Kama Magofu na Beaches ndio huvutia mamilioni ya watu Tunisia, Morocco & Egypt. Je, kuna haja gani ya kufuta vijiji kupanua mbuga za Wanyama?

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,048
49,731
Nimekuwa najiuliza swali na kuharibu kutafiti ni mambo yapi au vitu gani spesho ambavyo vinavuta Mamilioni ya watalii kutoka Nchi mbalimbali Duniani Kutembelea Nchi za Kaskazini mwa Afrika za Egypt, Morocco na Tunisia? Watu wanatoka Duniani kote kwenda kutumia mabilioni ya pesa huko, Kunani hasa? Nikatafuta kufahamu.

Yaani majibu niliyopata yamenishangaza sana.Kwamba kinachowapeleka watu kwenye hizo Nchi ni Magofu ya kale (Majengo chakavu ya tawala za kale),beaches na labda eti Pyramids.

Nikajiuliza zaidi na kuchimba ndani ni mambo hayo tu? Na Je idadi kubwa ya Watalii wanatoka wapi? For the case of Tunisia wengi wanatoka Algeria na Libya, Kwa Morocco wanatoka Ulaya hasa Spain na Egypt Kwa sehemu kubwa ndio wanatoka maeneo mbalimbali.

Maswali Yanayonitatiza.

Kwamba Utalii ni Magofu na Beaches na sio Nyumbu au vifaru. Yaani watu Wana shida na Magofu zaidi kuliko Wanyama ambao kutwa kucha tunafunga watu Wetu eti ni vivutio vya Utalii.

Nikaendekea kutafakari na kujiuliza, mbona Tanzania tuna Magofu ya kale ya kutosha tuu mfano Stonetown Zanzibar,Bagamoyo, Kilwa, Ismani nk? Hao Watalii mbona hatuwaoni Kwa Wingi? Kwani Magofu wanayokuja kuangalia yanatakiwa kuwaje?

Mbona Tanznaia tuna beaches nzuri kushinda wao na kubwa kuanzia Mtwara Hadi Tanga? Zanzibar yote na Maziwa yote Makuu? Mbona hatuwaoni wakija Kwa Wingi Kuchezea,kupiga picha na kuingiza aunkufanya matamasha?

Hata South Africa ambao nao Wana Wanyama kama sisi ,idadi kubwa ya Watalii wao hawaendi kuangalia Wanyama Bali ni majirani wanaokuja Kwa Ajili ya biashara,fukwe na wachache ndio wanakuja Kwa Ajili ya Wanyama.

Maswali.
Kama Utalii unaobamba Duniani kote hauhusiani na Wanyama Wala misitu Kwa nini mambo haya yanafanyika?

1. Kwa nini Serikali inafuata Vijiji,kunyang'anya watu maeneo Kwa kisingizio Cha Uhifadhi na kuwa kivutil Cha Utalii ambacho sio kitu watalii wanakipenda?

2. Kwa nini tutumie mabilioni ya pesa kuhamishia watu kwenye maeneo Yao Kwa kisingizio Cha Utalii ambao sio bidhaa ambayo Watalii wanahitaji?

3. Kwa nini tuwafunge watu Wetu miaka jela Kwa sababu eti za kukutwa na vipande vya Wanyama pori,tuwalipishe faini,mazao Yao yanaharibiaa na Wanyama nk? Huo Uhifadhi una faidia ipi Kwa jamii wakati sio kati ya mazao ya Utalii yenye soko Duniani?

Hitimisho.
Ni vyema Serikali ikajitafakari Kwa hayo niliyoeleza hapo Juu Kwa sababu tunakomaa na kuumiza jamii yetu Kwa vitu ambavyo havina faida Kwa watu Wetu labda kuwafaidisha Wazungu.

Kama tunataka Utalii tuweke Nguvu kwenye mazao ambayo Watalii wanataka na sio kuhangaika na Wanyama.

