Mafanikio ya mbuga ya Burigi - Chato yawa gumzo Duniani

JackisonDubai

JF-Expert Member
Mar 27, 2023
537
1,274
Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) imeiteuwa Hifadhi ya Burigi-Chato kuwa miongoni mwa hifadhi mbili nchini zitakazoendeleza kuhifadhi faru weupe ambao ni adimu zaidi nchini.

Kupelekwa kwa faru weupe katika hifadhi hiyo ambayo ni ya tano kwa ukubwa kati ya hifadhi 22 zilizopo. Hivyo kutaifanya kuwa miongoni mwa hifadhi zenye sifa ya kuwa na wanyama wakubwa watano.

Kwa mujibu wa Kamishna msaidizi wa uhifadhi, Jonny Nyamhanga ambaye pia ni msimamizi wa Hifadhi ya Taifa ya Burigi Chato amesema wanyama wengine wakubwa wanaopatikana katika hifadhi hiyo ni pamoja na tembo, nyati, simba na chui.

Akizungumza ofisini kwake na waandishi wa habari leo Desemba 02, 2022, Nyamhanga amesema uwepo wa faru katika hifadhi hiyo itakuwa kichocheo cha kuongeza wageni na kwamba watalii watapata fursa ya kumbatiza faru kwa kumpa jina ambalo atalilipia kwa kipindi fulani.

Nyamhanga amesema mbali na utalii wa wanyama wa nchi kavu pia watalii wanaweza kufanya utalii wa majini na kuona wanyama kama kiboko pamoja na kuvua samaki kwa ndoano na kwamba hifadhi hiyo inaupekee wa kuwa na maziwa matano ndani ya hifadhi.

“Hifadhi hii pamoja na uchanga wake lakini wanyama wanaongezeka kwa kasi zamani waliokuwa wakiwindwa, sasa wameanza kuamini kuwa wako salama hawajifichi kama mlivyotembelea na kujionea wenyewe ongezeko kubwa la wanyama. Pia vivutio kama mti mmoja mkubwa ambao ukiwa kwenye eneo hilo unaweza kuwatazama wanyama wote kwa wakati mmoja,” amesema Nyamhanga.

Aidha hifadhi hiyo inapakana na nchi tatu za Afrika Mashariki ambazo ni Rwanda, Burundi na Uganda na kwamba uwepo wa eneo la mipaka ya nchi tatu ni fursa nyingine inayoweza kuingiza watalii na kuongeza pato la Taifa.

Akizungumzia watalii wanaoingia katika hifadhi hiyo, Nyamhanga amesema idadi inaendelea kuongezeka siku kwa siku. Mwitikio wa wazawa uko chini na kuitaka jamii kubadilika na kuona hifadhi ni mali yao na wanapaswa kuwa mstari wa mbele kuzitembelea na kuona rasilimali zilizopo.

Consolata Evarest miongoni mwa wanahabari waliotembelea hifadhi hiyo amesema kutokana na ongezeko la wanyama ndani ya hifadhi ni wakati sasa wa makampuni ya utalii kutangaza hifadhi hiyo kwa kupeleka wageni kwa wingi.

“Tumezoea kuona magari mengi kwenye hifadhi nyingine kwa kuwa hii ni hifadhi changa na haijazoeleka ninaimani kampuni za utalii zitatembelea na kuona wanyama walivyo wengi,” amesema Evarest.

“Kujionea maziwa haya matano pamoja na eneo la mpaka wa nchi tatu, hivyo kwa sababu hizo ni rahisi kumtoa mgeni Rwanda na kuja Burigi anapita kwenda Serengeti kisha ataenda hifadhi zilizoko kaskazini,” amesema Evarest.

MWANANCHI
 
Kaburi, watu wanaenda kushuhudia kama kafa vizuri pamoja na ukatili wake
Wenye roho za hivyo wala hawezi kukanyaga lile kaburi. Maana watalionea wivu namna lilivyopambwa.

Wengi wanaenda kuangalia alipolala mwanamageuzi namba moja tanzania na mleta maendeleo namba moja Tanzania.

Kusini hadi kazikazini kaweka kazi ya mikono yake. Hivyo usibeze ndugu.
 
Labda maendeleo ya CHATO, ameleta kitu gani?
 
Wenye roho za hivyo wala hawezi kukanyaga lile kaburi. Maana watalionea wivu namna lilivyopambwa.

Wengi wanaenda kuangalia alipolala mwanamageuzi namba moja tanzania na mleta maendeleo namba moja Tanzania.

Kusini hadi kazikazini kaweka kazi ya mikono yake. Hivyo usibeze ndugu.
Mimi nadhani makaburi ni mengi sana.
Sasa kwenda kushangaa kaburi hii ni ajabu nyingine. Labda wanaenda kujiridhisha jambo flani ambalo hawakuamini kutukia kwake.
 
Alieyeanzisha hifadhi hii anastahiki sifa kwa kuwa mtu mwenye ubunifu. Hata Ghadafi alibadili jangwa na kuwa kama ardhi ya Tanzania.

Hapo nimependa hiyo kulipia jina la mnyama kwa kipindi fulani.Ni ujanja mzuri wa kuchota pesa za watalii wenye pesa zilizolala kwenye mabenki.

Na huo mti mrefu wa kuoangalia wanyama wote ni mti gani.Unapanda mwenyewe au kwa kubebwa na tinga tinga.
 
Alieyeanzisha hifadhi hii anastahiki sifa kwa kuwa mtu mwenye ubunifu. Hata Ghadafi alibadili jangwa na kuwa kama ardhi ya Tanzania.
Hapo nimependa hiyo kulipia jina la mnyama kwa kipindi fulani.Ni ujanja mzuri wa kuchota pesa za watalii wenye pesa zilizolala kwenye mabenki. Na huo mti mrefu wa kuoangalia wanyama wote ni mti gani.Unapanda mwenyewe au kwa kubebwa na tinga tinga.
Kweli kabisa
 
Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) imeiteuwa Hifadhi ya Burigi-Chato kuwa miongoni mwa hifadhi mbili nchini zitakazoendeleza kuhifadhi faru weupe ambao ni adimu zaidi nchini.

Kupelekwa kwa faru weupe katika hifadhi hiyo ambayo ni ya tano kwa ukubwa kati ya hifadhi 22 zilizopo. Hivyo kutaifanya kuwa miongoni mwa hifadhi zenye sifa ya kuwa na wanyama wakubwa watano.

MWANANCHI
Kiukweli I was very right niliposhauri Naunga mkono Uwanja wa Ndege wa Chato. Una justification, utakuwa kama Ggabolite au Yamoussoukro. Watalii watamiminika!
P
 
Back
Top Bottom