Kuelekea Uchaguzi Mkuu: Rais Magufuli amecheza kama Messi

Jun 2, 2020
18
29
Salaam wanajamvi,

Itakumbukwa kwamba ujio wa COVID-19 umekuwa ni mtihani mkubwa kwa marais wa mataifa mbalimbali hususani yanayotegemewa kufanya uchaguzi mwaka huu na mwaka ujao. Corona imekuwa ni moja ya mitihani mikubwa mwaka huu.

Niende moja kwa moja nchini (Tanzania), Corona ilipoanza kulikuwa na mawili; ama kuweka watu lockdown au kuachwa tukiendelea na shughuli zetu. Hapa, kila upande mmoja wa shilingi ulikuwa na athari zake. Mosi, Ku-lock watu walie njaa na wakitoka wakulilie na kukuchukia mpaka uchaguzi au uwaache wakiendelea na shughuli zao halafu waathiriwe na ugonjwa upate vilio zaidi.

magufuli.jpg


Mzee "Messi" akaingia chimbo, akaamua kuchagua kichwa (no lockdown), watu tukahofu sana na kulaumu sana tukijua sasa chaja kifo kikuu. Ikagonga miezi idadi sawa au chini ya waliojiweka "jela".

Kubwa kuliko yote, ndugu zangu wapinzani wakaamua kujilock-down wenyewe. Messi akasema "Barca" hakuna kusepa. Siku 14 za wabunge wapinzani zikakata huku kukiwa hakuna hata mbunge mmoja aliyefariki (kati ya wale waliobaki). Sasa nadhani wapinzani wanaweza kujutia uamzi ule kwa sababu wenzao watakuwa wakijivunia KUJITOA KUFA KWA AJILI YA WANANCHI. Sijui jamaa zangu wao watajiteteaje kwa sababu lockdown yao haijaonekana kuwa na maslahi kwa wananchi wala wabunge.

Mara paap, Messi akaamua vyuo vifunguliwe. Sasa siku zimepita saba tulichokihofia hakijawa kikubwa kama tulivyokusudia.

Ninavyowajua wapiga kura wa Bongo, Magufuli kwao ni shujaa na mwerevu.... Kwa maneno mafupi kama liquid, Magufuli amemaliza kampeni kipindi hiki cha COVID-19.

Asanteni japo mimi mwenyewe sijui nimeandika nini.
 
Back
Top Bottom