SoC02 Ongezeko la magonjwa ambukizi toka kwa wanyama kwenda kwa binadamu

Stories of Change - 2022 Competition

Mabula marko

Member
Jul 18, 2022
36
36
UTANGULIZI

Dunia imekuwa ikishuhudia mlipuko wa magonjwa toka kwa wanyama kwenda kwa binadamu na kushuhudia vifo vingi vikitokea tangu zamani sana, ugonjwa wa tauni ni moja ya magonjwa hatarishi kutokea hapa ulimwenguni ukisadikika kutokea miaka ya 1334 ukianzia Asia na kuenea maeneo ya Ulaya kupitia wafanyabiashara. Ugonjwa huu unakadiriwa kuua zaidi ya watu milioni 25 kwa mujibu wa historia ugonjwa huu ulisababishwa na bacteria ambaye hukaa ndani ya wanyama hususani jamii ya panya. (www.nationalgeographic.com2019)

Pia ugonjwa wa mafua ya nguruwe huu ulikuwa umetawanyika maeneo mbali mbali ulimwenguni shirika la afya duniani WHO linakadilia kuwa ugonjwa uliua watu laki 284,000 miaka ya 2009 na 2010, dunia pia imeshuhudia ugonjwa wa mafua ya ndege ambao binadamu huupata kutoka kwa jamii ya ndege kama kuku na wengine ambao pia ulikuwa janga kubwa na kipindi cha hivi karibuni dunia imeshuhudia ugonjwa wa corona ambao pia umekuwa janga kubwa na ukishuhudia kuua maelfu na maelfu ya watu ,biashara zikifungwa na nchi zikiwekeana mazuio mbali mbali , Dunia pia imeshuhudia ugonjwa ukimwi (HIV/AIDS) uliotokana na wanyama pia ukizidi kuwa tishio hadi sasa huku ukiwa umeuwa watu wengi Zaidi kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO.

Barani Afrika kutokana na shirika la afya duniani WHO kumetokea visa vingi vya magonjwa yatokanayo na wanyama na hadi sasa kuna ongezeko la hadi 63% katika muongo mmoja wa (2012-2022) ukilinganisha na (2001-2011) na kumesababisha vifo vingi vya watu ugonjwa wa ebola huko kongo na Africa ya kati kwa ujumla na vile vile hivi karibuni homa ya nyani huko Ghana na visa vingine vya ugonjwa kimeta , homa ya dengue na visa vingine.

Nchini Tanzania mara kazaa tumeshudia kukiripotiwa magonjwa kama mafua ya ndege, homa ya bonde la ufa kifua kikuu kitokanacho na wanyama, kichaa cha mbwa na hivi karibuni maeneo ya lindi visa vya ugonjwa wa mgunda na ugonjwa hatari wa ukimwi ambao nao ulitokana na wanyama ukizidi kuwa tishio kila mahali
Magonjwa ambukizi ni aina ya magonjwa ambayo wana ugua wanyama au huhifadhi vimelea vya ugonjwa husika na unaweza kuambukizwa kwa binadamu na binadamu akaugua mfano brucelosisi , homa ya bonde la ufa na magonjwa mengine kama mgunda na kichaa cha mbwa magonjwa haya yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku hasa katika bara la Africa kwa mjibu wa shirika la afya duniania WHO.


SABABU ZA KUONGEZEKA KWA MAGONJWA AMBUKIZI KUTOKA KWA WANYAMA KWENDA KWA BINADAMU

Kutokana na ripoti ya umoja wa mataifa UN yam waka 2020 magonjwa haya yanatokana na ongezeko la shughuli za binadamu zinazopelekea uharibifu katika makazi na mfumo wa maisha ya wanyama kwa ujumla (ripoti ya UN kitengo cha mazingira), kuna sababu zingine kama.

- Kuongezeka kwa kasi kwa idadi ya watu inayopelekea kuongezeka kwa mahitaji ya vyakula vitokanavyo na wanyama. ni ukweli usiopingika kwamba leo hii mahitaji ya mazao toka kwa wanyama kwani katika siku mtu huweza kutumia chochote kitokanacho na wanyama yaweza kuwa maziwa, nyama au mayai na samaki hali ambayo imepelekea sasa binadamu anaweza pata kwa urahisi kwa magonjwa kama kifua kikuu, minyoo aina ya taenia na mafua ya ndege ambayo ni moja kwa moja hutoka kwa wanyama wafugwao lakini pia corona ambayo imetoka kwa panya anaetumika kama chakula kwa jamii baadhi ya watu.

