Kuhatarisha usalama wa Taifa? Give me a Break!

Ili kuirudisha taasisi hii kwenye kazi /hadhi yake ya kulinda mali za nchi na watu wake kutoka kwa maadui wa ndani na nje ya nchi, kuna umuhimu wa kuiangalia upya sheria iliyounda UWT [TISS] with special emphasis ya majuku yake na jinsi mkuu wa taasisi hii anavyopatikana.

Hivi sasa mkuu wa hii taasisi anateuliwa na Rais kwa vigezo visivyoeleweka wazi wazi na mara nyingi the basisi of appointment ni nepotism ili akiwa kazini alinde maslahi ya yule aliyemteua hivyo basi kubadili mfumo wa uteuzi unaweza kusaidia kuirudishia intergrity ya TISS.
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Kwa nionavyo mimi, ww ni mmoja Wao ila umekuja kujaribu kuona tunawaonaje coz JFK ni kioo sana Kifupi ni kuwa u r nothing good for citizen wa kawaida but a threat kama vile nyie ndio wa kwanza kuwapora haki zao ktk uchaguzi, kusaidia wezi wa raslimali zetu kama wale twiga, kusaidia wauzaji unga ambao wanatuua kwa madawa hayo huku mkitumia kodi zetu. Kinauma sana kwa usaliti wenu

Mkuu uwemba mjenga nchi ni mwananchi mwenyewe na mbomoa nchi ni mwananchi mwenyewe,wewe unavyoona kwa mtizamo wako sikuzuii kwa kuwa siwezi kuingia ndani ya mawazo na kuyatoa huko unakoyapeleka ila thread yangu ilitaka kukushirikisha kama mwanajf [Great thinker] ndani ya Jamii Forum a place where people dare to talk openly for the good of the country and better for all.

Ila wewe umekataa kwa kutanguliza hisia na kuinyima haki yake nafasi yako ya kuwa great thinker kutafakari na kuchambua maswali ya thread hii kama walivyofanya wanajf ambao ni great thinker either wako Positive or Negative lakini hawakutazama kumzungumzia mtu binafsi bali issues za taasisi umma kama zilivyowakilisha, kwa nia njema ya kujenga kwa kuwa UTAKI UNATAKA NI LAZIMA IWEPO NA ITAENDELEA KUWEPO TAASISI HIYO KWA FAIDA YA UMMA.

Cha msingi ni sisi kupima na kukubaliana kama umma kuwa JE tunalidhika na utendaji wake na umma wote uwe na mtizamo chanya [Positive] na si hasi [Negative] kama ulio nao wewe.Niko/tupo kama wanajf hapa kama walivyo wengine humu kwa kusudio la kujenga siko/hatuko hapa kubomoa?Wewe hapa uko upande gani?Na kwa taarifa raia yoyote halali wa United Republic of Tanzania ni Mwanausalama wa Taifa lake!!!

Watu wa fani ya biashara za masoko [Marketers] wanasema hivi kama mteja/mwananchi [customer] akihudumiwa vizuri na kuondoka na bidhaa/huduma [Product or Service] akiwa AMELIZIKA [SATISFIED] basi mteja huyo atasambaza taarifa kwa WATU WENGINE WATATU atakaokutana nao kwamba bidhaa/huduma ile aliyonunua ni NZURI na BORA kwa matumizi husika.Lakini kama mteja huyo huyo akiondoka na bidhaa akiwa HAKULIZIKA [NOT SATISFIED] basi atawaambia WATU WENGINE TISA kuwa bidhaa/huduma ile SI BORA/HAIFAI.Accusation zako hazijengi kwa mwendo wako huo!!tunaitaji constructive idea kutibu sio kubomoa.
 