Tujiulize Kwa nini tuna fukwe nyingi na Magofu ya kutosha lakini hakuna watalii wa maana wanaokuja.

Mwisho tukuzee Utalii wa ndani Kwa Kuinua uchumi wa watu na pia tuishi vyema na Nchi Majirani na kukitangaza kwao maana hao ndio Watalii Wetu wa uhakika badala ya kuhangaika na WA Ulaya ambao wanaenda Kwa majirani zao.eg Cuba, Malta nk

View: https://twitter.com/AfricaFactsZone/status/1751212698614858037?t=PPV0rMBdm6kh-f_vFn_oXg&s=19

Wenye Magofu na fukwe wanapata watalii kati ya Milioni 9-15 na wenye Mbuga za Wanyama Wana pata watalii kati ya Milioni 1-5.Tutumie akili.
 
Kila nchi ipo unique kiutalii na dunia nzima haiwezi kuwa na utalii wa aina moja. Strength yetu tanzania ni hiyo touristic adventure ya mbugani haswa kwa upande wa bara

Kwa hiyo kama tunataka beach tourism na masalia ya kale, bado inawezekana tu kuifanyia promo pasipo kuathiri utalii wa mbugani

Kingine hizi mbuga ni vyema zikalindwa na kubakia ili kuzuia upotevu wa species flani za wanyama na mimea lakini pia, kutokana na uharibu wa mazingira na ubadilikaji wa tabia ya nchi, misitu na mapori ya hifadhi bado ni muhimu sana ili kuipungua athari yake.

Kumbuka sisi na wanyama wote tunahitaji maji na kikubwa zaidi, bado nchi yetu inategemea umeme wa maji ambao kwa kiasi flani unategemea mito inayohifadhiwa kwa kukatishaa katika hizo mbuga zinazohifadhiwa.

Kwa hiyo Tanzania bado ni kubwa sana hivyo, yaache baadhi ya maeneo na wanyama wahifadhiwe katika asili yao maana nao wana stahiki ya kuenjoy dunia kama wewe
 
Unatumiaje Nguvu kwenye kitu kisicho na manufaa ya Moja kwa Moja kwako na ambacho by the way hata hakihitajiki sana huko kwenye soko la Utalii?
 
Wanyama wanahamishika na ndio maana kila miji duniani wana zoo zao na wanyama wamewatoa sehemu wanakopatikana
Kama namuona nyoka kwenye zoo nifunge safari ya nini kuja kumtafuta huko?
Siku hizi kuna watu wana hifadhi zao za wanyama wala majani wakizunguka kwenye maeneo makubwa na hili nimeona 🇬🇧 sana

Waarabu pia wamebeba sana
Kila nikiona fukwe zetu zilivyo chafu na watu wakijisaidia huko huwa nashangaa sana
miji niliyotembea unaweza kukuta ni jangwa lakini wamezika fukwe kwa concrete na mawe makubwa sana na kusawazisha kujenga mahoteli ya maana
Mtalii anataka kwanza aje apumzike sehemu tulivu isiyo na kelele na pia amani itawale na kuombwa ombwa hawapendi
Hili nimeona askari wa zanzibar jamaa wanajua kuomba aisee
Hata Bara lazima wakusumbue ili utoe chochote maana hawajui kuomba bali wanatisha

Wizi nao unachangia watalii wengi wakija wakiibiwa hata simu au hela au nguo, viatu kwenye hoteli zao basi ataweka kwenye blogs na kuponda hiyo nchi na kusema kila kitu
Utalii siku hizi watu wanapokuja wanaangalia na maisha ya kustaafu pia
Kwa sasa wazungu na watu wa mataifa mengine wananunua sana nyumba Morocco kwa sababu pametulia sana
 
Mpaka hapo Kuna haja ya kuendelea kukomaa na Wanyama na kutesa na watu Wetu Kwa vitu visivyo na faida?
 
