Kufukuzwa kwa Rais wa Vijana wa ANC Julius Malema na hulka za Viongozi wa Afrika kukimbia Changamoto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kufukuzwa kwa Rais wa Vijana wa ANC Julius Malema na hulka za Viongozi wa Afrika kukimbia Changamoto

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ben Saanane, Nov 10, 2011.

 1. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #1
  Nov 10, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Muda mfupi uliopita kamati ya Nidhamu ya chama cha ANC imemfungia Julius Malema kwa mika mitano na kumvua madaraka ya Urais wa Vijana pamoja na Msemaji wa ANCYL Floyd Shivambu. Malema ameonekana kwamba amechochea mgawanyiko ndani ya chama na serikali

  Kilichomponza Julius Malema ni msimamo wake wa kupigania maslahi ya vijana na class ya chini ambayo haioni fursa ya kusonga mbele kwa matumaini huku uchumi wa nchi ukiendelea kuwa mikononi mwa Makaburu. Bado vijana wa Afrika kusini kama walivyo vijana wa Tanzania wanaishi kwa matumaini na hofu juu ya kesho yao. Hoja alizokuwa akipigania Malema za kufanya reforms katika sekta ya madini na Ardhi kwa maslahi ya maskini walio wengi iliungwa mkono kwa nguvu

  Hoja nyingine ya kuangusha serikali vibaraka kama Botswana na kumuunga mkono Robert Mugabe imetumika kama chambo tu ili kughilibu matakwa na maslahi ya vijana na maskini wa Afrika kusini ili kukwepa kuwajibika kufanya reforms.Madai ya Julius Malema ni ya Msingi sana kama kweli Afrika kusini inataka Taifa lisonge mbele na kuepuka mapambano ya kitabaka yaani class struggle ambazo zitachochea ubaguzi zaidi.

  Kitendo cha kumfukuza Julius Malema ni mwendelezo wa viongozi dhaifu na usaliti kwa umma huku wakijitahidi kukimbia matatizo yanayohitaji suluhisho. Mwenyekiti wa chama Jacob Zuma atawaambia nini au atawapa majibu gani vijana wa Afrika Kusini walioandamana juzi tu tarehe 28-29 mwezi uliopita wakiongozwa na Julius malema katika ku-address matatizo yao? Je kumfukuza Malema na viongozi waandamizi wa ANCYL ni suluhisho au jibu la msingi kwa yale waliyokuwa wanayasimamia?

  Inaeleweka wazi sasa viongozi wa Afrika wanapokuwa madarakani hugeuka kuwa masultani na miungu mtu huku wakijitungia kanuni zilizoandikwa au ambazo hazijaandikwa kunyamazisha,kutisha na kuminya demokrasia pale maslahi yao ya kisiasa na kijamii yanapoguswa. Jacob Zuma na viongozi wenzake wanadhihirisha kwamba kuna mstari mwembamba kati ya hulka zao na zile za makaburu na pia mtazamo wao juu ya wananchi wa Afrika kusini na Hatima yao. Jacob Zuma anaonekana kuweka mkakati wa wazi wazi kwa kuhofia uwepo wa Malema ndani ya chama hicho ungemfanya awe one term president kwa sababu Malema alishatangaza kutomuunga mkono Mwenyekiti wake Uchaguzi ujao ndani ya Chama. Zuma anahofia kilichomkuta Thabo mbeki yeye akiwa Kapteni iliyomghilibu Mbeki pamoja na Malema aliyefanya kazi kubwa kwa imani kwamba Zuma angesimamia maslahi ya vijana na wananchi maskini.

  Vijana wa Tanzania hatuna tofauti na vijana maskini wa Afrika kusini na pia viongozi wetu ingea si wote katika vyama vyetu vya siasa hawana tofauti na Jacob zuma wa Afrika Kusini. Wote wanataka kuwatumia vijana kwa ajili ya maslahi yao au kama Daraja. Tusikubaliane na hilo ni lazima tuingie mezani tuangalie ni kitu gani ambacho kila mmoja analeta. Najua kwa tabia za kuiga hata mambo yasiyo na faida hata viongozi wetu kwenye vyama vya siasa watakurupuka kuiga na kuifanya ANC kuwa Role model wao katika kunyamzisha sauti zinazohoji au zisizotaka kuburuzwa bila kujua ANC ya sasa ni ya makaburu weusi si ile ya akina Mandela tena.Sasa succeccion battle imekuwa too bitter, ANC itakuwa even more divided. Ni jukumu la Julius Malema na vijana kusimama kidete sasa hadi msaliti wa vijana na maskini wa Afrika Kusini Jacob Zuma aondoke!

