ShesRise_1
JF-Expert Member
- Aug 21, 2025
- 22,705
- 52,027
Je, ni kifo kipi bora: kufa ukiwa umesimama au ukiwa umepiga magoti?
For me ShesRise_1 najua kifo ni kifo
Kama mtu mmoja maarufu alivyosema
Nukuu: Kifo ni kifo !
Lakini kufa ukiwa umepiga magoti, ukilamba miguu ya adui yako ili tu akuache uendelee kuishi ni jambo ambalo kwangu ni gumu kulielewa na kulikubali
Labda upige magoti kwa lengo la kujipanga upya, lakini si kwa lengo la kujisalimisha
Afadhali kusimamia misimamo yako kupigania unachoamini na kukubali matokeo yake kuliko kuisaliti nafsi yako kwa ajili ya kuendelea kuishi
Na kama kuishi kwenyewe ni kuishi kwenye uchungu mwingi kuliko furaha, sasa maisha ya namna hiyo yana faida gani?
Maana mwisho wa siku.si suala la kuishi kwa muda gani bali ni namna gani umeishi na ni misingi gani uliisimamia
Huwezi kuishi kwenye dunia hii kama nyama ya nyongeza buchani ukisubiri tu wengine waamue hatima yako
Watu waovu hudhani watu wenye misimamo ni wajeuri na wenye kiburi
Wanasema hivyo kwa sababu hawajui kutofautisha kati ya kiburi, jeuri na kuwa na msimamo
Hawajui kutofautisha au wanajua lakini wanapuuza tu
Lakini je wewe unaonaje?
Utakufa huku umepiga magoti au ukiwa umesimama?
Au utapiga goti ili kujipanga upya na kuinuka tena?
Usiku ni mrefu ila kutakucha tu no matter what 😊
ShesRise_1 🤚