JamiiForums
JF Official Account
- Nov 9, 2006
- 6,227
- 5,267
Baija Bolobi said:Madudu mengi na ya hatari yanayotokea katika siasa za nchi yetu yanaashiria kuwa idara yetu ya Usalama wa Taifa imefika mwisho kiutendaji. Ebu ona:-
-Rais akamteua Chenge baada ya kuvunjwa kwa Baraza la mawaziri. Watu wakapiga kelele, yeye akakaidi. Baada ya muda mfupi akalazimika kumwondoa kwa aibu!
-Nape na Malisa wakavutana kuhusu uongozi wa UVCCM; Rais akawatosa wote na kumchukua Masauni. Amegundulika alifoji umri, akaondoka, lakini aibu ikabaki kwa Rais. Hakuna aliyewajibishwa katika idara ya Usalama.
-Sasa tunaambiwa Bashe si raia. Amekuwa katika nafasi nyingi ikiwamo NEC. Chiligati anasema walipitiwa tu. Wamepitiwa mangapi?
La kujiuliza, hivi tuna ile Idara ya Usalama wa Taifa au sasa ni Idara ya Uhasama wa Taifa? Kinachoonekana kujengeka sasa ni kuwa uhasama katika mahusiano ya watawala ni mkubwa sana. Leteni maoni ya nini mwisho wa uhasama huu.
Kwa wasiojua majukumu ya taasisi hii wa-download attachment hii:
Kazi ya Usalama wa Taifa pia imegawika katika mafungu haya:
1. Kulinda Viongozi Wakuu- Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, na Viongozi wa staafu wa ngazi hizo, (pamoja na kulinda viongozi wakuu wa UWT km mkurugenzi wake mkuu).
2. Kukusanya taarifa za usalama kwa lengo la kujua mood ya wananchi kuhusiana na kila tukio linalotokea ama lisilotokea nchini ili kuiwezesha serikali kufanya maamuzi sahihi, na mara zote kulinda maslahi ya taifa.
3. Kutafuta intelligensia kutoka nje ya mipaka zenye kuiwezesha nchi kujua siri za ndani za nchi nyingine, rafiki ama shindani, ama hasimu, ili ziweze kuisaidia kufikia maamuzi sahihi (informed decisions) kuhusiana na mambo mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.
Kufanya mauaji ni sehemu ya kazi ya TISS na idara yoyote ile ya kijasusi katika nchi mbalimbali ila haiwi wazi inaweza kufanyika kwa kuwekewa sumu ambayo mtu anaweza kufa hapohapo au baada ya siku tatu au hata zaidi kutegemea na aina ya sumu na kiwango chake na pia kuna ajali ya gari ambayo inaweza kuonekana kama ya kawaida kabisa au ya kusababishwa na aina ya hila yoyote ile kama ilivyotokea kwa Diana ionekane alikuwa anawakimbia wapiga picha na kuna ambayo wengi wamezoea ambayo ni ya kumfuata mlengwa na kumpiga risasi mahali popote nyumbani kwake, kwenye mkutano au sehemu yoyote inapopatikana nafasi hiyo.
Ni kweli kuwa kazi ya usalama wa Taifa ni kulinda masilahi ya Taifa lakini na raia wakeila kuna nyakati huwa ni kwaajili ya kulinda wakubwa wachache au serikali husika na masilahi yake na hapa inaweza kufikia hata kuua kiongozi mkubwa na mwandamizi au hata kundi la watu kwa mfano aliyekua waziri mkuu wa Israel Yitzak Rabin huyu alipigwa risasi na ikasemekana ni raia ila ukweli ulivyo yule hakuwa raia wa kawaida alikuwa alinda kile ambacho Waisrael wanakiamini siku zote na PM. Yeyote anapochukua nchi ile anatakiwa akifuate akikiuka siyo mwenzao tena atatolewa kafara kwa namna yoyote ile kuhakikisha Israel inabaki kuwa ilivyo kama wanavyoamini wayahudi na ni wakatili mawako tayari kuona mwarabu anapata anachokitaka okay basi tufanye hivi kule midle east kuna waarabu kibao tena ambao ni wazaliwa Israel kwa nini asitumwe kwenda kufanya yale mauaji lakini yakafanywa na myahudi mwenzake? Angalia wengine kama Rafik Harir wa Syria, na hata marehemu Kombe aliuawa na Polisi wakimtuhumu kuwa ni Jambazi pamoja na kuwa alijitambulisha kuwa yeye ni nani!
