SoC02 Kuenea kwa usugu wa vimelea na vimelea sugu vya magonjwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu kupitia matumizi ya mbolea za wanyama katika kilimo

Stories of Change - 2022 Competition

Mabula marko

Member
Jul 18, 2022
36
36
DIBAJI
Katika dunia ya leo ambayo muingiliano wa shughuli za kilimo na maisha ya binadamu vinaongeza utegemeano ongezeko la magonjwa sugu linaongezeka siku hadi siku kutokana na hali kwamba , matumizi ya mbolea kutoka kwa wanyama na biandamu katika kilimo hususani kilimo hai yanaongezeka na kufika kwa binadamu kupitia mazao zalishwa kama mboga mboga na matunda ambayo mara nyingi huzarishwa kwa kutegemea aina hiyo ya mbolea(S.Kiraci2018) .

Mara nyingi vimelea sugu hivi na hali hii ya usugu hujitokeza katika wanyama kufuatia matumizi hafifu ya dawa hususani kiuavijasumu katika kiwango kidogo au vilivykwisha muda wake wa matumizi au kuchanganywa katika vyakula vya wanyama hali ambayo imepelekea kuwa na wimbi kubwa la magonjwa yasiyotibika na kiuavijasumu vingi kwa binadamu hali inayokadiliwa kuwa kufikia mwaka 2050 (A Checcucci2020) Vijiuavijasumu nyingi hazitakuwa na uwezo wa kukinga tena magonjwa ambayo zamani ziliweza kuyatibu.Kutokana na hali hii kuongezeka kwa kasi ikalazimu kuja na njia zitakazoweza kupunguza uwezekanowa

Neno muhimu ; Vimelea sugu, kilimo hai, Usugu wa vimelea, Kiuavijasumu na mbolea

UTANGULIZI
Kutokana na agenda ya malengo endelevu ya dunia ya mwaka 2030 Afya ya mwanadamu ni lengo mkakati pia kuzuia njaa , kukomesha umasikini na mabadiliko ya tabia ya nchi ambapo dunia iliona kunahaja ya kuja na ajenda hizo kulingana na kuongezeka kwa watu duniani ,kutokana na idara ya uchumi na uhusiano wa kijamii ya umoja wa mataifa mwaka 2050 idadi ya watu itafikia billion 9.735 hali ambayo itapelekea mabadiliko makubwa ya hali ya mazingira ,maisha na uhitajikaji wa chakula ni unaongezeka pia ili kufanya afya ya binadamu iwe imara ,tabia ya nchi kuimarika na kukomesha umaskini haya yote huambatana na kuongezeka kwa shughuli za kilimo hususani kilimo hai ambacho huhimiza matumizi ya mbolea za wanyama na zile zitokanazo na binadamu ikiwa lengo ni kutunza ardhi isiharibikena pia kuhifadhi rutuba wezeshi kwa ustawi wa mimea , hali ambayo imekuwa ikichangia ueneaji wa vimerea sugu na usugu wa vimelea kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu kupitia vyakula zalishwa kama mboga mboga na hivyo kuadhiri afya za watumiaji wa mazao hayo(A.Mann 2021).

USUGU WA VIMELEA .hii ni hali ya vimelea vya magonjwa kuwa na uwezo wa kuzuia kiuavijasumu hali hii ni hujitokeza kutokana na mabadiliko ya vinasaba kwa vimerea hivyo VIMELEA SUGU. Hii ni aina ya vimelea ambavyo tayari vimeshakuwa na uwezo kujizuia visiweze kuasiliwa na kiuavijisumu ambacho hapo awali kilikuwa kikiathiriwa(A.Mann2021)

Kusambaa kwa vimelea vya magonjwa kuja kwa binadamu kutoka mashambani mara nyingi huwa ni kupitia vyakula zalishwa kama mboga mboga na matunda ambayo hulimwa kwa kutumia mbolea za wanyama hivyo mara zote hugusana na mbole hizo au maji maji ambayo yamekwisha changanikana na vimelea hivyo mchoro kufafanua kwa uchache jinsi mzunguko wa vimelea sugu hufika katika mazao baadae kuingia kwa binadamu kupitia chakula

Vimelea bacteria kama vile salmonella, Escherichia coli, campylobacter ,listeria, Yersinia na protozoa kama cryptosporidium na giardia hupatikana katika kinyesi cha wanyama na kinaweza kufika kwa binadamu na kumdhuru na vinaweza kutoka tayari vikiwa vimeshajenga usugu kutokea kwa wanyama na hivo punde tu binadamu akishakwisha kupata vinakuwa haviwezi tena kutibika(T.lima 2020)

