Kuepuka Radi kwa kufuga Kondoo

Status
Not open for further replies.

stephot

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2012
Messages
9,662
Points
2,000

stephot

JF-Expert Member
Joined Mar 1, 2012
9,662 2,000
Wana JF wenzangu, kuna kipindi nilipokuwa likizo nilitembelea mikoa ya Dodoma,Singida,Manyara na Arusha,nilichokigundua ni kuwa wafugaji karibu wote wa Ng'ombe wanakuwa na kundi la Kondoo, nilipouliza niliambiwa kuwa Kondoo wanasaidia kuzuia Radi,mwenye ufahamu wa kina naomba anifafanulie utaalamu uliopo nyuma ya hii kitu.
 
Nyenyere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Messages
11,932
Points
2,000

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined Sep 9, 2010
11,932 2,000
Wana JF wenzangu, kuna kipindi nilipokuwa likizo nilitembelea mikoa ya Dodoma,Singida,Manyara na Arusha,nilichokigundua ni kuwa wafugaji karibu wote wa Ng'ombe wanakuwa na kundi la Kondoo, nilipouliza niliambiwa kuwa Kondoo wanasaidia kuzuia Radi,mwenye ufahamu wa kina naomba anifafanulie utaalamu uliopo nyuma ya hii kitu.
Naam niliiona hiyo kitu Shinyanga vijijini. Kwamba radi huja kama jogoo, na inapokutana na kondoo hupigana sana na mara nyingi radi hushindwa.
 
kahtaan

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2009
Messages
17,488
Points
2,000

kahtaan

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2009
17,488 2,000
Naam niliiona hiyo kitu Shinyanga vijijini. Kwamba radi huja kama jogoo, na inapokutana na kondoo hupigana sana na mara nyingi radi hushindwa.
Halafu mtu kama wewe unajisifu umeenda shule!?
Teh teh teh teh!

Afadhali nimedaka hapa unaandika utumbo! Ntauhifadhi huu utumbo siku nyingine ukileta yale majigambo yako ya kusema wewe msomi!

Radi ya jogoo my foot!
 
Makanyaga

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2007
Messages
4,076
Points
2,000

Makanyaga

JF-Expert Member
Joined Sep 28, 2007
4,076 2,000
Halafu mtu kama wewe unajisifu umeenda shule!?
Teh teh teh teh!

Afadhali nimedaka hapa unaandika utumbo! Ntauhifadhi huu utumbo siku nyingine ukileta yale majigambo yako ya kusema wewe msomi!

Radi ya jogoo my foot!
Hapana, usimkatalie. Vitu spiritual mara nyingi nimekuja kugundua kuwa havikubaliani na sayansi ya kawaida na mara nyingi vinakuwa havina logic!
 
kahtaan

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2009
Messages
17,488
Points
2,000

kahtaan

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2009
17,488 2,000
Hapana, usimkatalie. Vitu spiritual mara nyingi nimekuja kugundua kuwa havikubaliani na sayansi ya kawaida na mara nyingi vinakuwa havina logic!
Makanyaga huyo Nyenyere anaonekana anatumia yale majani yalioharamishwa.
Sasa akishakula ile maneno anaona vitu vya ajabu ajabu. Juzi hapa alisema kaenda kumpoke yesu! Nikamuuliza je kaja kwa basi au treni. Akaanza matusi!
Huyu jamaa wazee wake wameshapata hasara kubwa sana!.
Faida hakuna kazi kujaza choo tu.
 
Last edited by a moderator:

Kennedy

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2011
Messages
19,499
Points
2,000

Kennedy

JF-Expert Member
Joined Dec 28, 2011
19,499 2,000
Makanyaga huyo Nyenyere anaonekana anatumia yale majani yalioharamishwa.
Sasa akishakula ile maneno anaona vitu vya ajabu ajabu. Juzi hapa alisema kaenda kumpoke yesu! Nikamuuliza je kaja kwa basi au treni. Akaanza matusi!
Huyu jamaa wazee wake wameshapata hasara kubwa sana!.
Faida hakuna kazi kujaza choo tu.