Ngoja nikupe mfano mwingine ambao huu utawachanganya wengi na wavivu wa kusoma na kuchunguza tutawaacha mbali sana WTC huko New York ambapo walikufa zaidi ya watu 3000 na kuwasingizia magaidi na kuzua vita ambavyo vimedhulumu maisha ya wanyonge wengi bila kujali aina ya dini kabila au hata utaifa maana walikufa wamarekani na waisilamu wa Iraq na kwingineko duniani na hata kumnyonga Sadam na hali ikawa mbaya Iraq kuliko alivyokuwepo Sadam Hussein na pia kubadilisha mambo mengi duniani ikiwemo kuvujiana heshima na kutuhumiana ugaidi kwa kumpima mtu kwa itikadi yake tu na hata kumdhalilisha
Ni matumain yangu humu JF. Kuna wakandarasi ambao wanaweza kutoa ufafanuzi wa jinsi gorofa linaweza kujengwa namna gani halafu ligongwe na ndege lishuke kama ice cream juani na kuwa vumbi na wanahabari watoe picha ambazo nyingi zinafanana na hasa ukizingatia kwa wenzetu suala TEKNOHAMA wako mbali wana vyombo vingi vya kudugundua mambo mengi HEBU WANAJF.TUSIWE WATU WA MALUMBANO MENGI HUMU NDANI TUPATE MUDA WA KUSOMA NA KUCHUNGUZA MAMBO KWA KINA UTANIELEWA NASEMA NINI HAYA NINAYOYANGEA HUMU
ANGALIZO: Hapa simaanishi magaidi hawapo laa ila magaidi wapo na wanafanya kazi zao na wengine kibao tunao hata hapa kwetu tena wanajishikamanisha vizuri sana wakubwa wa serikali zetu kwa kuifadhili na kutoa michango mbalimbali kwenye serikali na jamii kwa ujumla na ukijidai kuwafuatilia yaweza kukuta makubwa maana baadhi ya wakubwa wana masilahi yao huko.
Hivyo basi moja ya kazi ya idara yoyote ya ujajusi ni kufanya ujasusi na project za siri katika nchi mbalimbali tatizo ni kuwa hapa kwetu na baadhi ya nchi nyingi zinatumia vibaya Idara hizo badala ya kujiletea maendeleo kama Nchi za urusi na Asia na hivyo sehemu kubwa kuishia kulinda kundi la watu wachache na madaraka yao maana hao ndiyo wenye uwezo wa kumpoint mkurugenzi na wengine katika kazi nyeti za serikali iliyoko madarakani.