Unajua TISS wengine wanafikiri watu hawajui majukumu yaTISS, Tanzania ni kanchi kadooo saana TZ, watu wanajua majukumu ya CIA, KGB,MOSAD na mashirika makubwa mengine ya kijasusi, TISS kwa vyovyote wameiga huko!Sasa visemina vya wanaTISS wanaambiwa labda! Watanzania wengine hawaju majukumuya TISS, Watu wanafahamu na wanawaangalia mnavyochemsha!

Kwa taarifa yako TISS number 1 sio Rais ila ni akili kamili ya mtu binafsi(Mwenye akili kamili), ninavyosema kamili ni utashi wa mtu mwenye akili nyingialiyekamilika! Hujui hilo? Mawazo kama haya ndio yana haribu utendaji wa TISS,Tunajua TISS wanafikili wao ndio, wanatakiwa kuweka Rais, Kuchaguwa mawazir,kuchagulia watu wabungei on which wanaweka watu wasio na uwezo, kwa kuwa TISS 1yao haiko okay!

jinsi ilivyo kwa utashi kamili na akili zetu kamili i mean TISS 1, mnadanganywa kuwa watu hawafahamu, ukiclaim utaamini, ila ukiwa na TISS1 Kichwani utaelewa kitu ninacho kisema,
 
Kwa kweli ndugu zangu mmenigusa kwenye jambo moja la msingi ambalo nimekuwa nikijiuliza kila siku, hivi hii idara ina muhimu gani kwa taifa letu kwa
sasa fuatilia vizuri wizi wa pesa EPA,DEEP GREEN FINANCE,MEREMETA,RICHMOND na madudu mengine mengi baadhi ya maafisa wa idara hii wanausika moja kwa moja, kuna wizi wa mizigo bandarini wanahusika na ndiyo wanatumika. Haiwezekani matukio makubwa ya wizi na mikataba feki ifanyike bila baraka zao utaweza ni mpaka uwe mtu wao. Ikifika mahali rais anasema haijui kagoda kampuni iliyoiba pesa BOT halafu unasema una usalama wa taifa ni bora kuifuta taasisi hii isiendelee kutumia hela ya walipa kodi yetu bure hawatusaidii chochote wizi mtupu.
 
Unajua TISS wengine wanafikiri watu hawajui majukumu yaTISS, Tanzania ni kanchi kadooo saana TZ, watu wanajua majukumu ya CIA, KGB,MOSAD na mashirika makubwa mengine ya kijasusi, TISS kwa vyovyote wameiga huko!Sasa visemina vya wanaTISS wanaambiwa labda! Watanzania wengine hawaju majukumuya TISS, Watu wanafahamu na wanawaangalia mnavyochemsha!

Kwa taarifa yako TISS number 1 sio Rais ila ni akili kamili ya mtu binafsi(Mwenye akili kamili), ninavyosema kamili ni utashi wa mtu mwenye akili nyingialiyekamilika! Hujui hilo? Mawazo kama haya ndio yana haribu utendaji wa TISS,Tunajua TISS wanafikili wao ndio, wanatakiwa kuweka Rais, Kuchaguwa mawazir,kuchagulia watu wabungei on which wanaweka watu wasio na uwezo, kwa kuwa TISS 1yao haiko okay!

jinsi ilivyo kwa utashi kamili na akili zetu kamili i mean TISS 1, mnadanganywa kuwa watu hawafahamu, ukiclaim utaamini, ila ukiwa na TISS1 Kichwani utaelewa kitu ninacho kisema,

Tunajua wenzenu wanavyoshabikia vyombo vyao katika kulinda mali zao na Taifa lao kwa ujumla na kuliweka Taifa lao kwenye ramani ya Duniani,uwezi kuwa raia wa Marekani mwenye upeo wa wastani asijue CIA iko kwa kazi gani na ndio maana wako tayri kuitetea popote pale nani na nje ya mipaka yao.Vivyo hivyo Waisrael na MOSAD nao kwa nguvu ile ile ya sawa ya wamarekani wananchi wanajengwa kuthamini nguvu na uwezo wa vyombo vyao vya umma kuwapa msaada wa kuwa wanajua dhahili mashirika hayo yako kwa faida ya Taifa lao.Je sisi watanzania kwanini tujijenge kweye sura hasi [negative] kifanyike nini nasi kila anaezaliwa ndani ya Tanzania anakuwa mzalendo wa Taifa lake kwa kuwa mwishi wa yote kila ria ni Mwanausalama wa Taifa lake kadri ninavyoamini mimi kwa upeo wangu.
 
