Kuelekea 2015, tuna kundi jipya la urais CCM - Kigwangalla | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuelekea 2015, tuna kundi jipya la urais CCM - Kigwangalla

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mohamedi Mtoi, Jul 31, 2012.

 1. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #1
  Jul 31, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Vita ya makundi yenye nguvu hata kukimega chama kwa nyufa tunayo ishuhudia ndani ya CCM ilijionyesha dhahiri tangu mwaka 2005. Vita hiyo bado inaendelea na naamini haita kwisha hadi ccm itakapo ng'oka madarakani.

  Lipo kundi jipya linalojiita lenye ushawishi mkubwa ndani ya CCM linalo jipanga kwa kinyang'anyiro cha 2015. Haya yamebainishwa kwenye mjadala mmoja Mh Kingwangallah akimjibu Kamanda Tumaini Makene alisema "Kwenye mbio za Urais 2015 ndani ya Chama tumeanzisha kundi letu jipya kabisa na lina majembe ya ukweli na yote hayo hayategemei nguvu ama ushawishi wa hao wanaohangaika na Urais leo unaowajua...na sisi tuna uhakika kwamba kati ya wote hao hakuna atakayekuwa Rais miongoni mwao...

  Sisi tuna malengo ya kutafuta Rais safi na tutamsimamia kwa uwezo wake, kwa sifa zake na tutampitisha! Kundi letu ni kubwa na lina ushawishi mkubwa na tunaelewana vizuri, tuko vizuri na tunajipanga kwa siri kubwa!"

  Majibu haya ni baada ya Kigwangwallah kuambiwa anajitafutia umaarufu kupitia makundi kadhaa ndani ya CCM ambayo tayari yameshaanza kunyukana kutoka na michango yake bungeni kutengeneza urari kwa kundi la Mh. Lowassa na Mh. Sitta.
   
 2. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #2
  Jul 31, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Huyu Kigwangwallah kula za maoni za Ubunge tu zimemshinda, halafu anazungumzia ushawishi wa nafasi ya Urais!
   
 3. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #3
  Jul 31, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Kingwangallah alibebwa kwenye ubunge leo atatuambia nini tumsikilize !.
   
 4. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #4
  Jul 31, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Nimemuona leo akichangia kwa bajeti ya wizara ya afya, alifokewa na bibi kiroboto kama mtoto mdogo pale alipotaja tu jina "dr. Ulimboka" akanywea, akatia huruma!!! kigwangwalah huna haiba hiyo unayodhani kuwa nayo kwenye jamii ya watanzania, unachojua ni siri za mizengwe ya ccm, kamwe usijidanganye "kuunda kundi"
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. J

  JokaKuu Platinum Member

  #5
  Jul 31, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,729
  Likes Received: 4,948
  Trophy Points: 280
  ..hamjaona Maprofesa na madokta wanaozunguka na Nape ktk mikoa mbalimbali.

  ..wapo Dr.Magufuli, Prof.Maghembe, Prof.Tibaijuka, na Dr.Mwakyembe.

  ..nadhani karibuni ataongezeka Prof.Muhongo.
   
 6. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #6
  Jul 31, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,286
  Likes Received: 597
  Trophy Points: 280
  Sidhani kuwa kuna atakayepenya kwenye NEC na mkutano mkuu wao kati ya hao. CCM ina wenyewe.
   
 7. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #7
  Jul 31, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Kwa faida ya mjadala huu naomba kumnukuu muandishi nguli na mhariri mahiri wa The Guardian kaka Richard Mghamba.
  Kwenye mjadala husika nae amesema

  "HK na wengine,
  Chadema kwa sasa in a makundi ya hatari kuliko hata ya CCM tena ambayo
  yanajengwa kwa misingi ya ukanda na hata ukabila. Kila anayetaka kugombea
  nafasi ya juu katika chama, utasikia mizengwe ya
  hatari inaibuliwa wakati nilitaraji chama kama
  Chadema—kiruhusu
  demokrasia itawale na yule anayekubalika—anaibuka mshindi.