Unatumiaje Nguvu kwenye kitu kisicho na manufaa ya Moja kwa Moja kwako na ambacho by the way hata hakihitajiki sana huko kwenye soko la Utalii?

Nadhani ungekuja na figures maana ukisema haina manufaa inabidi uoneshe earnings za utalii ukilinganisha na sekta nyingine

Kwa Tanzania bara ni suala la wazi kuwa pamoja tunategemea mbuga kuliko beach tourism au utalii wa mambo ya kale tofauti na Zanzbar lakini je, uwepo wa utalii wa mbuga unatuzuia kuwekeza kwenye hizo zingine. Jibu ni HAPANA

Na kingine unachotakiwa kujua ni kuwa utalii unauza EXPERIENCE, kwa hiyo hukoomat Egypt, South Africa au Tunisia, tayari wamewekeza katika experience nzuri kwa wageni wao

Ukija Tanzania ni huzuni. Watalii watakuja na kuondoka ila hawana vitu vya kufanya kwenye miji yetu. Hata hiyo Arusha ambayo ndio Gateway ya utalii kwa kanda yetu maana ipo karibu na mlima Kilimanjaro, ngorongoro, serengeti, lake manyara etc.
Lakini je, Arusha imetengenezwa kuwa tourist city ambayo malli atatamani akitoka mbugani akateketeze pesa zake..

Ni obvious fact kuwa huo ni uongo, so tukubaliane, tunategemea utalii wa natural resources kwa sababu vinajiuza vyenyewe tofauti na vitu vingine
 
Angalia wingi wa Hifadhi za Taifa na adha ambazo Wananchi wanapata kupitia hicho mnaita Hifadhi.

Sehemu zingine Kuna Hadi Mali kama Madini yenye maana zaidi kuliko hao nyumbu mnaogangaika nao.

Mchango wa sekta ya Utalii ni mdogo sana kwenye uchumi isipokuwa kidogo kwenye Fedha za Nje.

Hoja yangu hapa ni aina ya Utalii tunaokomaa nao vs mazao mwengine ya Utalii.

Miji mingine imetengenezwaje huko Afrika? Binafsi sioni kama ni ishu ya kutengenezwa Kwa sababu hakuna mahala wao wametengeneza Miji Yao zaidi ya watu kuona Magofu na kucheza ufukweni.
 
Mpaka hapo Kuna haja ya kuendelea kukomaa na Wanyama na kutesa na watu Wetu Kwa vitu visivyo na faida?
Hapana mkuu sioni haja ya kuendelea kuwa na mambuga makubwa
Hebu angalia mfano Kruger National Park sehemu ambayo wana mahoteli unaoga kwenye swimming pool na Tembo wanakuja kunywa maji hapo na twiga wanakusalimia ukiwa kwenye balcony sehemu kama Kenya

Sisi hata barabara za hifadhi huna uhakika kama utafika
Majengo ya kizamani Dar mkavunja yote kwa tamaa ya baadhi ya watu Ardhi na kupisha ujenzi
Kwa sasa pigeni kelele tuwe na mahoteli hata maili moja ya fukwe hapo na mimi walahi ntawekeza
 
Kwa kuangalia hizo numbers utagundua TZ na KE zina underperform vibaya sana. Both TZ na KE zinaingiza about 1.7M tourists annually pamoja na vivutio vyote walivyonavyo, huku Rwanda is closing in with 1.4M kwa vivutio vichache sana.

Egypt, Morocco, Tunisia zipo karibu na Europe na mazingira rafiki. Ni rahisi mtalii kwenda huko kuliko kusafiri across the globe kuja East Africa. SA mazingira rafiki ila mbali ndo maana haigusi namba za Northern Africa.
 