Ninaelewa nchi nyingi ambazo ili ufanyiwe vetting kuwa katika Shirika / Taasisi ya Usalama wa Taifa si tu kuwa wewe ni Mwaminifu na Mzalendo kwelikweli bali lazima uwe na AKILI MAONO NA PIA AKILI NYINGI (uwezo wa kutambua, kuhisi na kushughulikia mambo kwa ufanisi zaidi kuliko binadamu wengine wa kawaida).

Sasa kila aliye TISS sasa anayenisoma hapa ajipime hapo na aseme na roho yake kama anafaa kuwa humo!!

Idara hii ni ya muhimu sana na niseme bado inafanya kazi nzuri lakini ingetakuwa kuwa inafanya zaidi ya hapo kwa sababu ajira ya baadhi ya walioko humo hawana hizo sifa zinazotakiwa au wamekiuka na kukosa uzalendo.

Hata kama wewe ni mkubwa wangu ukinipa amri ambayo inakiuka uzalendo na maendeleo ya Mtanzania niko tayari kukukatalia na huwezi nifanya chochote! Kiapo chao na cha Mabosi wao wote hatimaye ni kuilinda na kuitetea KATIBA YA NCHI. Sasa nionyeshe ambapo Katiba inasema kuwa kuna bosi wako (haijalishi ana rank gani )ambaye yuko juu ya Katiba?

Tuwasaidie ili TISS iweze kuwa na mabadiliko, iwe ya kisasa na yenye ufanisi zaidi. Na zaidi ya yote wapewe meno ya kungáta !!! sio kuchunguza tu na kuripoti!
 
1: Je Usalama wa Taifa ni haki ya Serikali au ni Haki ya Umma?
JIBU- Usalama wa taifa ni haki ya umma unaoratibiwa na kuongozwa na serikali kwa niaba ya umma.

2: Je raia wa kawaida wa Tanzania kujua taarifa za msingi kuhusu kazi [Basic Information] ya usalama wa Taifa lake ni kosa?
JIBU - Sio kosa kwa raia kujua kazi za usalama wa taifa, ambayo ni kulinda na kusimamia usalama wa nchi nje na ndani ya mipaka ya nchi.


3: Je nini objectives and role za Usalama wa Taifa kwa Serikali inayokuwa Madarakani?
JIBU; Usalama wa taifa upo blank katika role zilizo nje ya kulinda na kusimamia usalama wa nchi, lakini utatekeleza role inayopewa na serikali kwa niaba ya umma, na hapa ndiyo serikali iliyopo madarakani huchukua fursa ya kutumia TISS kujiwekea mizizi.

4: Je nini objective and role za Usalama wa Taifa kwa Wananchi yani Umma wa Watanzania.
JIBU: Ni kuwahakikishia usalama umma wa watanzania sasa na baadaye.


5: Je majukumu na kazi za Usalama wa Taifa zinapaswa kuogopwa [Tisha] Wananchi au zinapaswa kuheshimiwa na hata kusaidiwa na raia wema [wazalendo] kama njia sahihi ya kulinda Taifa na mali zake?
JIBU; Sheria iliyopo inayounda usalama wa taifa haina direct link kati ya raia na idara hii, kwani sheria hii inadhani rai anaweza kuwasilisha anachoona hatarishi kwa idara nyingine kama polisi n.k
! Yes, kwa raia na asiye raia inamlazimu aiogope idara hii endapo atashiriki kutoa siri za nchi, atahatarisha usalama wa nchi au/na viongozi wakuu wa nchi, kufanya jinai ambazo zinafuatiliwa na idara hii, tofauti na uvunjifu wa hivyo idara hiyo haipaswi kuogopwa.

#CIA kwa marekani ni kitengo cha kijasusi kinacho linda na ktafuta masilahi yao nje ya nchi, mbali ya kulinda usalama wa nchi yao. Wanayo FBI na idara yao ya usalama pia. Kuna Mi5 na Mi6 in UK, mbali na inteligncy agncy dept nchini mwao.
-Ndiyo maana nimeshauri kuwa badala ya TISS kunyooshewa kidole kwa kufanya shughuli wasizo tarajiwa na umma, au kutofanya majukumu yaliyo tarajiwa na umma, ni vyema turekebishe kwanza sheria inayoiunda idara yenyewe.
-Nafikiri katika muundo wa katiba, tupendekeze Tiss iundwe na kitengo cha biashara na sheria za kimataifa, propaganda na masoko, halafu na usalama wa nchi kwa maana ya ulinzi. Katika idara ya propaganda Tiss iweke Contacts zake na baadhi ya shughuli zao kwa wananchi via websites n.k!

Kibanga Msese
 
Ninapofuatilia mada hii, nakumbuka usemi usemao ukicheka na nyani utavuna mabua na mchelea mwana hulia mwenyewe. Hivi ndugu zangu watanzania wenzangu, mimi binafsi sioni hata sababu ya kukichokonoa saaaaaaaaaana chombo hiki mhimu sana kwa usalama wa nchi yetu.

Ni kweli kuwa huenda wapo wachache wa members wake ambao siyo diligent, hii haimaanishi kuwa chombo kizima ni rotten! Bado usalama wa taifa ndicho chombo pekee kinachosimamia mstakabali wa taifa hili. Wengi wetu hatujui majukumu yao na pengine ndiyo maana hata tunadodosa weeeeee, eti kwa kulinganisha na intelligenge agency ya Kenya!

Tukumbuke kuwa kila nchi ina mfumo wake wa kuendesha shughuli za kijasusi na si kwambwa kwasababu wakenya wameainisha majukumu ya intelligence agency yao kwa uwazi basi na Tanzania ifanye hivyo, hapana. Ninashauri kuwa tuchezee vitu na idara zote lakini hii hebu tuiache ieendelee na kazi zake. Huu ndiyo moyo wa nchi yoyote ile duniani, tunapokichezea chombo hiki tunachezea hatima ya taifa letu.

Ndugu zangu hebu tuwe na uzalendo, tuwaamini hawa jamaa kuwa hawalali usiku kucha kwaajili yetu. Mimi kitaaluma ni mwalimu lakini nina ndugu rafiki yangu anayefanya kazi TISS, ninajua namna jamaa anavyokuwa busy na kazi kiasi hata familia yake hakai nayo muda mwingi. Kiukweli jamaa wanapiga kazi jamani.
 
Tunajua wenzenu wanavyoshabikia vyombo vyao katika kulinda mali zao na Taifa lao kwa ujumla na kuliweka Taifa lao kwenye ramani ya Duniani,uwezi kuwa raia wa Marekani mwenye upeo wa wastani asijue CIA iko kwa kazi gani na ndio maana wako tayri kuitetea popote pale nani na nje ya mipaka yao.Vivyo hivyo Waisrael na MOSAD nao kwa nguvu ile ile ya sawa ya wamarekani wananchi wanajengwa kuthamini nguvu na uwezo wa vyombo vyao vya umma kuwapa msaada wa kuwa wanajua dhahili mashirika hayo yako kwa faida ya Taifa lao.Je sisi watanzania kwanini tujijenge kweye sura hasi [negative] kifanyike nini nasi kila anaezaliwa ndani ya Tanzania anakuwa mzalendo wa Taifa lake kwa kuwa mwishi wa yote kila ria ni Mwanausalama wa Taifa lake kadri ninavyoamini mimi kwa upeo wangu.

