bless on
JF-Expert Member
- May 22, 2026
- 684
- 1,586
Acha uoga na ufungue akili yako.Kuzaliwa na kufa ni biashara ileile moja.
Watu wengi mnaishi kama watumwa wa uoga. Mnaogopa kuzikwa ardhini wakati mmesahau kuwa mmetoka kwenye giza nene kule tumboni kwa mama zenu.
Na Kifo ni kurudi huko huko ulipokuwa kabla ya kuzaliwa, maana hii ni hali moja.
Mimi siogopi kufa hata sekunde moja, kwa sababu najua kabisa sikuogopa wakati nazaliwa. Kuzaliwa na kufa ni jambo lilelile. Wale wanaopiga mayowe na kulia sana kwenye mazishi ni watu wasiojua hesabu rahisi za maisha.
Kifo ndicho kinachofanya maisha haya yawe na thamani, maana tunarudi kule kule tulipokuwa kabla ya kuzaliwa.
Mimi na wewe ni wasafiri tu hapa. Acha kulialia na kuleta uoga wa kijinga. Tunarudi kule tulikokuwa kabla hatujazaliwa.
Ulikuja hapa duniani huna hata nguo ya ndani, huna jina, huna hata mia mbovu mfukoni.
Hivyo basi hakuna haja ya kuogopa kufa ingali unajua hukuogopa kabla hujazaliwa...
Kifo ni kurudi kule kule. Kama hukulalamika ukiwa ndani ya tumbo unazaliwa, unalalamika nini unaporudi kufa?.
Wakati hali ni zile zile, kufa na kuzaliwa ni kitu kile kile...
Kwaiyo hakuna haja ya kuogopa utakufaje kufaje.
Wewe kazi yako ni kuishi, Kwani siku unazaliwa, ulijua utazaliwa vipi? Ulijua kama utazaliwa salama au kwa shida? Hukujua! Asili ilikutoa huko ulikokuwa na ikakuleta hapa duniani salama. Ikiwa asili iliweza kukuleta, ina uwezo wa kukurudisha bila kukuomba ushauri.
Acha kimbelembele cha kutaka kupangia asili namna ya kukutoa!
Unajifanya unawajali sana ndugu zako, lakini ukweli ni kwamba unaogopa nafsi yako! Kabla hujazaliwa, hao ndugu walikuwa wanakula na kulala vizuri tu. Na ukishasepa, wataendelea na maisha yao, watakula pilau kwenye msiba wako, na maisha yataendelea.
Wacha wasikuelewe, wacha waone unaweweseka, lakini wewe simamia ukweli mmoja Kuzaliwa na kufa ni biashara moja, Hakuna kuogopa.