Kuelekea 2015, tuna kundi jipya la urais CCM - Kigwangalla

hakuna msafi anaweza kutokea ccm kwa mfumo wa chama chenyewe na mfumo mbovuwa serikali legelege.afadhari hata kipindi cha mkapa rais alikuwa na mvuto hata na madudu aliyoyafanya mwishoni.Lakini kwa sasa rais hana heshima inaonekana hana mcheza show anaweza kuongoza nchi hii inatokana na rais aliye madarakani kuwa anafanya mizaha mingi kwenye mambo ya msingi kwa kifupi ni rais goigoi anayeongoza serikali dhaifu anyesindikiza chama cha walarushwa na mafisadi urais sasa ni kama kuwa celebrity tu na hili tz tutalijutia kwa karne yote ijayo.

Ndugu,
You have said it all.
Ila kinachonishangaza ni kuwa hawa jamaa wa "kijana" hawaoni wa hawataki kusikia!!!
Hivi ni wao ndo wana matatizo au sisi wakosoaji ndo tuna matatizo???
 
Ndugu,
You have said it all.
Ila kinachonishangaza ni kuwa hawa jamaa wa "kijana" hawaoni wa hawataki kusikia!!!
Hivi ni wao ndo wana matatizo au sisi wakosoaji ndo tuna matatizo???

Ungewataja kwa majina ingesaidia ili kama wapo humu waweze kuelezea their position on the matter ili wapimane na wadau wengine kwa hoja. Usisahu at JF we Dare to Speak Openly. Let's keep this spirit alive.
 
Watu wanaopitishwa kugombea Urais uwa ni bidhaa ya makundi yenye maslahi yao (yoyote yale) Hapa najiuliza demokrasia inafanyaje kazi hapa ikiwa Wananchi tunasukumiwa watakacho kikundi cha watu halafu tunawekwa as if we have any choice....Mfumo wa vyama katika kuwapata wagombea Urais umejaa ukiritimba, ni wakati tudai mabadiliko katika vyama vyetu ili Mgombea apatikane kwa matakwa ya wanachama kwa ujumla na sio kikundi cha watu......Tanzania hatuchagui Rais, tunachaguliwa tena kwa viini macho
Maswali yapi hayo?
 
Mheshimiwa HKigwangalla,

Pole na shughuli za ujenzi wa taifa. Kwanza naomba ku declare interest kwamba mimi ni mwanachama (hai) wa CCM ambae nipo huku site. Hoja yako has stimulated akili yangu (kikada zaidi), as you have set a Premise that requires justification before conclusion i.e. you have to provide an adequate ground for it, hivyo nina maswali matano kama ifuatavyo :

1. Swali la Kwanza, ningependa kujua unazungumza kwa mamlaka ipi ili sisi wanachama wenzako tuweze kukuelewa zaidi both in content and context:
· Je, ni mjumbe wa mkutano mkuu wa taifa ambao utatusaidia kupata jina la mgombea? NDIYO MIMI NI MJUME HALALI WA KIKAO HIKI. HATA HIVYO SI LAZIMA UWE MJUMBE ILI KUSHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA KUTOA MCHANGO WAKO WA NANI ALIONGOZE TAIFA LETU!
· Je ni mjumbe wa kamati kuu ambae utakuwa mmoja wa wahusika katika kutubakishia majina ya wenye sifa yasiyozidi matano? HAPANA KWA SASA, ILA NATARAJIA KUGOMBEA KITI CHA WAZAZI TAIFA NA HIVYO NIKISHINDA NITAKUWA. HATA HIVYO ....KAMA HAPO JUU!
· Je ni mjumbe wa CCM-NEC ambae utakuwa mmoja wa wahusika watakaotubakishia majina matatu yatakayopelekwa kwenye mkutano wa taifa? HAPANA KWA SASA. ILA NATARAJIA KUGOMBEA NEC NA HIVYO KUWA MJUMBE KAMA NITASHINDA. HATA HIVYO...KAMA HAPO JUU!

Kama ni none of the above, kuwa mwangalifu kwani inaweza kutoa tafsiri kwamba yote hoja yako imejaa self – interest au ya kundi fulani au self – seeking kwani tumeshuhudia mara nyingi nyakati kama hizi viongozi wengi wa CCM huwa mstari wa mbele kupigia debe majina fulani fulani only to find out later kwamba kumbe sio kwa maslahi ya chama au taifa bali expectations za kuwa mawaziri au manaibu waziri iwapo mgombea wao atapita (rejea constructs and dynamics za mtandao). Naomba uelewe kwamba I am not accusing you katika hili bali ni angalizo tu to avoid wingu la namna hii lisitande juu yako. NAKUSHUKURU, ADVICE TAKEN. LAKINI NAKUHAKIKISHIA KUWA SINA INTEREST YA KUNDI LOLOTE (de facto) KATI YA UNAYOYAFAHAMU, ILA HILI, NA KWAMBA KUNDI LETU LIMEJENGWA KATIKA MISINGI KWAMBA HATUFUNGAMANI NA MTANDAO WOWOTE ULE ULIOPO KWA SASA. NA PIA NAPENDA KUKUFAHAMISHA KUWA SIJAWAHI KUJIPANGA KUWA WAZIRI MAANA NAJUA HII NAFASI YA KUTEULIWA NA HUJUI MAMLAKA YA UTEUZI INA VIGEZO VIPI, HIVYO HUWA SIKOSI USINGIZI NIKIUWAZA UWAZIRI, JAPOKUWA NAJUWA KUWA NIKIPEWA FURSA HIYO NITAWASHANGAZA WATU...WENGI WATAJIULIZA HUYU ALIKUWA WAPI? kWA NINI TUMECHELEWA KUMPA KAZI HII? NA ISITOSHE SIWAZII SANA UNAFSI WANGU BALI NASHIRIKI KWENYE HARAKATI HIZI KWA FAIDA YA NCHI NA CHAMA CHANGU.

2. Swali la Pili, katika mchakato huo wa kutupatia mgombea mzuri 2015, je wewe na wenzake mnatilia maanani kwa kiasi gani barua ya Mh. Joseph Butiku aliyomwandikia Mwenyekiti wa CCM (wa wakati ule) kuhusu jinsi gani utaratibu ulikiukwa katika kumpata mgombea? Nadhani kama uliisoma barua ile, suala hili limekitia CCM doa kubwa sana. Lakini sio kwa uchaguzi wa 2015 tu bali pia tuna matatizo katika ngazi ya uchaguzi wa NEC (rejea kitabu cha Pro Mwandosya). Mheshimiwa HKigwangalla, mnatuhakikishia vipi sisi wanachama kwamba 2015 Kiti hakitarudia makosa aliyoainisha Mh Butiku? Ni muhimu ukafahamu kwamba mwisho wa siku, ili mgombea wetu awe na nguvu mbele ya umma, ni lazima apate ushirikiano wa wazee wetu wa CCM – kina butiku, kitine, Kaduma, Warioba n.k. Kukana hili ni kukataa ukweli. Vinginevyo, wazee wengi wazalendo misimamo yao haipishani sana na yale yaliyopo kwenye barua ya butiku, hivyo ili kupata ushirikiano wao, utekelezaji wa masuala yaliyoainishwa ndani ya barua ile ambayo kwa kweli mengi ni objective and for the party’s interest, lazima yashughulikiwe. Isitoshe, wazee hawa hawatagombea, wameshaweka wazi. BARUA YA MZEE BUTIKU NIMEISOMA KARIBU MARA TATU SASA NA ZAIDI NAFAHAMU MTAZAMO NA MACHUNGU YAKE. NAMPA POLE. BINAFSI NAMUAMINI SANA MWENYEKITI WETU KWA SASA NA NINAAMINI UAMUZI ATAKAOUFANYA UTAKUWA NA MASLAHI YA CHAMA NA YA TAIFA MBELE, KULIKO YA KUNDI, KAMA AMBAVYO AMEWAHI KUDHIHIRISHA KTK MAAMUZI MBALIMBALI HUKO NYUMA. TOFAUTI ZETU NA HISTORIA YETU YA KUPASUKA ITAKUWA SABABU KUBWA YA KUHAKIKISHA TUNAKUWA WAMOJA HUKO TUENDAKO!

3. Swali la Tatu, Unaposema mtatutafutia mgombea mpya, sisi wana CCM hatutaki mgombea mpya mwenye mawazo yale yale, tunataka mgombea mpya mwenye mawazo mpya, au mgombea aliyekwisha onyesha dalili za kugombea lakini ana mawazo mapya. Bottom line hapa ni MAWAZO MAPYA, SIO MTU MPYA!!!.

OFCOURSE MTU MPYA MWENYE MAWAZO MAPYA SHOULD BE THE ANSWER! HILO SIYO TATIZO NA NDIYO MAANA NIMESEMA KWAMBA KAMATI YETU NI 'EXPLORATORY'. TUNAKUKARIBISHA KWENYE TEAM, KAMA UKO TAYARI, MAANA BADO TUNA-RECRUIT!

Naomba nikunukuu:

“…We are aiming at having a 'New Man' (Mtu Mpya!) ili iwe rahisi kumjenga na kumuuza kwa wananchi”

Nadhani wananchi watatununua sio tu mtu mpya, lakini muhimu zaidi, mawazo yake katika kuwaletea mabadiliko in their livelihoods struggles.

Vile vile sisi kama Chama, ni muhimu tukatilia maanani hoja ya Kobello pale anaposema kwamba (namnukuu):

“Asiwe mfanyabiashara (businessman), asiwe na biashara yeyote ile, asiwe na nyumba ya kupangisha, asiwe mlevi na definately awe mkulima au mfanyakazi (jembe na nyundo, hatuna fremu kwenye bendera yetu). Kama hampendi hili, ni vyema mkaanzisha chama chenu.” HILI LA KOBELLO SIYO LA MSINGI SANA, MUHIMU NI AWE MUADILIFU NA TUWE NA MFUMO MZURI WA KUMUWAJIISHA NA PIA KUMREKEBISHA NA KUMZUIA ASIFANYE MAAMUZI MABAYA KWA KUHAKIKISHA TUNAMSHAURI (BUNGE) KWA KILA UAMUZI MKUBWA..!

4. Swali la Nne, tunapoelekea uchaguzi wa wa ndani wa CCM na ule mkuu 2015, wewe kama mmoja wa viongozi wetu wa chama, ni lazima tukuambie kwamba sisi huku site tunazidi kuishia nyenzo za kushindana kihoja na wapinzani wetu. Kwa mfano, CCM tutasimamia itikadi ipi? Tunaelekea 2015 kwenye uchaguzi mkuu tukisimamia itikadi gani dhidi ya itikadi za wapinzani wetu? Natumaini utakuwa na majibu ya hapo kwa hapo kwani huku hali ni ngumu, tunakimbia vijiwe kutokana hili. Sitegemei jibu liashirie kwamba hatua itikadi ya vitendo bali ya nadharia; au hatuna itikadi inayoeleweka; au suala la itikadi kwa sasa halina umuhimu; au suala la itikadi tunalifanyia kazi; au itikadi yetu ni ya Ujamaa na kujitegemea; Jibu lolote kati ya haya litatufanya sio tu tukimbie vijiwe huku site, bali kuvihama kabisa kwani itazidi kujidhihirisha kwamba kumbe ni kweli chama chetu cha CCM hakina dira wala mwelekeo na badala yake kinashindana kupitia election manifestos zilizojaa ombwe la itikadi. ITIKADI YETU HAIJABADILIKA RASMI, BADO NI UJAMAA NA KUJITEGEMEA JAPOKUWA KUMEKUWA NA MUINGILIANO AMBAO UNAASHIRIA SOME DEVIATIONS FROM THE CORE, NAAMINI BADO TUKO IMARA KWENYE ITIKADI YETU SEMA TUMEINGIZA ELEMENTS ZA UBEPARI KWENYE MFUMO NA HIVYO KUATHIRI POSITION YETU YA AWALI. HUU MFUMO WA SASA NI NEO-UJAMAA NA KUJITEGEMEA NA UNAHITAJI REFORMS ZINAZOENDANA NA HALI YA SASA.