Nini maoni Yako sasa
 
Nini maoni Yako sasa
Maoni ni kwamba tumelala sana,

Na sababu ya huo usingizi ni chama lako la CCM,

Huwa unajitoe akili tu , lakini kila kitu unafahamu tatizo liko wapi,

Ndugu yangu wewe chawa ni hivi, watu tunaowategemea wawe Think tank ya kuleta mabadiliko , leo hiyo akili imeshawaponyoka,

Hawawazi tena kama wewe na mimi tunavyowaza, wanachowaza wao ni kwenda makazini kutafuta michongo tu, si kukuwazia wewe,

Hawa watu wetu wanasafiri sana kwenda nje , lakini hujiulizi kwa nini hawana kitu kipya, ni kwamba akili imeshadumaa,

Ni kama Mstaafu anayekaribia kustaafu , hawezi kufikilia kitu kingine cha kumfaa miaka 30 ijayo,

Na hata hiyo idadi unayoona hapo ya watalii waliokuja Tanzania, kwa taarifa yako hata nusu tu kuja huku Bara hawafiki , watalii wengi sana wanaenda Zanzibar, karibua asilimia 65 wanaenda ZNB kwa ahili ya utalii wa fukwe.

Na viongozi wako wanafahamu hilo,

Hivi huku bara umeshawahi ona ndege ya watalii zaidi ya 400, na wote wakiwa ni watalii inashuka hapa , basi Zanzibar ni kawaida,

Nimeshashuhudia mara nyingi tu pale uwanja wa ndege Sheikh Amri Abedi, zimekuja ndege tatu kwa kufuatana zote zimejaa binadamu kama 400 kila moja ,

Na baada ya dakika chache tu wote wameondoka na ukienda mjini humwoni hata mmoja, wote wamepotelea huko kwenye beanch, mpaka nikashangaa,

Huku kwetu bara inatakiwa tuwe na special Tourist Zone ukanda wote wa bahari kuanzia Tanga mpaka Mtwara,

Zikatwe block nyingi tu ambazo ni kwa ajili uwekezaji wa kitalii tu na tuweke condition kwa anayetaka kuwekeza ni nini sisi tunataka awekeze hapo, sio kutujazazia mabanda mabanda tu kama ya coco beanch , ziwekwe hoteli kweli na iwe marufuku mijitu kwenda kuzurula huko lapo uwe mfanyakazi , maana hawa wenzetu wanataka utulivu sana ,

Sisi kazi yetu iwe ni kukusanya kodi tu, na hapo ndio utaona namna uchumi wetu utakavyosisimka, kwanza tutakuwa na advantage mbili, BEANCH ECONOMY NA MBUGA ECONOMY.

Sasa kwa watu wetu hawa watunga sera , haya yako kichwani mwao zaidi ya upigaji tu.

Ningweza kukutana na Mama Samia , ningemwambia hii ndio legacy ambayo atakumbukwa nayo kamba Yule mama ndio alibadiri hii sekta ya utalii Tanzania,

Na kama tupo seriously basi hata kwenda Zanzibar ni karibu tukajifunze
 
Nimekuwa najiuliza swali na kuharibu kutafiti ni mambo yapi au vitu gani spesho ambavyo vinavuta Mamilioni ya watalii kutoka Nchi mbalimbali Duniani Kutembelea Nchi za Kaskazini mwa Afrika za Egypt, Morocco na Tunisia? Watu wanatoka Duniani kote kwenda kutumia mabilioni ya pesa huko, Kunani hasa? Nikatafuta kufahamu.

Yaani majibu niliyopata yamenishangaza sana.Kwamba kinachowapeleka watu kwenye hizo Nchi ni Magofu ya kale (Majengo chakavu ya tawala za kale),beaches na labda eti Pyramids.

Nikajiuliza zaidi na kuchimba ndani ni mambo hayo tu? Na Je idadi kubwa ya Watalii wanatoka wapi? For the case of Tunisia wengi wanatoka Algeria na Libya, Kwa Morocco wanatoka Ulaya hasa Spain na Egypt Kwa sehemu kubwa ndio wanatoka maeneo mbalimbali.

