wazi kiasi kuwa kuna viini macho [Vodoo] zinauzwa waziwazi unachagua nini unataka,ni moja ya mambo makubwa yanayopatikana katika kanchi hako kadogo lakini kenye historia ya aina yake Duniani katika mambo ya Vodoo.

Hivyo sina cha kumlaumu kiongozi huyu kwa kuwa uwezo wake wa kuelewa [Intellectual ability] umefikia kikomo katika upana mzima wa hicho kinachoita USALAMA WA TAIFA,ingawa nae anao mchango wake mkubwa tu wa kuisaidia idala hiyo kama Mtanzania mwenye lengo jema la kuleta ustawi wa Watanzania.

Kwa waelevu [Intellectuals] huyu nae ana nafasi kubwa sana,tena katika kipindi hiki cha watendaji wengi katika utekelezaji wa majukumu yao wanapokutana na vitisho vya vodoo.

Asidharauliwe kwa fani yake bali apuuzwe kwa uelewa wake katika jambo zima la upeo wa mada husika kwa kuzingatia kuwa uwezo wake wa elimu umefikia kikomo.
 
Maji marefu hawezi kutofautisha polisi, jeshi(jw) na usalama wa taifa!.
Hii ni aibu kwa wana-korogwe kwa kumchagua huyu jamaa.Na hata hilo la kushindwa kutofautisha kati ya Polisi, Jeshi, UWT, Mgambo, Sungusungu, Polisi Jamii, Polisi Shirikishi n.k. ni kutokana na elimu yake ndogo ya Std 7.Iwepo sheria ya kudhibiti vilaza kama hawa kuingia bungeni.
 
Kama sio KGB Urusi ingekwisha na kutoweka duniani. tumeni vijana kwenda kujifunza jinsi usalama wa taifa unavyotakiwa kufanya kazi zake.
msione vyaelea ni wananchi chini ya ubantu wao.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom