Nini cha kufanya endapo joto la gari lako limepanda?

geranteeh

JF-Expert Member
May 21, 2015
266
618
Habari za weekend Wakuu, Madere na Wapenzi wa magari. Bila shaka leo ni siku nyingine ya kujifunza kitu ambacho pengine tumekutana nacho sana hasa sisi washinda barabarani. Kwa kawaida mfumo wa gari lako pale mbele kwenye engine ni moto tupu ndo maana utasikia hiki kimechoma hiki au kile kikichomwa kinasababisha hivi lakini hayo yote ntawaachia mechanics wenye elimu zao.

Mimi leo kama kawaida ntakupa elimu ya kukufanya uelewe kama mtumiaji wa gari na si kama fundi ndiyo maana tunashauri tatizo ukiona ni kubwa wasiliana na fundi wako kwa utaalamu na marekebisho zaidi. Turudi kwenye mada kabla sijaanza kukutoa ulimi ndugu yangu. Ni muhimu kuelewa hili somo kwani joto la engine yako ndilo linalokadiria maisha yake kwani endapo hutokuwa makini na joto la mashine itasababisha kuua engine yako ukaingia gharama ya kununua engine mpya. Kuna kanuni ya udereva ambayo watu wengi huwa hawaizingatii ambayo unatakiwa wakati unaendesha kila baada ya sekunde kadhaa uangalie dashboard yako kwani itakupa taarifa kama vile joto litapanda basi utaona kwenye mshale wa jotoridi au kwa gari za kisasa kuna taa ya joto huwaka sasa endapo utakua ni mtazama mbele basi hizi taarifa hutozipata na kupelekea gari yako kupata hitilafu zaidi au hata engine kufa kwani nina watu ninaowafaham zaid ya watano washawahi kuua engine zao kwa kuendesha gari huku joto likiwa juu. Trust me walinunua engine mpya na wengine miswaki.

NINI SABABU YA TAA YA TEMPERATURE KUWAKA AU MSHALE WA JOTO KUPANDA?

Kuna sababu nyingi sana ambazo zinaweza sababisha gari yako kupanda joto ila sababu kubwa ni kiwango cha maji kwenye rejeta yako kupungua au kuisha kabisa. Kazi kubwa ya rejeta yako ni kupoza engine ambapo maji hupelekwa kwenye engine kwa upozaji kisha kurudi kwenye rejeta yanapozwa then yanarudi kwenye engine na huu mzunguko huenda na kuenda mpaka utakapozima gari lako hivo basi pindi maji yanapokosekana kwenye rejeta automatically engine inakosa kitu cha kupozwa hivo joto hupanda na kusababisha matatizo zaidi.

Kuna mtu anaweza uliza kwanini maji ya kwenye rejeta inatokea yanaisha? Kuna sababu nyingi lakini kubwa ambayo hata namm nimei experience ni kupasuka kwa rejeta kiasi kupelekea kuvuja kwa maji na unapowasha gari ile pressure inakua kubwa hata mpasuko ukiwa mdogo tu basi maji yatatoka kwa wingi na solution yake ni kwenda kuziba kwa fundi rejeta.

Sababu ya pili inayopelekea maji kupotea ni kuziba kwa vinjia vya rejeta ambapo kumbuka niliandika kuhusu mzunguko wa kutoka kwenye engine kwenda kwenye rejeta na kurudi so huo mzunguko hufanyika kwenye vinjia vya rejeta hivo inapotokea vimeziba itapelekea maji kutozunguka na kutafuta pa kutokea mfano kwenye weak pipe, kimtungi cha reserve au kwenye kifuniko cha rejeta.

Sababu ya pili inayopelekea temperature kupanda ni kutofanya kazi kwa feni ya rejeta. Utajiuliza femi ya rejeta ndo nini? Kama ulikua makini kwa nliyoyaongea hapo juu utapata picha ya kuhusu ule mzunguko wa maji kutoka kwenye rejeta kwenda kwenye engine na kurudi je ulijiuliza kwenye rejeta hayo maji yanapozwa na nini kabla ya kurudi kwenye engine?

Kuna vitu viwili ambavyo vinapoza maji ya kwenye rejeta cha kwanza kabisa ni feni ambayo ipo mbele ya rejeta na cha pili ni upepo kutoka nje ya gari unaopitia kwenye show ya gari pale mbele. Ushawahi jiuliza kwanini gari pale mbele haizibwi lazima kila gari inakuwa na matundu matundu? Atleast leo ushapata jibu ndugu yangu. Sasa tukirudi kwenye mada endapo hii feni ikiwa haifanyi kazi inamaana maji ya kwenye rejeta hayatapozwa kumaanisha rejeta itarudisha maji yakiwa yamoto so engine haitapozwa na temperature itapanda.

Sababu nyingine ya temperature kupanda ntazitaja kwa ufupi na kwa umoja ambazo ni kama vile kifuniko kuharibika cha rejeta hivo kupitisha maji na mvuke kwa juu hivo kupelekea maji kupungua, pipe zinazopeleka maji kwenye engine kulegea ama kutoboka hivo kupelekea maji kupungua.

