Kuendesha Gari huku Umewasha taa mchana, nini sababu??

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
29,459
29,156
Wadau,

Nimekua nikiona watu wanaendesha magari yao mchana huku wamewasha taa. Uwashaji huu sio ule unaohusiana na matukio ya dharura kama msiba, harusi, msafara au vingine.

Hata aina za magari yanayowasha taa ni zile za aina flani hivi ambazo labda ukiiuza moja basi unaweza kununua vi-Carina vyetu kama 8 au zaidi.

Sasa nimeshindwa kupata jibu juu ya hii tabia, nilipata kuwaza labda ni kutafuta attention kwa watu wengine waziangalie gari zao zilivyo kali.

Pia nikafikiri labda dashboard zao zina giza so inabidi wawashe parking muda wote.

Au pengine wanatoa tahadhari ili tusiwaguse/tusiwagonge maana gari zao ni expensive sana.

But yote ya yote sijapata jibu juu ya hii tabia. Wadau naombeni msaada wenu please.
 
Magari mengine by design yako hivyo. Kwa mfano najua Volvo wana tabia hiyo nadhani kwa sababu ya usalama kwenye nchi za ukungu n.k.
JEEP pia. Kwa hiyo ukiwasha gari tu na taa zitawaka. Kuna pikipiki pia zimetengenezwa hivyo. Haya hayaondoi pia uwezekano wa utashi wa mtu katika kuwasha taa akiwa barabarani. Mfano ni watu wa Mbagala. Kwa sababu wanatoka kwa usiku sana wakiwa wamewasha taa na wanafika mjini kumeshapambazuka wanasahau kuzima taa. Ukikutana nao hasa majira ya asubuni we elewa tu safari ni ndefu.!!
 
Wataalamu wa "Defensive Driving" wanashauri hivyo pia!
 
1) kuna baadhi ya magari hususani ya ulaya na yale ni automatic pindi uwashapo switch on na taa za parking zinawaka na mda mwingine zinakuwa na mwanga kulingana na hali ya hewa. Haya magari yanakifaa ambacho kinaakisi mwanga kama ni giza na yenyewe inabadilisha mwanga.
2) inategemea na ukubwa(Upana) kwani upana wa magari mengine ni tofauti na ya kijapani. mf. ford explorer,Mercedes Benz na pia ni kutoa tahadhari wawapo barabarani aidha kuna gari nyuma yenye mzigo mkubwa mf. caterpillar, greda
 
Wadau,

Nimekua nikiona watu wanaendesha magari yao mchana huku wamewasha taa. Uwashaji huu sio ule unaohusiana na matukio ya dharura kama msiba, harusi, msafara au vingine.

Hata aina za magari yanayowasha taa ni zile za aina flani hivi ambazo labda ukiiuza moja basi unaweza kununua vi-Carina vyetu kama 8 au zaidi.

Sasa nimeshindwa kupata jibu juu ya hii tabia, nilipata kuwaza labda ni kutafuta attention kwa watu wengine waziangalie gari zao zilivyo kali.

Pia nikafikiri labda dashboard zao zina giza so inabidi wawashe parking muda wote.

Au pengine wanatoa tahadhari ili tusiwaguse/tusiwagonge maana gari zao ni expensive sana.

But yote ya yote sijapata jibu juu ya hii tabia. Wadau naombeni msaada wenu please.

Continental Europe kwa sasa ni sheria. Katika baadhi ya nchi ukikamatwa unaendesha gari bila kuwasha taa kubwa unakamatwa, kwa kuwa kuna ajali nyingi zinatokea kutokana na fog. Kwa huku bongo kama mtu amewasha inawezekana anatumia gari ambazo ni automatic kwenye kuwasha hizo taa.

Lakini kuna wengine wanaiga tu hata bila kujua sababu, hasa mashororo na ma-b-show. So inategemea ni gari gani na nani anaendesha.
 
Nikiendesha kigari changu mchana, madreva na watu wa pembeni huniambia.."mkuu umesaahu kuzima taa..." ama wanatoa ishara kwa mkono kuashiria taa zinawaka. Natamani kuwaambia, ndivyo lilivyo hilo...taa lazima ziwake Hamijei... Ni kigari cha Ulaya!!
 
Ukiwa unasafiri mwendo mrefu kwenye barabara yenye magari yanayoenda kasi ya juu, eg Dar-Moshi, ni vizuri kuwasha taa. Dereva anayokuja upande wa pili atakuona toka uko kilomita kadhaa na atajua kabisa, na kwa dhati, kuwa wewe ni gari na siyo mbuzi. Mara nyingi ajali zinztokea kutokana na judgement errors za kitoto ambazo huambata na uchovu unapokolea.
 
Si bahati mbaya.Ni kawaida mno naamini Marekani asilimia 99 ya magari utembea yakiwa yamewasha taa si mchana wala muda gani.so ni kitu cha kawaida tu

Siyo bahati mbaya! Ni kwmb sana sana magari yanayowasha taa mchana inakuwaga ya gharama mara nyingi sana!
Kwa hiyo nitahadhari usije kugonga ukasema nilikuwa sijaona!
Litakuwa linakuhusu!
 
Continental Europe kwa sasa ni sheria. Katika baadhi ya nchi ukikamatwa unaendesha gari bila kuwasha taa kubwa unakamatwa, kwa kuwa kuna ajali nyingi zinatokea kutokana na fog. Kwa huku bongo kama mtu amewasha inawezekana anatumia gari ambazo ni automatic kwenye kuwasha hizo taa.