5. Na mwisho – hivi kweli Mheshimiwa HKigwangalla, katika majina yanayotajwa tajwa huko mitaani kweli CCM hatuna hata mtu mmoja ambae kwa dhati kabisa (tukiweka self interest pembeni), tunaona anaweza kutufaa? Ni dhahiri kwamba majina kama Magufuli na Mwandosya, hata wapinzani na pia political independents wakiyasikia wanayakubali sana (hata kama sio in public). Mimi nadhani tuanze kubadilika na kuachana na utamaduni wa viongozi wetu kujifungia kwenye vikao, kulipana posho na kutujia na jina kwamba – HUYU NDIYO CHAGUO LETU NA ANATUFAA. Kama kuna wana CCM ambao pamoja na kuwa wanatajwa huko mitaani kwa muda mrefu lakini bado hawajachafuka, tujaribu kuwapa nafasi. Ni kweli kwamba bado ni mapema sana na wapo watakaojitokeza wengi na pengine tukapata mmoja anaetufaa kutoka miongoni mwao, lakini ni muhimu huyo mgombea wenu muanze kufanye utaratibu wa kumweka hadharani kwani chema chajiuza, kibaya chajitembeza na kama hatakuwa na madudu yoyote, atang’ara kama Mwandosya na magufuli ambao kwa miaka mitano sasa majina yao yanatajwa na bado yanazidi kupaa in a non – partisan context. Nasisitiza kwamba ni kweli ni mapema mno, lakini nashauri msichelewe sana. TUTAKAPOKAMILISHA EXPLORATION YETU TUTAANZA MIKAKATI YA KUMUWEKA WAZI TUNAYEMUUNGA MKONO NA HAPO UTAJUA SASA 'NGOMA INOGILE', HATA HIVYO SI LAZIMA AWE MIONGONI MWA HAO WANAOTAJWA TAJWA...NA NI MAPEMA MNO KUTABIRI!

Asante.

Nashukuru nimeyaona maswali yako na samahani kwa kuchelewa kuyajibu. Angalia majibu ya kila swali lako kwenye capitals zenye rangi ya blue mbele ya swali husika! I hope utayaona na kufuatilia vizuri
 
Kwa vyovyote sitaki rais ajaye atoke CCM tena hata kama atkuwa mtu mzuri sana na uwezo mkubwa wa kuongoza. Tunahitaji kuvunja hili zunguko la imani ya chama kimoja kwanza. Itasadia taasisi nyeti kam polisi, mahakama na jeshi la ulinzi kutambua tofauti ya CCM na serikali.

Sijui migogoro ndani ya CHADEMA inachochewa na nani, lakini mara zote imekuwa inahusu aspiration ya mtu mmoja na madaraka. Sijawahi kusikia migogoro inayotakana na uhalifu wa mwanachama fulani ndani ya chama hicho. Migogoro hiyo ya kisisasa tunaweza kuishi nayo kuliko rushwa na wizi.
yaya umenifurahisha sana na post yako kuhusu "mwandishi mahiri"; it was the best.
 
Last edited by a moderator:
Nashukuru nimeyaona maswali yako na samahani kwa kuchelewa kuyajibu. Angalia majibu ya kila swali lako kwenye capitals zenye rangi ya blue mbele ya swali husika! I hope utayaona na kufuatilia vizuri

Nimefurahi jinsi ulivyo muwazi, ingawa mimi siungi mkono chama chako.

We need to do something to stop CCM from getting to the State House again; they have failed us over the years. We can't expect different results by doing the same things again and again.
 
Nashukuru nimeyaona maswali yako na samahani kwa kuchelewa kuyajibu. Angalia majibu ya kila swali lako kwenye capitals zenye rangi ya blue mbele ya swali husika! I hope utayaona na kufuatilia vizuri

Nashukuru kwa majibu yako Mheshimiwa. Nimetosheka na majibu yako kwani yamejitosheleza. Ni matumaini yangu kwamba mtafanya kila linalowezekana kuokoa nchi yetu (sio koukoa CCM) kwani wokozi wa CCM ni secondary but if CCM ikiwa part of that process, itakuwa jambo la kheri kwetu sisi vijana ambao bado tuna matumaini na ccm licha ya chama chetu kukosa mwelekeo kwa muda sasa, lakini wengi wetu hatujali sana kama CCM itapoteza uongozi wa nchi ikiwa mbadala wake utakuwa namanufaa kwa vijana wa nchi yetu/taifa kwa ujumla.
 
