Kufunga jela viongozi wa Upinzani ni maagizo iliyopewa mahakama ya Tanzania ?

Nidhamu inatakiwa ianzie juu.Katiba yetu inasemaje kuhusu Mikutano ya vyama vya siasa??Ukilijibu hili basi yule Mathew wa Lindi hakutakiwa hata kufunga siku moja.

pole uwe chizi kuliko kuwa Mwanachama wa CCM


Na bora uwe chizi kuliko Ukawa maana akili zao zimeshikwa na mtu mmoja.
Ndio maana leo mkisema ndio kesho mtasema hapana,mngekuwa timamu yale maneno mliyokuwa mnamsema Lowasa sidhani kama mngediriki kumuomba aje Ukawa tena kwa kupiga magoti.
 
Nchi yetu saiv inadall zote za kdkteta, ushaid n kutokana na rais malaika tulyenaye kuliongoza taifa hl kwa kuvunja katba na sheria, kwahyo watanzania wenzangu tuko ktk kpnd kgum sana nchi tukiiona taratiiiiiibu ikielekea kwenye udkteta.MUNGU barik taifa hl
 
sheria ipi imevunjwa........?

Au katiba kuruhusu vyama vingi ndio kosa?

huyu kafungwa kwakufanya mkutano....hakufanya mtu afe wala uhalibifu wowote haukutokea

Swali

1. IPTL mpaka leo inatukamuwa vilivyo....nani anahusika?? yupo wapi? nani!

2. Lugumi inatutesa kutwa kucha....nani mhusika? mbona hatuoni wakifungwa?

3. Wezi wa Escrow wapo wapi? nao nimakada wa ccm.....wengine wapo madarakani

4. Wezi wa twiga wetu kwa ndege tena yakijeshi wapo wapi?

5. Wezi wa mafuta bandalini miaaka kadhaa wamechepusha mafuta na kuzima mita wapo wapi?......sheria ipo wapi hapa?

6. Alieuza nyumba za serikali sasa hivi watumishi wanataabika yupo wapi? kwanini hakamatwi...na yule wa kiwira coal mine?

7. Alieuwa watu kwa kuwauzia dawa feki za ukimwi ...muuwaji kada wa ccm yupo wapi?

8. waliofilisi Shirika la ndege na reli wapo wapi?

9. Alipeleka meli uchina imejaa meno ya tembo wa tanzania yupo wapi?

nknknknknknknknk

Nyinyi mnaodhani kufunga mtu kwa simple case tena za kipuuzi je...kuna uzito kama makosa hayo hapo juuuu? wapo wapi hao kama sheria infuata mkondo na hakuna upendeleo?
Hoja hapa ni Lugumi au kufungwa jela mbunge? Sheria inasema nini kuhusu mikutano ya siasa?
 
Lakini kiongozi mzima utafanyaje siasa za kiharifu? ? Kwanini wasiige siasa za Zitto, Mnyika, Kafulila usshawahi kuona wanawekwa ndani? ? Lakini ona mchango wao wa serikali na jamii nzima. .
Hapo umeongea point aise, kula LIKE ya nguvu. Miili saba inatoka wapi kwenye sandarusi kama si SIASA ZA KIHARIFU?!!!
 
Na bora uwe chizi kuliko Ukawa maana akili zao zimeshikwa na mtu mmoja.
Ndio maana leo mkisema ndio kesho mtasema hapana,mngekuwa timamu yale maneno mliyokuwa mnamsema Lowasa sidhani kama mngediriki kumuomba aje Ukawa tena kwa kupiga magoti.
Hiyo sound wamebaki wanaitumia wajinga tuu. Ndio maana huwezi kukuta kiongozi wenu hata mmoja wa ccm anarejea kauli hizo zilizokuwa zinatumika wakati wa kampeni ili kuwahadaeni.
Hata washabiki wenye ufahamu hukuti hata kidogo wakirejea maneno hayo ila imebaki kundi dogo la wenye upeo wa aina yako. Huelewi historia ya Lowassa na hujui chanzo cha kashfa zake bali umekaririshwa uimbe kama kasuku tuu.
 
Lazima upinzani ujifunze kujihami nje ya mifumo ya haki awamu hii, vinginevyo tutakwisha wote hakuna atakayepona wakati unatangazwa ukuta watu waliona ni maskhara ila sasa hakuna aliye salama kuanzia upinzani vyombo vya habari mpaka viongozi wa upande pinzani na watoa maoni mbadala wote hatarini.
 
Swali la msingi je alikuwa na kosa au kabambikiwa.?
Na je haki kwenu kufanya makosa?.Je ni dhambi kwenu kuhojiwa kwa makosa?
sasa cha msingi jifunzeni nidhamu tu ya maisha,otherwise mtapata shida.
Shida hata mandela kapata hakuna anaeishi miaka 1000 wote pua zetu zinaangalia chini na chini tutarud
 
Hili la kuwafunga jela viongozi wa upinzani bila faini , hata kama kuna adhabu ya faini kwenye makosa wanayohukumiwa nayo haliwezi kupita bila kujadiliwa.

Tuliambiwa kwamba Mh Lijuakali amepewa kifungo bila faini kwa vile ni mtu anayerudiarudia makosa yaleyale ( niko tayari kusahihishwa ) . Huo ulikuwa ndio msisitizo wa Hakimu katika style ya kunawa mikono.

Sasa najiuliza kwa kifungo cha Suleiman Methew cha miezi 8 bila faini , naye amerudia makosa yale yale kila mara , au ni mkakati wa mahakama nchi nzima wa kutii maagizo ya ccm , ili kukomoa na kutisha wapinzani wa kweli ?

Zipo tetesi kwamba kuna vifungo vya watu maarufu vinakuja , sasa huu ni mkakati wa kutuandaa kisaikolojia , lakini natoa wito kwa Mahakama kutenda haki bila uonevu , maana huwezi kujua ni nani atakuwa mamlaka ya uteuzi kesho .
MHALIFU MZOEFU HUWA HAPEWI FAINI,KWANI AKITOKA TU ANARUDIA MAKOSA YALEYALE NDO MAANA WANAFUNGWA JELA !
 
Huwezi linganisha utawala uliopita kuhusu Uhuru wa mahakama na huu wa sasa kikwete alikuwa anaona mbali Sana hakuwahi ingilia muhimili mwingine hata siku moja hivi Kama mkuu anaweza sema polisi wafungue matairi ya wahalifu barabarani wauze unadhani nini kinashindikana kwake

Wapi Magufuli ameingilia uhuru wa mahakama? Polisi ni mahakama? Bavicha bana!
 
Mahakama haitumii logic, ni sheria zaidi, ukiona hadi wapinzania wanashinda kesi ujue serikali kupitia mahakama imeshindwa kutemper na ushahidi, ila ccm na serikali wanatoa hukumu kali hata mahali kusiko kuwa na ushahidi wa kutosha ikiwamo kupindisha adhabu, mfano Lijualikali amefungwa kwa kufanya fujo lakini pia Ndugai, wasira na Titus kamani walishafanya fujo za kupiga watu lakini hawakufanywa lolote.......

Jitahidi kuanalyse ukiwa na neutral mind utajua ukweli......

Yaani ni wapi na lini katika nchi hii ccm au serikali imewahi kutoa hukumu? Hivi nyinyi bavicha huwa mnatumia bongo zenu kweli? Huyo Lijualikali amehukumiwa na CCM au serikali?
 
Maskini wa fikra siku zote huona wanaonewa kila kukicha. Zitto anaongea mangapi kuhusu kuikosoa serikali? Lini katiwa nguvuni kwa ukosoaji huo! Pinga na kosoa kwa hoja, sio matusi na lugha chafu
 
Wanachotakiwa ni kimoja tu wapinzani wasidhani wako juu ya sheria pindi watakapolitambua hilo watakuwa salama. Walizoea kuchukuliwa poa na walioweza wengine Sheria inachukua mkondo wake!
Umeamua kujitoa ufahamu
 
Polisi walienda kwa sababu ndio wanasiamamia mikutano yote ya hadhara....

1. Mkutano ambao ndugai alipiga mwenzake ulilindwa na kenge?

2. Unafahamu maana halisi ya kashitakiwa na Jamhuri?

3. Wanaoshikwa kwa kuposti mitandaoni ...nani huwashitaki?
 
Hoja hapa ni Lugumi au kufungwa jela mbunge? Sheria inasema nini kuhusu mikutano ya siasa?

Inasema ccm pekee ndio wenye...

-Haki kulindwa na polisi

-Haki kupigana bila kufungwa

-Haki kukusanyika kisiasa

ccm ndio watanzania halisi wanaotambhlika na katiba
 
Back
Top Bottom