Lakini kuna wengine wanaiga tu hata bila kujua sababu, hasa mashororo na ma-b-show. So inategemea ni gari gani na nani anaendesha.
Ahsante kaka,
But mi nasemea hapa kwetu mtu yuko Posta mchana wa Saa saba, na taa kawasha.
Kikubwa nilicho-note ni kua gari hizi hua ni zile expensive. Yaani mtu huwezi kumkuta na ka Corrola Limited kake ka 4.5Mil akafanya hivyo, never.

Ni Ushamba??!!!
 
In Canada gari kama taa haziwaki muda wote haliruhusiwi barabarani ni sheria kabisa

Mi nasemea hapa Bongo Mwalimu wangu,
kwa wenzetu wanaweza hata kupata mwanga hafifu mchana bila hata ya kuliona Jua.
 
Ni kweli kuna nchi kama za Scandnavia ni sheria kuendesha gari taa zimewaka kwa kuwa kule kuna hali ya ukungu kila wakati. Na zaidi ya hapo utafiti ulifanywa ikaonekana kwamba gari zenye rangi za aina fulani huwa zinahusika sana katika kugongwa, kugongana na kugonga watumiaji wengine wa barabara kwa sababu hazionekani vizuri barabarani. Hivyo kuongeza visibility ya gari kwa watumiaji wengine wa barabara, unashauriwa unapoendesha gari za rangi hizo (nyeusi, kahawia, nyekundu, kijani, - isipokuwa rangi kama nyeupe, blue bahari, njano, silver nk) ni vema ukawasha taa has ukiwa kwenye barabara kuu. Kuna baadhi ya kampuni za insurance premium zinakuwa juu ikiwa rangi ya gari yako ni ile iliyo "accident prone".
 
Siyo bahati mbaya! Ni kwmb sana sana magari yanayowasha taa mchana inakuwaga ya gharama mara nyingi sana!
Kwa hiyo nitahadhari usije kugonga ukasema nilikuwa sijaona!
Litakuwa linakuhusu!
Hii nimeifikiria sana. But hua wanawasha hata kwa zile njia ambazo ni double road, yaani hakuna uwezekano wa wanaoenda njia opposite kugongana.

Assume kipande kama cha kutoka Namanga mpaka Posta (Zote Dar es Salaam), barabara zimetenganishwa kati ya wanaoenda na wanaorudi, so hata akiwasha taa za mbele sijui anakua anamu-allert nani maana wote mmegeukia upande mmoja.
 
Kuna gari zina taa fulani kama shanga shanga fulani. ukiwasha zile parking zinakua kama ka urembo fulani. so hawa wanawasha ku atract attention ya watu waone magari yao yalivyo makali.

Ha, ha, ha! Taa kama shanga! Mkuu au unaongelea LED lights. Ndiyo technology ya sasa ya taa, kwa matumizi ya ndani, magari na hata taa za barabarani. Ni kama zile tochi za wachina unazoona Kariakoo. Zinatumia umeme kidogo sana, mwanga mwangavu zaidi na zinadumu zaidi ya taa za kawaida. Ila bado ziko ghali kidogo. LED lights ni baada ya zile zilizokuwa zinaitwa CFL - compact fluorescent lights. LED technogy imeeingia hata kwenye TV, picha inakuwa na quality ya juu sana (LED TVs).
 
Ahsante kaka,
But mi nasemea hapa kwetu mtu yuko Posta mchana wa Saa saba, na taa kawasha.
Kikubwa nilicho-note ni kua gari hizi hua ni zile expensive. Yaani mtu huwezi kumkuta na ka Corrola Limited kake ka 4.5Mil akafanya hivyo, never.

Ni Ushamba??!!!
Shark kidogo nicheke kuhusu uzi wako lakini nikagundua una hoja. Ukweli kuhusu magari mengi yanayowasha taa mchana inaweza kuwa ni kwa sababu;
1.0 Magari hayo yapo hivyo, yaani mfumo wake ni kuwa ikiwasha na taa za parking zinawaka automatic, sasa magari mengi mfumo huo yakija Bongo hawautoi. Bado sijaelewa ni fashion au gharama kuutoa mfumo huo?????
2.0 Attention au alert kwa madereva kuwa makini na kuepuka ajali maana magari kama hayo ukigonga lazima Nairobi ikuhusu kabisa.

Mkuu Shark huo ndiyo mtazamo wangu kuhusu baadhi ya magari kuwasha taa mchana.
 
Last edited by a moderator:
Shark kidogo nicheke kuhusu uzi wako lakini nikagundua una hoja. Ukweli kuhusu magari mengi yanayowasha taa mchana inaweza kuwa ni kwa sababu;
1.0 Magari hayo yapo hivyo, yaani mfumo wake ni kuwa ikiwasha na taa za parking zinawaka automatic, sasa magari mengi mfumo huo yakija Bongo hawautoi. Bado sijaelewa ni fashion au gharama kuutoa mfumo huo?????
2.0 Attention au alert kwa madereva kuwa makini na kuepuka ajali maana magari

kama hayo ukigonga lazima Nairobi ikuhusu kabisa!

Mkuu Shark huo ndiyo mtazamo wangu kuhusu baadhi ya magari kuwasha taa mchana.

Hapo kwenye blue Mkubwa! Na hata unaweza ukakimbia kama gari lako ama toyo yako ndiyo hivyo!

Kazi kweli kweli!

Pamoja Mkubwa!!
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom