Bandiwe
JF-Expert Member
- Oct 19, 2013
- 9,530
- 3,553
Am here to stay acha porojo zako !Tumeona wanyama wakubwa wakubwa wakihamishwa kutoka sehemu mbalimbali na kupelekwa huko Burigi.
Pori la Burigi lipo ngara ambayo imepakana na Rwanda.
Kama tunavyojua, Rwanda ina wanyama wachache sana kulinganisha na Tanzania, kwa hiyo move hii ya Tanzania inaweza kusaidia Rwanda sasa kupata Wanyama na kukuza utalii.
Kama mnavyojua, Wanyama hawajui mipaka ya Kisiasa kwa hiyo msishangae wakaamua kuishi popote, Tanzania hata Rwanda, huwezi kuwazuia.
Binafsi naona kwa move hii ya kuhamishia Wanyama huko Ngara ni bonge la Neema kwa Kagame.
Mimi nilifikiri kwanza kabla ya kupeleka wanyama mapori mengine basi tuboreshe kwanza vyanzo vya utalii wa wanyama tulivyokuwa navyo, tuboreshe huduma za mahoteli, tujenge viwanja bora n.k
Lakini hii ya kuhamishia wanyama Ngara, tunaenda kuwasaidia Wanyarwanda nao kupata chanzo cha utalii kwa gharama ya wanyama wetu, Je tumejiandaa kwa ushindani?