Mkuu umenikumbusha dada yangu mmoja
yupo Dar basi alikuwa kipindi cha 2001
atuambia wadogo zangu kuzaa sio kupata

Ni kutoa Mchango mchafu tumboni yaani
unakuta mtoto akiwa mimba wanasema
huyu mtoto asingezaliwa basi angemuuwa

Mama yake akiwa tumboni.
Teh teh ha ha kwi kwi

Kondoo ni Ant- thunderstorm Tz ina rasimali
nyingi sana mpaka nakuwa km JK sijui kwanini
ni masikini .
 
Last edited by a moderator:

CYBERTEQ

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2012
Messages
7,385
Points
0

CYBERTEQ

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2012
7,385 0
Ni imani tu ya wafugaji kwa sababu ni mara chache sana kondoo kuuwawa kwa radi!

"A horse can get zapped by less than 2,000 volts and will almost never try the fence again, whether it's turned on or not. 2,500 volts will easily turn a cow but you better have a good 4,500 volts to even get a sheep's attention"
 
East African Eagle

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2013
Messages
3,761
Points
1,195

East African Eagle

JF-Expert Member
Joined Jul 26, 2013
3,761 1,195
Wana JF wenzangu, kuna kipindi nilipokuwa likizo nilitembelea mikoa ya Dodoma,Singida,Manyara na Arusha,nilichokigundua ni kuwa wafugaji karibu wote wa Ng'ombe wanakuwa na kundi la Kondoo, nilipouliza niliambiwa kuwa Kondoo wanasaidia kuzuia Radi,mwenye ufahamu wa kina naomba anifafanulie utaalamu uliopo nyuma ya hii kitu.
Wanyama wana uwezo mkubwa wa ku-sense natural disasters.Kukiwa na radi inataka kupiga eneo kondoo huanza kubadilika tabia akienda huko na huko kwa hasira ya mapigano mara ingine kugonga miti.ukiona yuko hivyo radi inataka kupiga eneo hilo usikae chini ya mti wowote kukokoa maisha yako na kama uko karibu na daraja kaa mbali nalo. Wachungaji wa mifugo kondoo kawasaidia mara nyingi kujua ujio wa radi na namna ya kujiokoa.

Wakati wa Elnino kabla haijatua kule Asia wanyama kama nyoka,mbwa na paka na wanyama wa mwituni walianza safari ya kutoroka kutoka maeneo tambarare na na kuanza kuhamia milimani ilikuwa ni mass exodus ya wanyama ambayo watu waliona tu kama kituko cha wanyama wakieelekea kwenye miinuko lakini watu hawakujali kuwa ni kwa nini wamekuwa hivyo.Elnino iliposhuka watu wengi walikufa .Watu wangewahi kufuatana na wanyama pengine vifo vingepungua.

Kukiwa na nyoka mfano hatari mahali mbwa ana uwezo wa ku-sense na kubadilisha tabia na mlio na wanyama kama ng`ombe kukiwa na kitu fulani hatari jirani kikubwa hunyanyua mikia juu na kuruka kwa nguvu kwa hasira.Ukiona hivyo mwenye mifugo unatoka na silaha tayari kwa mapambano.

Kondoo ni mnyama atumikaye kwa matambiko na makafara kwa dini zote na washirikina pia.Kwa sababu za miiko kuna mambo siwezi kueleza uwezo mwingine kondoo alionao na anavyotumika ila ninachoweza kusema ni kuwa radi haiwezi piga kondoo milele.Kondoo hapigwi na radi hata siku moja.Radi ni mtoto mdogo kwenye kichwa cha kondoo.
 
Status
Not open for further replies.

Forum statistics

Threads 1,391,011
Members 528,343
Posts 34,070,168
Top