MADHARA KWA BINADAMU, WANYAMA NA AFYA YA MAZINGIRA KATIKA MTAZAMO WA AFYA MOJA
Usugu wa vimelea umekuwa ukiangaliwa kama moja ya changamoto za AFYA MOJA(One health) ambazo mara zote huhitaji uangalizi wa karibu Zaidi na kuwekewa mipango ya uthibiti ili kuzuia mlolongo wa ueneaji wa usugu wa vimelea toka kwa wanyam –binadamu-mazingira

Kama tulivyokwisha kuona kwamba mbolea za wanyama na binadamu zina vimelea wenye usugu , vinasaba vya vimelea sugu ikitumika katika kilimo huweza kupelekea vimelea hao na vinasaba hivyo kuchafua mazingira na kupelekea mazingira kuwa sio salama kwa viumbe wengine ikiwemo binadamu mwenyewe kwasababu vinasaba vinaweza kuingia katika mwili wa binadamu na kusababisha vimelea vingine vya magonjwa kuchukua usugu huo kutoka kwa vinasaba hata kutoka kwa wanyama wasio fanana na kufanya binadamu kuwa na magonjwa sugu na hali ya kuongezeka kwa usugu wa magonjwa kila siku na pia kuibuka kwa magonjwa mapya kila siku

Mara nyingi mazingira huwa kama daraja kwa namna moja ama nyingine kwa vimelea kutoka kwa wanyama kwenda katika mbolea kwenda kwa ardhi na baadae maji na mabaki wakati huo huo mazingira huhifadhi vinasaba safirishi ambavyo vinaweza safiri na kuingia kwa binadamu na hata wanyama pia(A.Mann 2021)


NAMNA YA KUPUNGUZA VIMELEA KATIKA MBOLEA ZA WANYAMA NA BINADAMU KABLA YA KUTUMIKA

Mara nyingi uwezo wa vimelea kuishi katika mbolea na mazingira hutegemeana na sifa za kila kimelea na vile vile sifa za kikemikali za mbolea kama vile joto,ammonia, PH, oxygen pamoja na hali ya unyevu nyevu ya mbolea hivo mbolea inapaswa kutishwa katika hali Fulani ya kupunguza vimelea hatarishi vya magonjwa ambavyo vinaweza kumfikia binadamu na kumsababishia magonjwa sugu yasiyo tiba kabisa (CE.many-loh 2016)

Kuna njia kadhaa za kuweza kuzuia au kupunguza hali hii kama ifuatavyo

Kukausha mbolea katika hewa;
njia hii husaidia kuuwa vimelea kwa kuiweka mbolea katika ardhi kwa muda katika hewa na jua hali ambayo hupelekea baadhi ya vimelea kufa hasa vile visivyo hitaji joto na vile visivyo hitaji hewa pia mara nyingi ufanisi wa njia hii hutegemea sana sana idadi ya siku na muda wa kukaushwa katika kipindi cha jua hukaushwa muda mfupi na katika kipindi cha unyevu nyevu hukaa siku nyingi Zaidi

Kuzuia kwa kutengeneza mboji; Njia hii mara nyingi huwauwa vimelea wa magonjwa katika uwepo wa hewa ya oksijeni , hii imekuwa ikifanya vizuri kwa vimelea kama E.coli na salmonella(gurtler et al.,2018)

Kuchoma mbolea; Njia hii huhitaji joto katika uwepo wa oksijeni joto la nyuzi joto 850 ,mbolea hubadilishwa kuwa majivu ambayo baadae huwekwa katika udongo ikiwa salama(Turner et al.,2000)

Kuzuia kwa kutengeneza biogesi; Njia hii hufanyika katika tanki ambazo hazina hewa ya oksijeni hali ambayohupelekea vimelea kufa huku vikisaidia kutoa gesi(Font-palma2019)

HITIMISHO
Uzuiaji wa vimelea vya magonjwa, usugu na vimelea sugu kutoka kwa wanyama kwenda kwa binandamu ni mhimu sana kwa dunia ya leo kutokana na hali kuongozeka siku hadi siku na kuongezeka pia kwa magonjwa yatokayo kwa wanyama kuja kwa binadamu hasa katika nchi zinazoendelea kama ilivyolipotiwa na shirika la Afya duniani, Jamii ikielewa zaidi mzunhuko huu tutapunguza magonjwa mengi yanayozidi kuibuka Sikukipiga had Sikukipiga katika nchi yeti na dunia kwa ujumla
 
Back
Top Bottom