Kuendesha Gari huku Umewasha taa mchana, nini sababu??

Shark kidogo nicheke kuhusu uzi wako lakini nikagundua una hoja. Ukweli kuhusu magari mengi yanayowasha taa mchana inaweza kuwa ni kwa sababu;
1.0 Magari hayo yapo hivyo, yaani mfumo wake ni kuwa ikiwasha na taa za parking zinawaka automatic, sasa magari mengi mfumo huo yakija Bongo hawautoi. Bado sijaelewa ni fashion au gharama kuutoa mfumo huo?????
2.0 Attention au alert kwa madereva kuwa makini na kuepuka ajali maana magari kama hayo ukigonga lazima Nairobi ikuhusu kabisa.

Mkuu Shark huo ndiyo mtazamo wangu kuhusu baadhi ya magari kuwasha taa mchana.
sasa naanza kukupata Mkuu Mzee wa Rula kwamba ndivyo yalivyo, na nikihusianisha na ukweli kwamba ni magari "ya aina flani" hivi basi nakubaliana na wewe kua kwa Taa tu unaweza kuhitajika kwenda Nairobi
 
Hapo kwenye blue Mkubwa! Na hata unaweza ukakimbia kama gari lako ama toyo yako ndiyo hivyo!

Kazi kweli kweli!

Pamoja Mkubwa!!

Yeah,
Inaweza kua inalipa kuacha toyo ya Tshs 800,000 (Tshs 1,000,000 Less Depreciation Tsh 200,000) ukaingia mitini kuliko kujitosa mzima mzima kwenye deni la Tshs 3,000,000/= kwa ajili ya taa tu (bado kunyoosha, rangi, n.k).

Wacha yaendelee kuwaka tu hizo taa ili tuyaone vizuri barabarani na kujiepusha nayo tusije tukatafutiana kesi bure.
 
Kwenye nchi nyingine kuwasha taa mchana ni lazima. Ukiendesha kutoka Windhoek kuelekea na Walvis Bay unakumbana na vibao vingi vinavyokukumbusha kuwasha taa kwani njia hiyo ina sehemu nyingi amabzo ukungu mzito unaweza kutokea ghafla na ukakuzuia kuona mbele, na wanaokuja mbele yako kuona gari yako.
 
Ahsante kaka,
But mi nasemea hapa kwetu mtu yuko Posta mchana wa Saa saba, na taa kawasha.
Kikubwa nilicho-note ni kua gari hizi hua ni zile expensive. Yaani mtu huwezi kumkuta na ka Corrola Limited kake ka 4.5Mil akafanya hivyo, never.

Ni Ushamba??!!!

labda usharobaro.....
Anyway na mie kakorola kangu ntaaanza kukawasha taa mchana loh...........
 
1. kuna gari zinakuja ivo ivo kutoka kwa nchi husika sababu ya ukungu kama US na nchi zingine>
2. convoy eg. Msiba,harusi
3. identify eg. Embassy cars
4. Mbwembwe eg. BWM angel/eagle eyes or Chleysler nad VW >>>its nice to unique
 
Nafikiri hiyo ya tatu inahusu zaidi.
Ngoja kesho nami niwashe taa mchana kwenye
Mark ll -GR (Box) yangu!!
 
wakati mwingine hutokea iwapo uzimagari usiku wakati wa kupaki bila kuzima taa, asubuhi yake katika haraka za kuwahi kazina umewasha gari na taa lazima zitakuwa on kama ulivyoziacha kuzima jana yake, then baadae unashituliwa na dereva unaepishana nae kwa kukuwashia full au kushtuka kwa kuangalia dashboard
 
asante mleta mada hili nimejiuliza mda mrefu bila kupata jibu nafikiri wanaojua watatujuza zaidi
 
wakati mwingine hutokea iwapo uzimagari usiku wakati wa kupaki bila kuzima taa, asubuhi yake katika haraka za kuwahi kazina umewasha gari na taa lazima zitakuwa on kama ulivyoziacha kuzima jana yake, then baadae unashituliwa na dereva unaepishana nae kwa kukuwashia full au kushtuka kwa kuangalia dashboard

Mimi nlishamshtuaga dereva mmoja na akanijibu kua anajua kua taa zake zinawaka (hivyo nipotezee tu!!)