Idara hii ina watu wengi sana tena wengine hawathaminiki katika jamii kabisa na wanafanya kazi kizalendo zaidi na kutanguliza masilahi ya Taifa mbele lakini wanakwamishwa na urasimu na kutokuchukuliwa hatua kwa wahusika (watu hatarishi wa usalama) na ikumbukwe kuwa idara hizi kwenye nchi nyingi huingia maeneo mengi sana mbalimbali unaweza kumkuta waziri,Mchungaji, sheikhe, mhadhiri,mwana habari, mfagiaji, dereva wa dalala au tax, fundi viatu, mwalimu, padre,mwanamuziki, makahaba na kwa hapa Dsm. Hata muuza samaki (pweza) kwenye sinia anaweza akawa na akafanya kazi kwa ufanisi mzuri kabisa ila mwana usalama wa kweli hana na habebi bango la kujitangaza waziwazi kuwa yeye ni mwana usalama na ndiyo maana ukimwona mtu anajigamba sana ujue huyo ni feki na ana masilahi yake binafsi ukiacha wale ambao wanafanya kazi za wazi za kuwalinda viongozi Top5 kingine kazi ya kukamata wahalifu mara nyingi huwa ni kazi ya polisi na kama kuna ofisa usalam akitaka kukamata anaweza kukamata kama raia mwingine yeyote kulingana na sheria za nchi MZISOME! raia anaweza kumkamata mhalifu ila ikiwa ni lazima sana kwa mwanausalama kufanya hivyo kimabavu anaweza kufanya hivyo akishirikiana na polisi na vyombo vingine vya dola kama vile PCCB, Uhamiaji, TFDA, Jeshi nk. TENA IKUMBUKWE KUWA OFISA WA IDARA YA USALAMA WA TAIFA HAKAMATI MVUTA BANGI MARA NYINGI ATAKUWA RAFIKI YAKE ILI AWEZE KUJUA BANGI INALIMWA WAPI NA KUPELEKWA KUUZWA WAPI HAWAKURUPUKI TU. Lakini sio mbwembwe ambazo watu wengi wanapenda kujionyesha nazo kuwa wao ni wana usalama na kuwakera wengine.
Kwa kwa kuongezea ni kuwa hakuna jambo lolote la hasara na aibu ambalo linaipata nchi hii ambalo vyombo husika na Rais mwenyewe hana Taarifa nalo kila kitu kinajulikana na kutolewa ufanunuzi na hasra zake LAKINI KIKUBWA NI KWAMBA HUPUZWA KWANI WASIKA WENGI HUWA NI MASWAIHIBA WA RAIS AU WAZIRI MHUSIKA NA HATA VIONGOZI WAANDAMIZI Na ndiyo maana mara nyingi Rais anashindwa kuchukua maamuzi magumu maana yanaweza kumgusa yeye mwaneyewe au yalianzia kwake mwenyewe. Lakini idara ina heshima zake na kukusanya taarifa mbalimbali za kiulinzi na usalama na hata kiuchumi lakini hazitiliwi maanani zinawekwa kapuni na kama unabisha mtafute rafiki yako yeyote wa karibu muulize kiundani kama hawahui mambo yanyoendela nchi hii lakini hana namna ya kufanya.
OMBI NA TAHADHARI:
IDARA HII ISIBEZWE NA KULAUMIWA KWA KUWABEBA WANASIASA NA KUTOKUFANYA KAZI YAKE IPASAVYO NI KWA SABABU YA MFUMO WENYEWE ULIVYO KAMA NDANI YA JESHI NA IKUBUKWE KWA WALE WALIOPITIA HOJA ZANGU ZA MWANZO NILIONYESHA JINSI WANAVYOTOA KAZI KUANZIA NATIONAL SERVICE KWA MAANA HIYO IDARA HII NI PARAMILITARY NA KUNA CHAN OF COMMAND AMBAYO KILA MTU ANAIFUTA KULINGA NA ORDER ALIYOPEWA NA AMIRI JESHI MKUU WA MAJESHI NI RAIS MWENYEWE WA JMT.
ILA NA WAO WAMECHOKA NA UOVO UNAOENDELEA SERIKALINI MPAKA HUKO KWENYE MAJESHI NA HII NI HATARI SANA INAWEZA KUJA KULETA MACHUFUKO SIKU ZA USONI KAMA IVORY COAST NA KWINGINEKO MAANA HAWANA UHAKIKA NA MAISHA YAO YA BAADAYE YA WATOTO WAO NA NDUGU ZAO MAANA KILA KITU KIZURI NA CHENYE MASILAHI KIMESHIKWA NA WAKUBWA NA WAJANJA WACHACHE.