Kugombana na Wazungu ni kugombana na Utajiri

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,886
KUGOMBANA NA WAZUNGU NI KUGOMBANA NA UTAJIRI.

Anaandika Robert Heriel.

Kutokana na Elimu duni ya Watanzania waliowengi kuhusu mambo ya kihistoria, wengi hawana Uelewa Dunia imetoka wapi, ilipo na wapi inapoelekea. Hivyo sio ajabu kumsikia Mtanzania Fulani akisema Wazungu ni adui zetu, Wazungu hawatufai, na wakati mwingine kuwachukia watu wote wenye ukaribu na Wazungu kwani wanawaona kama wasaliti na vibaraka.

Hiyo sio ajabu Kwa mtu asiyeijua Historia ya Dunia kufikiri hivyo. Ila itakuwa ajabu Kwa mtu mwenye elimu ya Historia walau ya Form Six aliyechukua masomo ya Arts kuwa na mtazamo Kama huo. Tena itakuwa ni ajabu Kwa Wasomi wa Biblia waliobobea au wasomi wa Kurani waliohitimu Visomo vya juu kuwa na mtazamo Kama huu.

Wazungu Kwa mujibu wangu na andiko hili, istilahi hiyo "Wazungu" itawahusu jamii zote za watu waishio nchi za Magharibi, Kuanzia Waingereza(ambao ndio Wazungu hasa), Wajerumani, Wafaransa, Waitaliano, Warumi, Wahispania, wareno, na Wabeligiji miongoni mwa jamii zingine za Wazungu. Ingawaje kimsingi Wazungu OG ni waingereza.

Kuchukia jamii ya kizungu ni ukosefu wa maarifa.
Na endapo utawasikiliza wenye chuki na Wazungu hoja zao hazina mashiko, ni hoja nyepesi zinazochechemea,

Tunahitaji kiongozi anayejua Historia vyema na kuielewa, kisha tunahitaji kiongozi mwenye akili za biashara,
Tunahitaji kiongozi mwenye akili za kuitumia historia katika kuinufaisha Nchi yetu.

Nchi haiwezi kuendelea ikiwa Watanzania wataendelea na akili za kijinga kuhusu mtazamo wao Kwa Wazungu, au jamii za kiarabu au Kihindi.

Wote tunajua nchi ZETU hizi ni masikini, mbali na umasikini pia uwezo wetu katika kufikiri haulingani na jamii zingine Kama Jamii za mongoli, waarabu na Wazungu. Tukubali tukatae lakini ukweli utabaki hivyo.

Lazima Wazungu tushirikiane nao ili nasi tuwe matajiri, hatuwezi kuwaepuka. Labda tujidanganye.

Serikali na viongozi waliopo, ni lazima tuunde jamii itakayoweza kujifunza mazuri kutoka Kwa jamii zingine hasahasa zile zilizotuzidi.

Kusambaza chuki na hasira Kwa vizazi vyetu haitasaidia kitu.

Kama ni ukoloni na utumwa karibu jamii zote Duniani zilitawaliwa na mataifa mengine. Kama ni UTUMWA karibu mataifa yote yanahistoria ya kufanyishwa UTUMWA.
Sio waarabu, sio wachina, sio wajapan, sio Wayahudi sio Wazungu. Jamii zote zilipitia hayo.
Ndivyo mfumo wa Dunia ulivyokuwa.

Kutawaliana kwenye dunia ni Jambo ambalo halikwepeki, aidha utawale au utawaliwe.
Lakini lazima tuyafanye mambo haya kibiashara ili walau wote tunufaike.
Angalau Mtawala akipata 60% mtawaliwa naye apate 40% na hiyo ni Kama mtawaliwa atakuwa anajielewa na mwenye akili.

Lakini kama atakuwa Mpumbavu, sioni shida akilambwa 80% kisha naye apate 20% au 10% kabisa.

Ninao uhakika Kabisa Waafrika wengi Kama tutaamua kujifunza mazuri tutafika mbali, kuliko kujifanya jeuri na kupambana na watu waliotuacha mbali.

