Kudhibiti wahujumu uchumi: Mzee Kimiti amfananisha Rais Magufuli na mpambanaji shujaa Edward Moringe Sokoine

Jiwe anawakamata kweli mafisadi kibao ila tatizo lake kwanza bashite hata afanyeje ataendelea kupewa pipi, sijui wana mkataba gani, pili akikuchukia anakuweka kwenye kundi la hao wahujumu uchumi hata kama hujafanya hicho kitendo sababu tu huo uwezo anao huu ni ujinga, tatu wengine hawapigi madili yote anayapiga yeye sasa kwa kampuni zake. Ovyo kabisa hili dingi
 
Sokoine hakujilimbikizia mali. Mali zake karibia zote zilikuwa za urithi. Aliamini sana usawa!

Hakuamini usawa wowote, bali alikuwa bendera fuata upepo. Alichokuwa anasema Nyerere na yeye alikuwa anafuata hivyo bila hata kupima. Dunia ipi watu wote wanaweza kuwa sawa kama sio ujinga? Huyo na Nyerere ndio sababu hasa ya wananchi wa nchi kugeuka kuwa wanyonge.
 
Kwani sasa kuna anayengojea?

Taratibu za kisheria lazima zifuatwe!

Taratibu gani hizo? Mbona wapinzani na wale anaowachukia huwa hawangoji hizo taratibu? Akina Rugemalira, Kitilya nk wako ndani mpaka leo, mara uchunguzi haujakamilika sijui na uhuni gani, kwanini wasisubiri hizo taratibu za kisheria?
 
Haya maswali yanawahusu zaidi watu wa mahakama!
 
Mzee Paul Kimiti ambaye amewahi kushika nyadhifa mbalimbali nchini ikiwemo ubunge, ukuu wa mkoa na uwaziri kuanzia enzi za mwalimu Nyerere amemmwagia sifa za kutosha Rais Magufuli.

Mzee Kimiti anasema katika kupambana na wahujumu wa uchumi wa taifa letu Dr Magufuli anafanana sana na aliyekuwa Waziri mkuu awamu ya kwanza Edward Sokoine.

Sokoine hakumuogopa yoyote wala kumuonea aibu au kumpendelea yoyote na ndivyo alivyo Rais wetu mpendwa Dr Magufuli, amesisitiza.

Chanzo: Magazetini.

Maendeleo hayana vyama!
Milion 70 za ESCROW alirudisha?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee Paul Kimiti ambaye amewahi kushika nyadhifa mbalimbali nchini ikiwemo ubunge, ukuu wa mkoa na uwaziri kuanzia enzi za mwalimu Nyerere amemmwagia sifa za kutosha Rais Magufuli.

Mzee Kimiti anasema katika kupambana na wahujumu wa uchumi wa taifa letu Dr Magufuli anafanana sana na aliyekuwa Waziri mkuu awamu ya kwanza Edward Sokoine.

Sokoine hakumuogopa yoyote wala kumuonea aibu au kumpendelea yoyote na ndivyo alivyo Rais wetu mpendwa Dr Magufuli, amesisitiza.

Chanzo: Magazetini.

Maendeleo hayana vyama!

Kwa umri alionao Kimiti sasa ni senile. Siamini kuwa ana legal capacity ya kuingia mkataba na mtu yeyote halafu ukawa halali.

In short: hajui alisemalo sasa hivi.
 
Kwa umri alionao Kimiti sasa ni senile. Siamini kuwa ana legal capacity ya kuingia mkataba na mtu yeyote halafu ukawa halali.

In short: hajui alisemalo sasa hivi.
Mbona gari anaendesha na pale Kanisani ndiye mwenyekiti wa kamati ya Ujenzi?!
 
Labda awafananishe kwa kutopenda watu wafanikiwe, maana wote Wana chuki na matajiri uwatamani kuwashusha chini, maana hata sokoine aliwachukia matajiri
Tofautisha utajiri halali ambao mtu ameupata bila ya kuhujumu uchumi. Hata enzi za Marehemu sokoine palikuwepo matajiri wengi tu. Hoja ya msingi ni kudhibiti wahujumu uchumi,kama wakwepa kodi,watengeneza bidhaa za magendo n.k.
 
Muulize Mzee Kimiti atuambie Kange Lugola amefungwa jela gani kwa kuhujumu uchumi. Mzee Kimiti ajitahidi kutenganisha wapambanaji na wahujumu uchumi, na watu wenye madaraka wenye chuki binafsi na wanaokomoa watu wasiowapenda kwa kisingizio cha kupambans na wahujumu uchumi. Kisha mwambie mzee Kimiti CAG haruhusiwi kukagua ujenzi wa SGR, SG na ununuzi wa ndege, ili asimchanganye Sokoine na walevu wa madaraka.
Ishu ya akina Kangi Lugola ishu ipo kwa Dpp nafikiri ni vyema sasa ukasubiri achambue nani anahusika au nani hausiki alafu afungue kesi. Usihukikumu mtu kabla suala halijaenda mahakamani.
 
Back
Top Bottom