Jaguar
JF-Expert Member
- Mar 6, 2011
- 3,438
- 1,026
Mwalimu mmoja alienda shule moja ya kijijini kusimamia mitihani.Alipokuwa akiendelea na zoezi la usimamizi,alishangaa wanafunzi wote wametulia attention bila kuandika chochote.Mara ukasikika mdundo mmoja wa ngoma,watahiniwa wote kwa mpigo waliinama kuandika jibu,halafu wakatulia tena.Ikasikika midundo mitatu,wanafunzi wakainama tena kuandika halafu wakatulia tena.Msimamizi akaamua kutoka nje kufuatilia ile midundo ya ngoma inakotokea,cha ajabu alimkuta mwalimu mkuu wa shule chini ya mti akiwa na ngoma pamoja na copy ya ule mtihani uliokuwa ukifanyika muda ule.Kumbe mkuu wa shule alishawaambia wanafunzi wake,mkisikia mdundo mmoja wa ngoma basi jibu ni A,midundo miwili=B,mitatu=C n.k.[hii ilitokea kweli huko mbozi vijijini]