Ni muda sasa WA kuzigeuza nchi ZETU zinufaike na ushirikiano na Wazungu.

Sio wanasiasa uchwara wanaojifanya mbele ya majukwaa wanawapinga mabeberu alafu nyuma ya Pazia wanauza Mali za nchi Kwa haohao Wazungu na kujitajirisha wao wenyewe huku wakiwaacha Wananchi wakiimba wimbo usemao" Wazungu hawatupendi*

Wakati wananchi wanaimba Wazungu hawatupendi, nyuma ya Pazia wanasiasa wanapeleka watoto wao kusoma nchi za Wazungu huku Sisi masikini tukibakia na shule zetu zisizo na elimu nzuri.

Wakati wanasiasa wakiwaimbisha wananchi kuwa Wazungu ni wauaji wakubwa, wao huenda kutibiwa huko Kwa Wazungu wakirudi wamepona kabisa alafu Sisi tunabaki tukifa na Hospitali zisizo na Dawa.

Wakati wewe fukara ukiimbishwa Wazungu Wabaya, viongozi wanakuwa madalali na mawakala wa bidhaa za makampuni Makubwa ya kizungu na kuja kuwauzieni na kujipatia Utajiri ninyi mkifa masikini.

Siku zote wenye akili hutumia kanuni isemayo; ungana na mwenye nguvu, mwenye akili na mwenye uwezo.

Chuki za waliofanikiwa hazitakusaidia lolote.
Kuchukia Wazungu au jamii za kitabu na kichina hakutakusaidia lolote.

Hata hapa nchi jamii zilizoendelea huchukiwa na kupewa kejeli, mfano jamii za Wachaga, Wabaya, wakinga, wapemba, Waha hupewa kashfa za hapa na pale kuwa wanaroho mbaya, sijui wachawi, sijui wanatoa kafara, matapeli na wezi. Kisa tuu wanahangaika kutafuta Utajiri na baadhi Yao wanaunafuu

Sijui Kama naeleweka!

Acha niishie hapa!

Robert HERIEL
Taikon wa Fasihi
Kongowe
 
Wapo wazungu wenye nia njema na bara la Afrika, lakini pia wapo wazungu wanatamani waachie bomu liue Afrika nzima then waje wachukue rasilimali zetu ikiwezekan waishi huku kwenye utajil.
 
Wapo wazungu wenye nia njema na bara la Afrika, lakini pia wapo wazungu wanatamani waachie bomu liue Afrika nzima then waje wachukue rasilimali zetu ikiwezekan waishi huku kwenye utajil.


Halikadhalika wapo Waafrika tunaowaona kila siku wakiitakia mabaya nchi yetu. Huoni mpaka hivi leo nchi ni masikini?

Alafu haohao ndio wanakuwa mdomo mbele Kama filimbi kuwaponda Wazungu ili kuficha uhuni wao.
 
Wapo wazungu wenye nia njema na bara la Afrika, lakini pia wapo wazungu wanatamani waachie bomu liue Afrika nzima then waje wachukue rasilimali zetu ikiwezekan waishi huku kwenye utajil.
Tunawakaribisha waje wawekeze na kujenga vile vitu wanajengaga kwao kisha tuishi nao tuwaoe, waoe dada zetu n.k,,, ila sio kutuua
 
Historia unayoizungumzia wala hata huijui.

Ebu jiulize kwanza:

Wewe unajua vizazi vyako vigapi? Yaani unawajua historia ya mababu zako wangapi?
 
Acha kucheza na wazungu, hakuna wanalofanya kwa hasara wala kumsaidia mtu/Nchi for free!!.
There is no free lunch in the world of capitalist. Nchi pekee itakayotuvusha ni kuwa na taasisi imara zitakazowabana watawala wabovu.

Na taasisi imara inajengwa na kitu KATIBA.
 
Now we can see wale waliouza wenzao utumwani walikua watu wa aina gani

You are a true slave
 
Kuna mjinga mmoja alishupaza shingo kuwaita wadau wa maendeleo ni mabeberu huku tukiwategemea hadi vyoo watujengee wao.
 
Back
Top Bottom