Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 125,733
- 239,339
Hili la kuwafunga jela viongozi wa upinzani bila faini , hata kama kuna adhabu ya faini kwenye makosa wanayohukumiwa nayo haliwezi kupita bila kujadiliwa.
Tuliambiwa kwamba Mh Lijuakali amepewa kifungo bila faini kwa vile ni mtu anayerudiarudia makosa yaleyale ( niko tayari kusahihishwa ) . Huo ulikuwa ndio msisitizo wa Hakimu katika style ya kunawa mikono.
Sasa najiuliza kwa kifungo cha Suleiman Methew cha miezi 8 bila faini , naye amerudia makosa yale yale kila mara , au ni mkakati wa mahakama nchi nzima wa kutii maagizo ya ccm , ili kukomoa na kutisha wapinzani wa kweli ?
Zipo tetesi kwamba kuna vifungo vya watu maarufu vinakuja , sasa huu ni mkakati wa kutuandaa kisaikolojia , lakini natoa wito kwa Mahakama kutenda haki bila uonevu , maana huwezi kujua ni nani atakuwa mamlaka ya uteuzi kesho .