Nashukuru nimeyaona
maswali yako na samahani kwa kuchelewa kuyajibu. Angalia majibu ya kila
swali lako kwenye capitals zenye rangi ya blue mbele ya swali husika! I
hope utayaona na kufuatilia vizuri

i hope mtu wenu ni mzuri kama mawazo yenu.
 
Nimefurahi jinsi ulivyo muwazi, ingawa mimi siungi mkono chama chako.

We need to do something to stop CCM from getting to the State House again; they have failed us over the years. We can't expect different results by doing the same things again and again.
On the contract, we are working hard to ring the necessary reforms in the party so that when we win election in 2015 we are all new and ready to lead the nation to a promised land...mind you we would have a new constitution, and if we put in place a good team, we definitely would take us to a whole another level!
 
Mchambuzi, ni kitu kigumu kusema viongozi wetu wasiamue mustakabali wa Taifa, nani sasa ataamua? Ni lazima katika hatua za kumpata mgombea wetu tufike mahali viongozi wapendekeze a number of people eligible for the high office na hapo wataruhusu sasa demokrasia ya ndani ya chama ichague na baadaye demokrasia ya ndani ya nchi iamue ...

Dr. HKigwangalla "natoka nje ya mada kidogo" kuna swali huwa najiuliza na natamani nipate jibu jepesi ..! kwanini umeamua kusaliti fani ya udactari na kuingia kwenye siasa...? hudhani kwamba kama kutumikia wananchi ungewatumikia vizuri ukiwa hospitalini..?!
 
No country for old men Mimi naona hii imekaa vizuri zaidi.Kijana yeyote atakaye simama kura yangu inamuhusu
 
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO CHADEMA KATA YA USA-RIVER KINAPENDA KUWATANGAZIA WANANCHI WOTE WA USA RIVER NA VITONGOJI VYAKE NA MAENEO YOTE YA JIRANI KUWA KUTAKUWA NA MKUTANO WA HADHARA SIKU YA JUMAMOSI TAREHE .11-08-2012 KATIKA KIWANJA CHA SOKONI MAGADIRISHO KUANZIA SAA SABA KAMILI MCHANA.WAGENI RASMI NI VIONGOZI WA TAIFA CHADEMA,WILAYA,KATA NA TAWI,KARIBUNI WANANCHI WOTE TUENDELEZE KAULI MBIU YETU YA “VUA GAMBA VAA GWANDA” SAMBAMBA NA (M4C)NA WALE WOTE WANAO TAKA KURUDISHA KADI SIKU HIYO TUNAWAKARIBISHA.TAFADHARI FIKA BILA YA KUKOSA.
-Chanzo ni kuhusiana na aliyekuwa mwenyekiti wa tawi la magadirisho Ndugu NURU MAEDA kudanganywa kwa kuku mmoja mtetea na mayai mawili na kurudu ccm.
 
Dr. HKigwangalla "natoka nje ya mada kidogo" kuna swali huwa najiuliza na natamani nipate jibu jepesi ..! kwanini umeamua kusaliti fani ya udactari na kuingia kwenye siasa...? hudhani kwamba kama kutumikia wananchi ungewatumikia vizuri ukiwa hospitalini..?!
Udaktari una basic roles 3; curative, preventive na promotive. ukiamua kuzigawa proportionately kwa uzito ule ule, utagundua kuwa curative ni 33% only. the rest you could do a lot by influencing the social determinants of health, and you could do that much better by influencing decision making related to health at national level when you are in the parliament! Maamuzi ya kuchagua uwe bingwa kwenye nini ni ya mtu binafsi, na mimi niliamua siku nyingi kuwa nita-specialize kwenye fani ambayo itakuwa inaleta impact kwa watu wengi zaidi kuliko ile inayomgusa mtu mmoja mmoja, na ndiyo sasa nafanya Ph.D. kwenye public health nikijikita zaidi kwenye health economics, na malengo yangu ni kufanya tafiti mbalimbali za mifumo ya afya na jinsi ya kuhakikisha huduma sawa zinapatikana kwa kila mtu! cf. the theory of justice by John Rawls na pia soma Amartya Sen (people's capability to function), Norman Daniels and James Sabin (Just health care, accountability for reasonableness), Sudhir Anand etc Ukiyaelewa haya yote utajuwa ni kwa nini I am who I am, na ni kwa nini nafanya ninayoyasimamia kwenye siasa! Its about morality na social justice inclination ndani yangu, sina kingine...na practically na-enjoy kufanya ninachokifanya
 
No country for old men Mimi naona hii imekaa vizuri zaidi.Kijana yeyote atakaye simama kura yangu inamuhusu
Usipoteze kura yako kwa kutumia kigezo kimoja tu. chagua na pigania kama ni kijana basi awe muadilifu
 
On the contract, we are working hard to ring the necessary reforms in the party so that when we win election in 2015 we are all new and ready to lead the nation to a promised land...mind you we would have a new constitution, and if we put in place a good team, we definitely would take us to a whole another level!
sorry I meant to write, on the 'contrary'
 
Udaktari una basic roles 3; curative, preventive na promotive. ukiamua kuzigawa proportionately kwa uzito ule ule, utagundua kuwa curative ni 33% only. the rest you could do a lot by influencing the social determinants of health, and you could do that much better by influencing decision making related to health at national level when you are in the parliament! Maamuzi ya kuchagua uwe bingwa kwenye nini ni ya mtu binafsi, na mimi niliamua siku nyingi kuwa nita-specialize kwenye fani ambayo itakuwa inaleta impact kwa watu wengi zaidi kuliko ile inayomgusa mtu mmoja mmoja, na ndiyo sasa nafanya Ph.D. kwenye public health nikijikita zaidi kwenye health economics, na malengo yangu ni kufanya tafiti mbalimbali za mifumo ya afya na jinsi ya kuhakikisha huduma sawa zinapatikana kwa kila mtu! cf. the theory of justice by John Rawls na pia soma Amartya Sen (people's capability to function), Norman Daniels and James Sabin (Just health care, accountability for reasonableness), Sudhir Anand etc Ukiyaelewa haya yote utajuwa ni kwa nini I am who I am, na ni kwa nini nafanya ninayoyasimamia kwenye siasa! Its about morality na social justice inclination ndani yangu, sina kingine...na practically na-enjoy kufanya ninachokifanya

umesomeka Dr.
 
Vita iko nje nje hapa bila kutandikana CCM na Serikali yake haitashika adabu. Uwizi imekuwa ni halali yao na ukiwakataza wao wanaona anayewakataza yuko wrong. Kigwangala mwenyewe yuko hukohuko kwenye ujambazi, kama ubunge angekuwa halipwi na hakuna marupurupu yaani ubunge ingekuwa kazi ya kujitolea Kingwangwala angeacha fani yake ya udaktari na akawa mbunge?

Tusidanganyane hapa, utawala wa kiafrika ni wa kung'ang'ania madaraka kwa sababu ya uwizi/ujambazi/unyang'anyi.

Vita lazima, walionacho(waizi/wanyonyaji) vs wasiokuwanacho(wanyonywaji/walalahoi) hamtaki kuachia madaraka kwa kwa njia ya amani
 
Vita iko nje nje hapa bila kutandikana CCM na Serikali yake haitashika adabu. Uwizi imekuwa ni halali yao na ukiwakataza wao wanaona anayewakataza yuko wrong. Kigwangala mwenyewe yuko hukohuko kwenye ujambazi, kama ubunge angekuwa halipwi na hakuna marupurupu yaani ubunge ingekuwa kazi ya kujitolea Kingwangwala angeacha fani yake ya udaktari na akawa mbunge?

Tusidanganyane hapa, utawala wa kiafrika ni wa kung'ang'ania madaraka kwa sababu ya uwizi/ujambazi/unyang'anyi.

Vita lazima, walionacho(waizi/wanyonyaji) vs wasiokuwanacho(wanyonywaji/walalahoi) hamtaki kuachia madaraka kwa kwa njia ya amani.
Kodi yote inayokusanywa ni kwa ajili yenu nyie viongozi mnunue magari ya kifahari, manyumba ya kifahari, viwanja, mishahara minono, marupurupu kibao kwa kodi tunazowalipia nyie viongozi ili mneemeke na sisi tuishie kwenye maisha duni milele, wapi na wapi si bora nife kwa sababu tayari natakiwa nife sina cha kupoteza.
 
Back
Top Bottom