- Uharibifu wa maeneo ya wanyama pori.kuongezeka kwa watu kwa kasi kumepelekea pia kuharibu maeneo ambayo yamekuwa yaakikaliwa na wanyama mwitu kama nyani na wanyama wengine ujenzi wa barabara, rail, uchomaji misitu na makazi kwa jamii za kifugaji umeleta mchango mkuwa wa magonjwa haya kujitokeza siku hadi siku kwani wanyama waliokuwa wakiathiriwa na magonjwa hayo hawakuwa karibu na makazi ya watu na hawakuwa na uwezo wakukutana na watu lakini pia muingiliano wa watu na watu kwa urahisi umepelekea kusababisha madhara na kuenea kwa kasi sana kwa magonjwa haya kati ya binadamu na biandamu na(chuo kikuu cha Montpellier na aix-marseille).

- Mabadiliko ya tabia ya nchi. hali imekuwa changamoto kubwa hasa katika bara la Africa ambako shughuli za binadamu zimekuwa zikizidi kuharibu mazingira siku hadi siku hali ambayo imekuwa ikiwa radhimu watu kufyeka na kuharibu mazingira huku akizidi kujiweka karibu na wanyama ambao huishi na magonjwa na vimelea vya magonjwa lakini pia kujitokeza kwa hali inayoweza kufanya wazaliane kwa wingi Zaidi hasa magonjwa ambayo mwanzo yalikuwa nyanda za joto kama.

  • Shughuli za kilimo horera. shughuli za kilimo kama vile ufugaji wa nguruwe horera bila mpangilio umekuwa sababu kubwa ya kutokea kwa janga kama vile ufugaji wa nguruwe ulivosababisha homa ya mafua ya nguruwe iliyopelekea vifo vya watu wengi duniani.

  • Biashara za wanyama pori,mazao yake na matumizi yake kwa ujumla. Kumekuwa na ongezeko la vimelea hata wasiotambulika toka kwa wanyama pori hasa pale mazao yao yanapotumika kama vile nyama, ngozi na hata wanyama hai pia wamekuwa chocheo la magonjwa mbali mbali kutokea hasa wakati wa mrorongo mzima wa biashara hizi.

  • Kusafiri na usafirishaji. safari kutoka sehemu moja kwenda nyingine imekuwa ikichangia kwa namna moja ama nyingine kujitokeza kwa magonjwa haya katika maeneo ambayo mwanzo hayakuwa na changamoto ya magonjwa hayo na kusababisha kuongezeka kwa magonjwa haya ambukizi toka kwa wanyama kwenda kwa binadamu.


NJIA ZA KUWEZA KUZUIA ONGEZEKO LA MAGONJWA AMBUKIZI TOKA KWA WANYAMA KWENDA KWA BINADAMU

Magonjwa mengine yanayojitokeza na kuongezeka kwa namna moja amna nyingine yanaweza zuilika au kuyapunguza kasi ya uongezekaji ingawa hutegemeana na aina ya vimelea visababishi kuna njia nyingi kama ifuatavyo.

  • Tafiti za kisayansi na maendeleo ina paswa kuongeza katika Nyanja na mianya iwezayo kusababisha kuongekezeka kwa magonjwa hivo tafiti zinapaswa kuwepo, kuwepo kwa vipimo, chanjo na matibabu yanayowekanika lakini pia kunapaswa kuwepo tafiti zinazo weza kungundua mahali vimelea walipo , njia za uambukizaji ili kusaidia kuzuia uwezekano wa magonjwa kuibuka na kusambaa.

  • Ushirikishwaji wa jamii na utolewaji wa elimu. Kunahitajika ushirikishwaji wa jamii na kutolewa kwa elimu juu ya magonjwa hayo, wanasayansi na serikali wanapaswa kutoa elimu kwa watu ili waweze kuwa na uelewa mkubwa juu ya magonjwa hayo, njia zitumikazo kuenea kwa ugonjwa na namna ya uzuiaji wa hayo magonjwa katika jamii, kama unawaji wa mikono baada ya kugusana na wanyama.

  • Kuimarishwa kwa mahusiano ya taasisi zote zinazounda AFYA MOJA (one health) .kunapaswa kuimarika kwa ushirikiano baina ya taasisi kama vile shirika la afya duniani WHO, shirika la chakula duniani FAO, shirika la afya ya wanyama OIE katika kuweka mikakati mizuri ya kuzuia uibukaji wa magonjwa yatokanayo na wanyama.

  • Kuweka muongozo salama wakutunza wanyama. Hii ikiwemo kupima afya za wanyama kabla ya kusafirishwa kutoka eneo moja kwenda eneo jingine, usalama wa vyakula pia, ukaguzi wa vyakula kama nyama kabla ya kuruhusu kwenda kutumika kwa jamii.


HITIMISHO

Afya ya binadamu huteshabiana na usalama wa wanyama kwani magonjwa mengi yampatayo mnyama binadamu naye humpata, AFYA MOJA ni suluhisho kubwa kama ikizingatiwa vizuri kwani huwaleta pamoja wataalamu wa mifugo na binadamu pia.
 
Nimepitia nimepata faida.

Nimetamani sana kujua zaidi kuhusu ugonjwa wa tauni ila link haifunguki.
Nitafurahi kama nikijua historia ya ugonjwa huu kwahapa Tanzania
 
Back
Top Bottom