Taa yoyote nyekundu kwenye dashboard ya gari yako siyo ya kuipuuza

JituMirabaMinne

JF-Expert Member
May 4, 2020
3,327
9,328
images (3).jpeg


images (2).jpeg

Asilimia kubwa ya magari huwa yanakuwa na warning lights(taa za tahadhari) za aina tatu. Aina hizi nitazitofautisha kulingana na rangi za hizo warning lights. Aina hizo ni kama ifuatavyo.

1. Kijani/Blue

2. Njano/Rangi ya machungwa

3. Nyekundu

Namba moja ipo tu kwa ajili ya kukupa taarifa. Mfano kama umewasha High beam, au upo kwenye ECO mode au taarifa yoyote ile. Hapa wewe endelea tu kufurahi kuendesha gari lako.

Namba mbili ipo kwa ajili ya kukupa warning na unaweza kuendelea kuendesha gari lako kama kawaida. Ila ni vizuri ukarekebisha tatizo linalopelekea taa ya tahadhari yenye rangi ya njano kuwaka maana kama utaliacha huenda taa nyekundu ikakuwakia. na mambo yakawa mabaya. Mifano ya taa ya njano ni taa inayoonesha gari kuishiwa mafuta, check engine light n.k.

Namba tatu hapo ndio hasa lilikuwa lengo la uzi huu. Kama ilivo katika maeneo mengine ambapo taa nyekundu huwaka kuashiria hatari. Hata kwenye magari taa nyekundu kwenye dashboard huwaka kuonesha ama tatizo kubwa kwenye gari lako au matatizo katika vifaa vya usalama kwenye gari yako. Au kwa kifupi tunaweza kusema taa nyekundu huonesha jambo ambalo linahitaji kuchukuliwa hatua haraka iwezekanavyo(immediate actions) kabla mambo hayajawa mabaya. Ukiona taa nyekundu imekuwakia kwenye dashboard siyo salama kabisa kuendesha gari lako tena hasa kama inablink.

Hapa chini nimejaribu kuelezea baadhi ya warning lights na nini huwa kinatokea kwenye gari lako zinapokuwa zimewaka.

1. Taa ya airbag

airbag-warning-light-300x300.png

Hii ni moja ya taa ambayo watu wengi huipuuza inapowaka lakini kiuhalisia unapoiona hiyo taa ni kama unakiona kifo chako. Taa hii humaanisha kwamba kuna tatizo kwenye mfumo wa Airbag wa gari lako. Na kulingana na hilo inaweza kupelekea airbag isifanye kazi kabisa wakati unapata ajali. Watu wengi huwakiwa na hii taa wanapobadili airbag clock spring ambayo ndio circuit ya honi na airbag ya pale kwenye usukani. Clock spring ikifungwa bila kutafuta centre ya rotation yake lazima ikatike ndani ya muda mfupi tu.

2. Taa ya ABS

abs-antilock-brake-system-300x300.png

ABS ni mfumo wa usalama ambao huyafanya matairi ya gari lako yasijilock wakati unapofunga brake. Taa hii inapowaka maana yake ni kwamba kuna shida katika mfumo wa ABS kwenye gari lako. Inapotokea shida yoyote katika mfumo wa ABS gari yako, control module itaamuru gari yako kuingia katika Non-ABS module Na hii inaweza kukusababishia ajali wakati unaendesha gari lako hasa wakati wa kufunga brake au matairi kujilock. Na ukashindwa kuendesha gari lako.

3. Taa ya engine oil pressure

oil-pressure-light-300x300.png

Taa hii huwaka ikiwa kuna presha ndogo kwenye njia za oil. Presha ndogo inaweza kusababishwa na kiasi kidogo cha oil, kuharibika kwa oil pump au kuziba kwa njia za oil. Hii inaweza kupelekea baadhi ya parts za gari yako kuyeyuka na kushikana pamoja na hivyo engine yako haitazunguka kabisa.

4. Taa ya coolant temperature

engine-temperature-light-300x300.png

Taa hii huonesha joto la coolant ni kubwa kuliko ni kubwa kuliko kawaida. Joto kubwa husababishwa na kiasi kidogo cha coolant, thermostat kustack, radiator fan kutozunguka n.k. ukiendelea kuendesha gari katika hali hii basi ujiandae kuikaanga engine yako.

5. Taa ya Seatbelt

seatbelt-reminder-light-300x300.png

Kama usipofunga mkanda kwenye gari yako basi taa hii huwaka tena ikiwa inablink. Kazi ya mkanda huwa ni kukufanya ubaki palepale kwenye seat ajali inapotokea. Hata kama gari yako ina airbag kama hujafunga mkanda ukipata ajali umekwisha kwa maana hiyo airbag haitokuwa na msaada wowote.

6. Taa ya battery

battery-light-300x300.png

Taa hii humaanisha kwamba battery yako haiingizi charge. Inaweza kusababishwa na lolote kwenye charging system ya gari yako. Anywhere kati ya battery na alternator.

Hizo ni baadhi tu ya taa za tahadhari. Ninachojaribu kueleza hapa ni umuhimu wa taa hizo. Kama umesoma basi unaweza kuona kwa hizo taa chache ambazo nimezielezea, kila moja kama haikusababishii majanga ya moja kwa moja basi tatizo itakalosababisha linaweza kukuingiza kwenye gharama kubwa, kukusababishia ajali au kukusababishia majeraha makubwa.
 
Juzi JUMAPILI jioni baada ya kuwasha gari iliwaka taa ya check engine baadae engine ilipopata joto zaidi Ile taa ilizima,Jana j3 nikaona Bora niende Kwa fundi wangu alihangaika mpaka pale alipokuja fundi umeme akagungua ni injection imekufa lkn kabla ya kubadilisha akaona Bora asafishe Kwanza nashukuru gari imetulia.

Sometimes Kwenye haya mambo ya Magari unaweza kubadilisha kitu cha gharama kubwa kumbe kinahitaji kusafishwa tu na gari inatulia
 
Juzi JUMAPILI jioni baada ya kuwasha gari iliwaka taa ya check engine baadae engine ilipopata joto zaidi Ile taa ilizima,Jana j3 nikaona Bora niende Kwa fundi wangu alihangaika mpaka pale alipokuja fundi umeme akagungua ni injection imekufa lkn kabla ya kubadilisha akaona Bora asafishe Kwanza nashukuru gari imetulia..

Sometimes Kwenye haya mambo ya Magari unaweza kubadilisha kitu cha gharama kubwa kumbe kinahitaji kusafishwa Tu na gari inatulia

Injection unamaanisha hii?
throttle-body-solo---clipped.png
 
Juzi JUMAPILI jioni baada ya kuwasha gari iliwaka taa ya check engine baadae engine ilipopata joto zaidi Ile taa ilizima,Jana j3 nikaona Bora niende Kwa fundi wangu alihangaika mpaka pale alipokuja fundi umeme akagungua ni injection imekufa lkn kabla ya kubadilisha akaona Bora asafishe Kwanza nashukuru gari imetulia..

Sometimes Kwenye haya mambo ya Magari unaweza kubadilisha kitu cha gharama kubwa kumbe kinahitaji kusafishwa Tu na gari inatulia
Nina tatizo kama hili, tatizo fundi wangu anapenda sana hela, hata kama tatizo dogo,naendelea kumute kwanza.. naendelea kudrive hivyo hivyo nikisaka hela, inaweza niletea shida mkuu?
 
Back
Top Bottom