Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 2,397
- 3,884
Moja ya jambo muhimu katik biashara ni upekee wa bidhaa yako. Watu hawaji kununua kwako bidhaa au huduma kwa sababu ya huruma, ni kwa sababu una kitu wanachohitaji na unakitoa kwa ubora kuliko washindani wako.
Kwa miaka kadhaa huko nyuma Tanzania tumetokea kugawa wanyama wetu kwa mataifa mbalimbali. Inawezekana hii ilifanywa kukuza mahusiano na nchi hizo, inawezekana imefanywa tu kwa sababu ya tamaa ya wachache. Inawezekana pia tulilipwa fidia.
Ila tujiulize tunapoteza nini kwa kufanya hivyo? Je mtalii akiambiwa achague kwenda safari Dubai, sehemu yenye miundombinu na huduma bora kutuzidi, kweli atachagua kuja kwetu aache kule? Tena ukizingatia hawa hawa tunaowapa wanyama tunawapa pia nafasi ya kufungua mahoteli katika mbuga zetu na kuwa agents wa utalii, hawawezi kuwa wanavutia kuwapeleka watalii kwao badala ya kuwaleta huku kwetu?
Ujangili tumeshindwa pia kuudhibiti kwa maana hiyo kuna uwezekano kuna wanyama watapotea huku kwetu ila watakuwepo huko tulipowagawa. Hizi lawama atazibeba nani?
Kwa mtazamo wangu, dunia inahitaji mashirikiano kati ya nchi na nchi ila ni muhimu sana kumaintain competitive advantage uliyo nayo katika uchumi na biashara. Uzalendo unaanzia hapo.