Mkuu kama unakumbuka mabadiliko aliyofanya Mkapa, alifanya decision making zote kuhusu operation ya issue kubwa za nchi zinafanywa na political establishment, wao TISS ni kutekeleza tu yale wanayoambiwa na politicians. Kama kweli TISS wangekuwa wanafanya utekekelezaji wenyewe mambo yasingekuwa kama yalivyo sasa, wako kama aylivyo kwa sababu sio TISS wanafanya hivyo. TISS wanaripoti kwa TISS 1 yaani Rais na yeye ndiye anayewateua kwenye nyadhifa mbalimbali, na sio kuwa Rais anaripoti kwa TISS.

Sasa ni kipindi amcho TISS ina opportunity kubwa ya kujenga imani yake kwa watanzania, lakini haiwezi kufanya hivyo kwa kuwa ya sasa imegawanyika mara mbili au tatu, (Tiss-Mwang'onda, Tiss Kitine na Tiss Othmam) nayo iko very politicised, sio ile iliyokuwa inafahamika, iliyokuwa inafanya kazi ya usalama wa taifa. sasa hivi majibu mpaka yanafanya hata uhalifu karibu na Tiss HQ. au hata ndani ya HQ kwenyewe zamani ujinga huo haukuwepo.
 
Naomba kujua jaman...maana tangu nizaliwe nachosikia na ninachokijua ni kuwa TISS inahusika zaidi na
1.Kuiba kura halali za wananchi hasa wakati wa uchaguzi wa wabunge na rais na kuzipachika kwa CCM wakishirikiana na tume ya wachakachuaji(tume ya uchaguzi

2.Kupeleleza taarifa za siri kutoka kwa viongozi wa kisiasa mf.kuweka vinasa sauti kwenye hoteli zao

3.Kupanga na kutekeleza mauaji ya viongozi wanaokosoa serikali mf kombe,kolimba nk

4.Kuuhadaa umma wa watanzania kuwa viongozi wanaoshukiwa na makosa makubwa ya jinai wamefariki mfano Balali,Dito

Naomba kujua kama hizi ndio kazi zao msingi na wanatumia kodi zetu kuzitekeleza na zipo kwa mujibu wa sheria,kama sio hizi,basi kazi zao hasa ni nini?
 
pole kwa ulimbukeni wako na kutokujua kwako majukumu ya chombo hicho.... hakuna hata moja kati ya hayo ni jukumu lake. Soma sheria ya TISS ya 1996 inapatikana kwenye mtandao.

hali yote hii imekutokea kwa sababu ya uwezo wako wa kuelewa mabo na kuchanganua bila kushirisha siasa kwenye mambo makuu ya kitaifa
 
pole kwa ulimbukeni wako na kutokujua kwako majukumu ya chombo hicho.... hakuna hata moja kati ya hayo ni jukumu lake. Soma sheria ya TISS ya 1966 inapatikana kwenye mtandao
Hii sheria bado iko valid kweli even after 46 years? Labda tu cha kumkumbusha mtoa mada ni kuwa kazi kubwa ya Idara ya Usalama wa Taifa ni KUHAKIKISHA TAIFA LIKO SALAMA. Baaaaasi!!!!!!!!
 
Mkuu nimekuunga mkono. Lakini, kama utasoma sheria iya kuunda TISS, utaona ni jinsi gari rais amepewa madaraka makubwa katika kuteua na kusimamia utendaji wa idara hiyo.

Sasa kama rais akichagua shoga yake kuongoza idara hiyo, unategemea atampinga? Si ndio maana TISS wanaaacha majukumu yao ya msingi na kuanza kushughulika na mgomo wa madaktari na CHADEMA!

Jamani, piganieni mabadiliko ya sheria ya kuunda TISS.
 
Back
Top Bottom