  Mfano wote tunafahamu Dr
  Slaa anakubalika sehemu kubwa ya Tanzania lakini
  kama Zitto Kabwe
  anaamua naye kugombea,
  acha atengeneze CV yake na chama hakina budi kuruhusu wagombea
  kujitokeza kama ilivyo ndani ya Republican,
  ambacho ni chama rafiki kwa Chadema.
  Marehemu Chacha Wangwe alipoamua kutangaza kugombea uenyekiti wa
  Chama, seke seke
  iliyompata kabla hajafa wote tunafahamu. Ni
  lazima tufike mahali kama tuna sema CCM kuna rushwa na makundi, then
  Chama mbadala kiwe
  smart, lakini kama na
  chenyewe hata kabla ya kushika dola tayari kuna fujo, then kimeshajichimbia
  kaburi".
   
 8. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #8
  Jul 31, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Makundi, makundi, makundi... ndiyo yametufikisha hapa tulipo. Hivi bado hawatuhurmii tu? Haya makundi yaliyopo hayatoshi mpaka waanza kuanzisha mengine mapya? Imefika wakati sasa hii nchi tugawane kila mtu afe na chake
   
 9. B

  Bubona JF-Expert Member

  #9
  Jul 31, 2012
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kuibuka kwa kundi jingine ndani ya CCM ni faida kwa ukombozi wa Taifa letu!
   
 10. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #10
  Jul 31, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,143
  Likes Received: 2,465
  Trophy Points: 280
  hili si kundi bali ni ki sub-group kwenye kundi lingine kubwa ndani ya ccm
   
 11. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #11
  Jul 31, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,093
  Likes Received: 1,477
  Trophy Points: 280
  inawezekana lisiwe kundi jipya ila tu ni wajanja wenye makundi ambayo yanafahamika wanaamua kutengeneza kundi jingine ili kupoteza malengo kumbuka mchezo uliochezwa kwenye uchaguzi wa spika hicho ndicho kitakachokuwepo
   
 12. S

  SURUMA JF-Expert Member

  #12
  Jul 31, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Sasa huyu Nape ndiyo DALALI wao kwamba anawanadi kimyakimya (kabla ya muda) au???
   
 13. y

  yaya JF-Expert Member

  #13
  Jul 31, 2012
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu, pamoja na kumpa sifa ya "muandishi nguli na mhariri mahiri wa The Guardian kaka Richard Mghamba", binafsi sijaona kudhihirisha u-nguli wake katika comments hizi.

  Kama ni ukanda na ukabila, Dr Slaa ni mpweke sana katika CDM, lakini aliombwa na kupitishwa kugombea urais wa TZ mwaka 2010. Hapo ukabila na ukanda uko wapi?

  Ninachokiona katika CDM ni kwamba hilo ambalo wengine wanaliita zengwe ili fulani asigombee cheo fulani ni kama ambalo TZ inaugua mpaka sasa kutokana na maamuzi ya wapigakura ya tangu uchaguzi wa 2015 na ule wa 2010, ugonjwa unaoitwa "Popularity".

  Watu wanapima uongozi kwa popularity ya mtu na si kwa uwezo wa kuongoza. Ni kweli Mhe. marehemu Wangwe was popular in CDM like wise Hon. Zitto. But the question is was he (Wangwe) and is he (Zitto), really capable of being a top leader of his party and his country?

  Kwa sababu kusema ni tofauti na kutenda.
   
 14. ha ha ha

  ha ha ha JF-Expert Member

  #14
  Jul 31, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 641
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kila mwenye hoja hafifu kuhusu cdm anataja 'demokrasia ya ndani ya chama'.kwani nini maana ya demokrasia?ni change political figure au ni achievement of common goal through any of the group members presiding? Nadhani malengo,kazi za kichama na mengine mengi yanafanikiwa vizur chini ya hao waliopo,ni kweli ni vzuri kubadili uongozi baada ya muda fulani lakini si swala la lazima kiasi hiki. Au kuna mamluki?
   
 15. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #15
  Jul 31, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  yaya,
  Kungekuwepo kitufe cha thanks, ningekuwekea mara mia.
   
 16. y

  yaya JF-Expert Member

  #16
  Jul 31, 2012
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nami nasema, asante Mkuu.
   