  Vyama vya siasa vishughulikie matatizo ya msingi na visikilize sauti za vijana. Makosa yarekebishwe, vijana wanastahili kusikilizwa na kusaidiwa na sio kutishwa. ANC itachochea mgawanyiko zaidi na kama vyama vya siasa Tanzania tunataka kutatua migogoro kwa njia hii basi igeni muone
   
 2. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #2
  Nov 10, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,503
  Likes Received: 5,613
  Trophy Points: 280
  Mkuu Ben,

  Wewe ni mwana CDM tena uliyekaribu kabisa na viongozi na ni majuzi uligombea uongozi wa BAVICHA! Ebu acha kuzunguka Mbuyu, kuwa jasiri kama Malema unae mfagilia sana kwa kusema wazi CDM inawabana vipi vijana?

  Naamini huzungumzii CCM maana hata wao hawalalamiki! Najua zaidi unaisema CDM! Hebu kuwa muwazi kijasiri,Kiongozi gani wa Cdm anaeogopa vijana na anawabana? Tupe mifano hai jinsi wanavyobanwa bwana Ben!
   
 3. M

  Marytina JF-Expert Member

  #3
  Nov 10, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  dont hit around the bush, njoo moja kwa moja
  Malema ana uzalendo sio baadhi ya vijana wanaopenda maslahi binafsi wanataka kujipenyeza kushika madaraka.
   
 4. K

  Kubingwa JF-Expert Member

  #4
  Nov 10, 2011
  Joined: Apr 23, 2010
  Messages: 502
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hayo ndo maamuzi magumu!
   
 5. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #5
  Nov 10, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,503
  Likes Received: 5,613
  Trophy Points: 280
  Nafikiri tufanye huu mjadala kwa uwazi bila ushabiki,minong'ono haifai,tujadili hili kupitia CDM ambako baadhi ya vijana wake kama Ben wamekuwa wakalalamika indirect!! Uongozi na siasa ni ujasiri,hebu Ben tupe uzoefu wako CDM na ushirikishwaji wa vijana na kama vijana hawasikilizwi!
   
 6. lukatony

  lukatony JF-Expert Member

  #6
  Nov 10, 2011
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 428
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Hili jambo linafundisha jambo moja tu hasa kwako wewe ben na ndugu yako Zitto! Ikifika muda na mnayoyafanya tutawaondoa kwenye chama na zingatieni hilo!! Kujua kwenu kusikojua mnaharibu chama chetu!
   
 7. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #7
  Nov 10, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  Malema ni kijana mtukutu - alilewa saana madaraaka. Anatumia kivuli cha kutetea walala hoi wakati hiyo ni ku scapegoat! Ni kijana aliyetayari kufanya lolote kwenye pesa, akipania tender hap SA lazima aipate.

  Nafikiri hiyo miaka mitano atrudi akiwa mature enough kuelewa kwamba pesa si kila kitu. Na kama anaona ana majority support basi ahamie chama kingine au aanzishe chake. Najua hawezi kwa sababu umaarufu wake ni kupitia ANC, nje ya hapo no way.
   
 8. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #8
  Nov 10, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,503
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Hayo ndiyo maamuzi magumu. Vijana CCM wanagombana hakuna kinachofanyika kwa ajili ya kogopa kufanya maamuzi magumu. CCM igeni mfano RSA!!
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  Nov 10, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  ....word!
   
 10. C

  Chakusonje Member

  #10
  Nov 10, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  "maskini Zuma! Urais umekufanya kinyonga. Kweli tunashangaa ya jk mzee wa ari! Nguvu! Na kasi mpya sasa tunayaona ya Zuma! Hawa jamaa wanafiki kweli kweli. Tuna muombea j,malema asikate taama, ahame anc ukombozi utapatikana tu
   
 11. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #11
  Nov 10, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Oh Really? Hebu tuelekeze nguvu na hayo maamuzi magumu kunakostahili na kuingia kwenye solutions za matatizo ya vijana na si kutoa vitisho vya kizuzu.