NINI CHA KUFANYA ENDAPO JOTO LA GARI LIMEPANDA?

A.. Kwanza unatakiwa kujua kwamba hutakiwi kuendesha gari yako endapo joto limepanda either kwa alama ya taa ya temperature au ule mshale kupanda hakikisha unatafta sehem unaegesha gari haraka sana. Baada ya kuegesha gari izime au kama hali ni mbaya sana gari za kisasa hujizima zenyewe.

Baada ya hapo shuka na ufungue bonet ya gari yako kwanza ili hewa iingie na gari ipate kupoa zaidi na usifungue au kugusa chochote. Acha gari yako kwa muda mpaka utakapojiridhisha imepoa estimation huwa ni nusu saa inatosha sana na kwa gari zakisasa hata uwashe vipi gari haitawaka endapo utajaribu kuwasha trust me so usijisumbue (hii ni ikiwa joto limepanda sana).

Baada ya hapo tafuta kitambaa au taulo na ukikosa hata nguo yako uitumie kufungulia mfuniko wa rejeta taratibu then angalia kiwango cha maji au coolant kilichopo endapo kimepungua kama kimepungua ongeza then washa gari ikiwezekana nenda garage ikaangaliwe.

B. Endapo utawasha gari yako na kukuta taa bado inawaka au ukaendesha kwa muda mshale ukapanda basi angalia feni ya rejeta kama inafanya kazi kama haifanyi kazi ni vema ukawasiliana na fundi wako aje kuirekebisha akiweza kuirekebisha ni jambo la kheri kwani kuna wakati inakua nia matatizo ya umeme waya haupeleki moto au fuse inakua na shida au kama itahitajika mpya unaweza ukatupatia rizqi nasi tukakuuzia kitu mang'anyu ila kumbuka haishauriwi kuendesha gari yako ikiwa joto liko juu hata mara moja kwani madhara yake madogo ni kuharibu silinda head gasket na makubwa ni kuua engine.....

Makala hii imeandikwa na Hamis Mgaya

IMG-20230619-WA0019.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shukran kwa uzi mzur mkuu ilinikuta week 2 zmepita nilianza safar bila kukagua gari( si kawaida yangu kuasafir bila kukagua gari ) nikatembea km 550 naona temp ipo juu gafla.. ila nashkru ilinitokea npo maeneo ya mjin basi nikalitatua vyema ilo tatzo
 
Kaka una bahati ilikutokea mjini mm ilinitokea kwenye kipori cha mbwewe saa mbili usiku yani mazingira yalikua kama saa nane usiku af niko pekeangu

Kwel nina bahat kaka maana nmetoka kusin uko nafika mbagala pale ndo naona changamoto nikashkuru npo mjin fundi uhakika ila pole snaa vp ss ulitatuaje changamoto iyo uck huu au ilibd ulale tu porin
 
Shukran kwa uzi mzur mkuu ilinikuta week 2 zmepita nilianza safar bila kukagua gari( si kawaida yangu kuasafir bila kukagua gari ) nikatembea km 550 naona temp ipo juu gafla.. ila nashkru ilinitokea npo maeneo ya mjin basi nikalitatua vyema ilo tatzo
Ulikosea Sana ndugu yangu, safari ndefu kama hiyo ulishindwa kuchek vitu vya msingi kama maji
 
Kwel nina bahat kaka maana nmetoka kusin uko nafika mbagala pale ndo naona changamoto nikashkuru npo mjin fundi uhakika ila pole snaa vp ss ulitatuaje changamoto iyo uck huu au ilibd ulale tu porin
Kaka temp ilipanda mara ya kwanza nkasimama ikapoa nkaongeza maji baada ya km moja gari ikachemsha tena nka park nkaongeza maji kwenda km moja tena gari inachemsha nkasema leo shughuli nnayo, nkaingia hotelin mbwewe nkatulia saa zima na nusu then nkaongeza maji yan natembea km moja mzigo huu hapa unavuja, nikazama uvunguni kagua sana nkakuta gari inatoa maji kwenye rejeta kwa chini nkasogea hivo hivo tia maji tia maji kama neno lenyewe hadi mandela pale nkanunua pakti mbili za majani ya chai nkajaza kwenye rejeta yote then ndo nkatia maji
Gari nilifika dar maji hayajapungua na nkaitumia siku tatu haikuchemsha tena. Siku ya tatu nikaenda kwa fundi akaifungua akaisafisha then akaiziba baada ya hapo gari ikakaa sawa yan bahati yang ni kwamba ilikua imepasuka kwa chini
 
Majani ya chai?
 
Vipi kuhusu kupaki gari bila kuzima na mshale wa temperature unapanda H ila ukiondoa mshale unarudi normal,hii inatokea nikipaki mlimani je ni tatizo au kawaida? geranteeh
 
Back
Top Bottom