 17. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #17
  Jul 31, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Hoja ya mtoa mada imesisimua akili yangu kufikiria yafuatayo – kwamba iwapo kuna mpango maalum tayari under way, basi kuna uwezekano mkubwa kwamba anayeandaliwa ni Dr. Abdalah Kigoda kwa sababu kuu tano zifuatazo:

  1. Moja ni argument ya udini: kumekuwa na hii hoja chini kwa chini, kwa muda sasa – kwamba wakristo wametawala kwa miaka 33 (Nyerere 23 + Mkapa 10),na waislamu miaka 20 (Mwinyi 10 + JK 10), hivyo akiingia Rais muislamu mwaka 2015, angalau itatokea hali ya usawa katika hilo yani miaka 33 ya Urais wa kikristo dhidi ya miaka 30 yaUrais wa kislamu.

  2. Mbili ni argument ya Rais kutoka kaskazini: nadhani itabidi ifikie mahali watunzi wa hoja kwamba Rais ajaye hatatokea Kaskazini (kama ni kweli walitamka hivyo) wajisafishe na kufanikisha mgombea atoke kaskazini. Hii ni mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga na Manyara. Dr. Kigoda anatokea Tanga. Wakifanikisha hili, wataua ndege watatu kwa jiwe moja.

  3. Tatu ni argument ya mahitaji ya mgombea neutral (asiyefungamana na upande wowote ndani ya CCM): Dr Kigoda anafiti vizuri katika mlinganyo huu kwani wagombea wengine wengi ni dhahiri kwamba wakisimamishwa, hapatakuwa na unconditional support kwa mgombea mmoja kutoka wagombea/makundi mengine, suala ambalo linaweza kukipasua chama.

  4. Nne ni argument ya zamu ya Rais Msomi (PhD): Kuna madokta/profesa ambao watajaribu bahati yao aidha kwa mara ya kwanza au mara ya pili na ambao wanaweza kuvutia wajumbe wa mkutano mkuu kutokana na usomi wao, hasa katika nyakati hizi, na pia kutokana na experience ya Dr. Slaa 2005, hivyo kuwepo na hoja kwamba tumjaribu msomi. Iwapo hoja hii itashika kasi, njia pekee ya kuwaondoa wagombea madokta na maprofesa wengine ni kusema OK FINE, YUPO DR. KIGODA, anafiti vizuri kama suala ni kukujaribu msomi wa kiwango hicho.

  5. Na mwisho ni tabia ya CCM kurudia historia. Ushindi wa JK 2005 ulichangiwa sana na the fact kwamba pamoja na nguvu kubwa ya jina lake 1995, hakuwa na kinyongo na mizengwe iliyotokea dhidi yake, na kwa utiifu mkubwa kwa Chama, alikubali kumuunga mkono mgombea aliyesimamishwa wakati ule. Lakini muhimu zaidi hapa ni kwamba, tangia wakati huo, majina ya wagombea ambao walishindana na JK 2005 na kushindwa, yamekuwa yanapewa nafasi zaidi for 2015 kuliko majina mapya. If this argument stands, then ebu tutazame waliobakia from 2005:

  · Sumaye – ataangushwa kwa urahisi naKigoda based on arguments namba moja na mbili hapo juu (among others);
  · Salim (yeye alishasema hagombei tena);
  · Mwandosya (Afya yake bado sio nzuri).

  Vinginevyo nadhani Dr. Kigoda ana vigezo vingi vizuri vya kuweka kuimudu nafasi ya Urais, na ana nafasi kubwa ya kupita iwapo wanaomuunga mkono ndani ya chama watajipanga vizuri.
   
 18. m

  mharakati JF-Expert Member

  #18
  Jul 31, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145

  mafaili ya kigoda kuuza uuza hovyo mashirika watayaweka wapi? mkapa analaumiwa kwa hili pamoja na ufisadi mwingine na pale kitchen alikuepo kigoda, pamoja na mramba na yona. sasa kama ufisadi itakua ni theme hadi 2015 basi kigoda, timu yake na sekretariet ya CCM itakua na wakati mgumu kuuzuia upinzani kurusha hili kombora la matumizi mabaya au kuuza mali za taifa kizembe.
   
 19. m

  mharakati JF-Expert Member

  #19
  Jul 31, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Prof Mwandosya angekua na afya yake ya kawaida ndiyo rais wanaCCM wazalendo tungemtaka 2015 kuja kuweka nchi kwenye mstari tena.
   
 20. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #20
  Jul 31, 2012
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  "Mwandosya (Afya yake bado sio nzuri)."

  Afya ya Kigoda ni mgogoro kuliko ya Mwandosya.
   
Loading...