  Malema has been unpopular among the higher echelon of the ANC for some time now, mainly due to his stated intentions on enforcing Zimbabwe-style land grabs, on enforcing Chile-style nationalization of the mines, and on sending an ANCYL team to Botswana to overthrow the democratically elected government there. Interestingly, though, the disciplinary committee made no statements on Malema's rampant rascism

  So. What's next? Does this mean that Malema's fangs have been pulled, or even slightly blunted? Of course not. First (and soon) he will mobilize his mob ANCYL members, who will be out in force and protest loudly, to the accompaniment of violence, vandalism, disorder, and the waving about of cardboard machine guns. They will demand that law and rule be set aside, and that the verdict of the ANC's disciplinary committee be summarily thrown out - not unlike the charges against Jacob Zuma shortly before his instalment election as president of South Africa.

  Malama and his groupies will blame, in no particular order, nebulous Apartheid forces, political rivals within the ANC and other parties, America, white citizens of the world in general, and Hellen Zille . Malema will declare himself a martyr, a freedom fighter and an oppressed minority, and somewhere in there will be a call for the sort of violence (bombings, assassinations and sabotage) that were the hallmark of the ANC during the days of the "struggle for freedom". And when all is said and done, who knows - we may even see a new party, or at least a new ANC faction, which will be even more radical and rabid than ever before.
   
 12. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #12
  Nov 10, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,063
  Likes Received: 7,529
  Trophy Points: 280
  The way unavyo m-frame Malema inakunyima sifa za kusimama naye upande mmoja au hata kumuomboleza.
  Tukirudi upande mwingine na ule halisi wa Malema ukilinganisha na hizo unazozipaint inaonyesha humjui Malema au umeshindwa kumuelewa....au analysis yako imekuwa clouded na mapenzi yako binafsi juu yake..
   
 13. T

  Thesi JF-Expert Member

  #13
  Nov 10, 2011
  Joined: Aug 8, 2010
  Messages: 998
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ben,

  Julius Malema ni mfano mbaya kabisa wa kiongozi wa vijana katika Afrika. Japo Jacob Zuma tokea mwanzo alopochaguliwa ckua nae imani lakini wazo la Malema ni ujinga wa vijana wanaofikiri vilivoundwa vimejiunda hivo ni kaz rahisi tu ya serkali kivigawa kwa maskini. Hivi mtu anaposema serikali yenye heshima inayofata utawala bora na uwajibikaji kama serikali ya Botswana huyo kweli anazo kichwani? Eti muuaji na dikteta kama Mugabe ndio mzalendo eti kisa kawanyanganya wazungu ardhi kuwagawia rafiki zake. Hivi bila serkali ya Mugabekuunganishwa na kina Tshangerai Zimbabwe si ilikuwa inatembelea tumbo? Sukari kilo moja shilingi mil5 eti huko ndiko Malema anakoona neema ya Afrika kusini?

  Ubaguzi ni ubaguzi akibaguliwa mwafrika au akibaguliwa mzungu. Kwa kuwa. Sasa unapoongea maneno ya kibaguzi na kuchochea watu kuwabagua wengine kwa sababu hapo zamani waliwabagua ni ubaguzi.

  Huwezi kutaifisha mali tu hovyo hovyo katika ulimwengu wa sasa ambao ni tofauti na pale tulipotoka ukoloni halafu ukawa salama. Lazima iwe ni viable plan inayoweza kufanya kazi sio tu kuongea kwenye majukwaa kujitafutia umaarufu kama Malema.
   
 14. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #14
  Nov 10, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280


  Naongelea vyama vyote.Hakuna chama hata kimoja kimekuwa perfect katika kuhakikisha vijana wanakuwa independent na wana-spear head ajenda zao.Vijana wanatishwa na kamati kuu za vyama vya siasa huku tukijibaraguza wakati wa kura kuhitaji kura zao.Nina uhakika huu ni muendelezo wa madhaifu ndani ya vyama vya siasa na serikali kwa ujumla ndiyo maana hatuna baraza huru la vijana.

  Suala la Chadema ni suala lililo ndani ya uwezo wetu tutajadili,tutashinikiza ndani ya chama hiki itakaposhindikana kama ilivyoshindikana ndani ya ANC ndipo tutakapofanya movement za wazi kama alizofanya Julius Malema na ANCYL.Nisome between the line...........!


  Hakuna cha ushabiki hapa.Hili ni suala linalohusu vyama vyote ikiwemo CCM.Ni jana tu kuna mijadala iliyokuwa inamuongelea Mwenyekiti wa NCCR na Kafulila,Huko CCM Nape alipokuwa anagombea uenyekiti wa vijana nae alfanyiwa ghiliba,Chadema tuna yetu tunayapigania sitayajadili kwa sasa hadi solution ishindikane, CUF wana yao kwenye nafasi ya ukatibu mkuu,TLP kwa sababu hakuna jumuiya ya vijana wameelekeza nguvu kusikostahili kwa Hamad Tao.Ni yapi yasiyojulikuana saa hizi?

  Sijui Nyerere alipokuwa anaongea ukweli kuhusu mapungufu ya chama chake na serikali kwa nini hakufukuzwa.Tuige basi angalao aina ya siasa wanayofanya Raila Odinga na chama cha ODM na Akina Ruto,Kosgey na wenzake.Naona political immaturity na maslahi binafsi vinatuwekea ukungu katikati ya daraja la Demokrasia,daraja lililotoboka! Afrika,eish!
   
 15. B

  BigMan JF-Expert Member

  #15
  Nov 10, 2011
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,097
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  mbowe ni miongoni mwao rejea jinsi walivyomsambaratisha zitto kwa kuwatumia hakina mzee mtei na wazee wengine wa kichaga wenye chama chao cha cdm pamoja na jinsi chacha wangwe alivyochomolewa
   
 16. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #16
  Nov 10, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  You are entitled to your opinion. Malema ana mapungufu yake,pia ninamfahamu kuliko unavyofikiri.The bottomline ni nini suluhisho la yale aliyokuwa ana-address? kumbuka aliungwa mkono na makundi mengi ikiwamo vyama vya wafanyakazi

  No wonder tunamuongelea Morgan Tsavangirai kama hero kisa ni mpinzani.Si kila mpinzani Afrika ni admirable na si kila chama tawala ni admirable.wapinzani kama akina Morgan Tsavangirai ni Disguist,ni fedheha sio MDC yote maana kuna wenye akili kama akina Tendai Biti

  Mbona verdict ya ANC haijaongelea kuhusu rascism?Does it mean wanakuwa more concerned na mambo ya kuangusha serikali ya Botswana than incitement of genocide and threat of sub-nationalism within the borders?For God sake ni nani mshauri wa rais kwenye maswala ya Peace and security,je walichambua na kuweka mezani kabla ya kuchukua uamuzi juu ya security analysis of external-Internal threats kweli?
  Kuhusu land Grabbing na Nationalization of minings niliwahi kumweleza ni lazima kuwe na framed models kama za Chile nilipokutana nae Nairobi mwezi February na pia Mwezi July.

  Hata hivyo hoja ambazo zilitolewa na chama cha wafanyakazi kuhusu njia zitakazotumika zilikuwa viable.Ni lazima tukubali maamuzi yaliyofanyika ni mwendelezo wa ghiliba za wanasiasa kwa vijana na maskini wa nchi za Afrika bila kutoa suluhisho.kigezo cha nidhamu kilichotumika kitazuia vipi division ndani ya chama na serikali zaidi?Tuache ushabiki let us face the problems
   
 17. Y

  Yakuonea JF-Expert Member

  #17
  Nov 10, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 601
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Malema amekuwa mkorofi mno, na amekuwa akitumia vijana for pushing his own agenda, hata baada ya kupewa 'suspended sentence' wengi tulifikiri angejirekebisha lakini alizidisha ukorofi pamoja na back up ya winnie mandela, Tokyo Sexwale, Fikile Mbalula na wengine ilikuwa ni dhahiri this time asingepona, sidhani kama alikuwa ni mfano mzuri wa kuiga,alijisahau sana na alifikiri he is untouchable
   
 18. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #18
  Nov 10, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,063
  Likes Received: 7,529
  Trophy Points: 280
  Ben.....nadhani unaelewa vyema kuwa tunapohitaji viongozi huwa hatutafuti toka kundi la malaika bali miongoni mwetu wanaadam ambao hatuyakosi mapungufu but how we deal with them.
  Kama tuna mapungufu sawa lakini si kuyaendekeza.
  Katika mtazamo wangu mimi, kwangu Malema alikuwa ni Daytime friend but a night time.............
  Tabia ambayo ni moja kwa moja inam disqualify a hero/heroin from the upper position to the root level.
   
 19. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #19
  Nov 10, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Ben,

  Au hujui Siasa au unajua ila hapa unatuimbia ule wimbo wa Ludacris wa "act like a ....."

  Kumtetea Mugabe inabidi uwe na akili za Mlevi ndiyo utaona haswa maana ya Mugabe. Kwanza ukisema Mugabe ni mzuri, hapo hapo unajipunguzia maksi zako maana kila mwenye ufahamu, anajua kuwa chama chake kipo hoi na wanagombania kila kinachowezekana na wanajua kuwa siku Mugabe akifa au kuacha kazi, basi utakuwa mwisho wao. Dawa iliyopo ni kumuacha pale juu kama picha (Yeltsin wa Russia) huku kakundi fulani kakijitajirisha kwa haraka iwezekanavyo. Sijui kama ulikuwa unalijua hili.

  Julius Malema ni watu kama Adlof Hitler ambao siku zote wana maneno matamu sana na kutumia hali halisi iliyopo nchini kutatua matatizo kwa kutumia njia za mkato. Hata akiwaua Boers wote wa SA na au wakimbie, jamaa wataondoka na mali zao zote na kibaya zaidi ni Techniical Know How. Hitler alitumia mabavu kuwafungia watu jela na baadaye kuanza kuwatumikisha. unatumia ubongo wako unaishi safi tu ingawa upo jela au hutumii basi Nywele zako zitaenda kutengeneza Sabuni na mwili kuchomwa kwenye tanuri.

  Malema kutengeneza Concentation Camp hawezi na ukweli utabaki kuwa Wazungu wakiondoka, SA kwishieni.

  Malema ni mtu MLEVI sana. Alishakiri hata kwenye BBC Hardtalk kuwa alikuwa akinywa sana na pombe ndiyo imemuharibu hata sura yake. Jamaa anavaa nguo za bei mbaya sana na kajenga jumba la kutisha. Majibu yake yalikuwa yameenda shule kidogo na si kama ya mwenzake mmoja aliyedai "anaishi kimjini mjini." Alidai kuwa nyumba ni mali ya Bank (Amekopa...!!! ingawa mchezo wa kukopa tunajua maana unakopa na kuwa unalipa kidogo kidogo wakati huo Bank nyingine una account ya kulipa deni lote). Gari alidai kama Riz1 kuwa anatumia magari ya vigogo wa ANC na mojawapo ni hilo Rangerover lake. Kuhusu Nguo za bei mbaya kama Gucci na Prado, alidai kuwa na yeye ni binadamu na hizo zimetengenezwa kwa ajili ya binadamu.

  Ila cha kushangaza, hao anaowatetea, hata msosi wao una wasiwasi. Yeye anataka tu kumnyang'anya Mzungu na ajipe yeye kwanza na kisehehemu ndiyo awagawie hao weusi wengine. Kwa umasikini na ufinyu wa akili kama CCM na Watanzania, watu wananunua hayo maneno ya kumuona jamaa ana akili sana. Ni mtu wa kuogopwa kama ukoma na wewe kama utaaanza kujipa image za akina Malema, ni poa tu kuwa tumeanza kukuona sura yako mapema.

  Hebu muone huyo jamaa yako akisisitiza Wazungu wauwawe. Wazungu ambao babu zao wamezaliwa hapo, sasa aende wapi?

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #20
  Nov 10, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hivi hawezi hama chama aendeleze mapambano?
   
Loading...