Kiteto: Mwenyekiti wa Mtaa Jela Miaka 4 kwa kupokea Rushwa ya Tsh. 60,000

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
Mahakama ya Wilaya Kiteto imemhukumu MAMBE MOHAMED MAMBE, Mwenyekiti wa Kijiji cha Nasetan, Kata ya Engusero, Wilaya ya Kiteto Mkoa wa Manyara.

Mshtakiwa ametiwa hatiani na kuamriwa kwenda Jela miaka minne au kulipa faini ya shilingi 1,000,000/= kwa makosa ya kuomba na kupokea hongo kiasi cha shilingi 60,000/= kinyume na k/f 15(1)(a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 kama ilivyofanyiwa marejeo Mwaka 2022.

Hukumu hiyo dhidi ya MAMBE MOHAMED MAMBE katika kesi ya jinai Na.20/2023, imetolewa na Mhe. Boniface Lihamwike, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Kiteto, Machi 27, 2024.

Mshtakiwa aliomba hongo ya sh. 60,000/= ili asimchukulie hatua za kisheria mwananchi ambaye alifanya mkutano wa wafugaji bila kibali cha serikali ya kijiji.

Mshtakiwa ameshindwa kulipa faini na amepelekwa magereza kutumikia kifungo chake.
 
Issue sio Milioni Moja wala Miaka.Issue ni Tafsiri ya Hukumu Hii mintarafu Rushwa
 
Hii hukumu imekaaje? Kuna kiongozi mwingine wa serikali nimeona amehukumiwa na mahakama hii hii kwa kosa la ubadhirifu wa fedha za wananchi kama milioni moja hivi na kidogo, hukumu yake ilikuwa jela miezi tano au faini ya laki 2.

Sasa huyu hongo ya elfu 60 asote rumande miaka minne au fainu ya milioni 1? Kwani hizi sheria zinakaaga aje?
 
Hakimu mwingine mpumbavu huyu,hana tofauti na yule aliyempeleka jela poor of the poorest eti kwa kukutwa na kilo moja ya nyama ambayo inadaiwa ni ya swala!!,pale pale iringa kuna fisadi lililoua tembo wetu wengi tu lakini lipo huru
 
Back
Top Bottom