Maswali Yanayonitatiza.

Kwamba Utalii ni Magofu na Beaches na sio Nyumbu au vifaru. Yaani watu Wana shida na Magofu zaidi kuliko Wanyama ambao kutwa kucha tunafunga watu Wetu eti ni vivutio vya Utalii.

Nikaendekea kutafakari na kujiuliza, mbona Tanzania tuna Magofu ya kale ya kutosha tuu mfano Stonetown Zanzibar,Bagamoyo, Kilwa, Ismani nk? Hao Watalii mbona hatuwaoni Kwa Wingi? Kwani Magofu wanayokuja kuangalia yanatakiwa kuwaje?

Mbona Tanznaia tuna beaches nzuri kushinda wao na kubwa kuanzia Mtwara Hadi Tanga? Zanzibar yote na Maziwa yote Makuu? Mbona hatuwaoni wakija Kwa Wingi Kuchezea,kupiga picha na kuingiza aunkufanya matamasha?

Hata South Africa ambao nao Wana Wanyama kama sisi ,idadi kubwa ya Watalii wao hawaendi kuangalia Wanyama Bali ni majirani wanaokuja Kwa Ajili ya biashara,fukwe na wachache ndio wanakuja Kwa Ajili ya Wanyama.

Maswali.
Kama Utalii unaobamba Duniani kote hauhusiani na Wanyama Wala misitu Kwa nini mambo haya yanafanyika?

1. Kwa nini Serikali inafuata Vijiji,kunyang'anya watu maeneo Kwa kisingizio Cha Uhifadhi na kuwa kivutil Cha Utalii ambacho sio kitu watalii wanakipenda?

2. Kwa nini tutumie mabilioni ya pesa kuhamishia watu kwenye maeneo Yao Kwa kisingizio Cha Utalii ambao sio bidhaa ambayo Watalii wanahitaji?

3. Kwa nini tuwafunge watu Wetu miaka jela Kwa sababu eti za kukutwa na vipande vya Wanyama pori,tuwalipishe faini,mazao Yao yanaharibiaa na Wanyama nk? Huo Uhifadhi una faidia ipi Kwa jamii wakati sio kati ya mazao ya Utalii yenye soko Duniani?

Hitimisho.
Ni vyema Serikali ikajitafakari Kwa hayo niliyoeleza hapo Juu Kwa sababu tunakomaa na kuumiza jamii yetu Kwa vitu ambavyo havina faida Kwa watu Wetu labda kuwafaidisha Wazungu.

Kama tunataka Utalii tuweke Nguvu kwenye mazao ambayo Watalii wanataka na sio kuhangaika na Wanyama.

Tujiulize Kwa nini tuna fukwe nyingi na Magofu ya kutosha lakini hakuna watalii wa maana wanaokuja.

Mwisho tukuzee Utalii wa ndani Kwa Kuinua uchumi wa watu na pia tuishi vyema na Nchi Majirani na kukitangaza kwao maana hao ndio Watalii Wetu wa uhakika badala ya kuhangaika na WA Ulaya ambao wanaenda Kwa majirani zao.eg Cuba, Malta nk

View: https://twitter.com/AfricaFactsZone/status/1751212698614858037?t=PPV0rMBdm6kh-f_vFn_oXg&s=19

Wenye Magofu na fukwe wanapata watalii kati ya Milioni 9-15 na wenye Mbuga za Wanyama Wana pata watalii kati ya Milioni 1-5.Tutumie akili.

Tanzania imejaa Magofu kama haya ya Kilwa ila Watalii ni WA kutafuta na tochi mbona?👇👇

View: https://www.instagram.com/p/C3Ak3mnI3xt/?igsh=MXYzcmJjNGxleTRjbA==
 
Back
Top Bottom