Na still HAKUZIMA!!
 
Ahsante kaka,
But mi nasemea hapa kwetu mtu yuko Posta mchana wa Saa saba, na taa kawasha.
Kikubwa nilicho-note ni kua gari hizi hua ni zile expensive. Yaani mtu huwezi kumkuta na ka Corrola Limited kake ka 4.5Mil akafanya hivyo, never.

Ni Ushamba??!!!

Ukweli ni kwamba, sheria za uendeshaji magari pamoja na kutofautiana kutoka nchi hadi nchi utaona sheria za nchi nyingi zinataka magari yawapo katika mwendo pole au kasi barabarani taa ziwe zinawaka inaponyesha mvua, kuna ukungu, usiku nk, pengine nchi nyingine muda wote uhakikishe head lights on all the time or whens raining or patch of fog, or what ever.

Kwa nchi za magharibi kama Ulaya na Marekani karibu sheria zao hazitofautiani sana ni mambo machache tu hukaziwa katika ukanda fulani na sehemu nyingine, nimeendesha gari nchi za Ulaya na Marekani karibu madai ni yale yale.

Jambo lingine na kutokana na sheria hizo magari mengi ya siku hizi karibu yote yametegeshewa muda wote head lights on, kama hutaki basi you can turn headlight off.

Mimi nina mazoea ya kuhakikisha naendesha gari likiwa head lights on muda wote kwa sababu naweza kujisahau katika yafuatayo:
  • Giza ikiingia naweza jisahau kuwasha taa za gari hasa kwenye barabara zenye taa za kuangaza barabara hasa mijini, porini giza ikiingia hutaona njia lazima uwashe.
  • Kusahau kuwasha taa za gari inaponyesha mvua, muhimu inaponyesha headlight must be on.
  • Kusahau kuwasha taa kunapokuwa na ukungu (fog). Kuna sehemu nyingine ukungu unafunga huwezi kuona hata gari ya tatu kutoka kwako kama mnaendesha mmefuatana.

Mengine napenda gari langu kuwa barabarani likiwa na headlights on kwa sababu ya kiusalama kwa sababu ni rahisi kuonekana toka mbali, kuna madereva wengine macho yao yana kiza.

NB: Niliwahi kusimamishwa barabara huko majuu wakati naendesha gari kwa kusahau to turn on headlight, polisi alinishauri niwe naendesha gari huku headlights on muda wote kukwepa usumbufu wa kusimamishwa na polisi, ingawa si kosa la kupigwa faini ila polisi anakuangalisha kwa maneno, lakini anakupotezea muda wako pengine zaidi hata ya dakika tano au kumi anapohakiki uhalali wa leseni ya udereva, bima, umiliki wa gari na hata kama ni mhamiaji uhalili wako wa kuwepo katika nchi husika.

Magari ya siku hisi hata hizo Camry na Corolla zina mfumo huo wa taa ambazo ni automatic. Unapozima gari na unatoa ufunguo kwenye ignition na kufungua mlango tu taa zinazimika.
 
Zinatumia umeme kidogo sana, mwanga mwangavu zaidi na zinadumu zaidi ya taa za kawaida. Ila bado ziko ghali kidogo. LED lights ni baada ya zile zilizokuwa zinaitwa CFL - compact fluorescent lights.
Bado bei zake ghali mpaka hivi sasa?
Nataka nibadili beam zangu, mwanga wake hafifu.
 
Baadhi ya magari hizo taa ni automatic,.
Na zingine zina'sense hali ya hewa/mwanga na zinajiwasha hasa haya magari ya bei mbaya
 
Mimi nilijisahau TU kuzima usiku... Mchana nikatembea Hivyo Hivyo nikakamatwa na traffic akaniambia nizime taa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom