Kudhibiti wahujumu uchumi: Mzee Kimiti amfananisha Rais Magufuli na mpambanaji shujaa Edward Moringe Sokoine

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,512
141,240
Mzee Paul Kimiti ambaye amewahi kushika nyadhifa mbalimbali nchini ikiwemo ubunge, ukuu wa mkoa na uwaziri kuanzia enzi za mwalimu Nyerere amemmwagia sifa za kutosha Rais Magufuli.

Mzee Kimiti anasema katika kupambana na wahujumu wa uchumi wa taifa letu Dr Magufuli anafanana sana na aliyekuwa Waziri mkuu awamu ya kwanza Edward Sokoine.

Sokoine hakumuogopa yoyote wala kumuonea aibu au kumpendelea yoyote na ndivyo alivyo Rais wetu mpendwa Dr Magufuli, amesisitiza.

Chanzo: Magazetini.

Maendeleo hayana vyama!
 
Muulize Mzee Kimiti atuambie Kange Lugola amefungwa jela gani kwa kuhujumu uchumi. Mzee Kimiti ajitahidi kutenganisha wapambanaji na wahujumu uchumi, na watu wenye madaraka wenye chuki binafsi na wanaokomoa watu wasiowapenda kwa kisingizio cha kupambans na wahujumu uchumi. Kisha mwambie mzee Kimiti CAG haruhusiwi kukagua ujenzi wa SGR, SG na ununuzi wa ndege, ili asimchanganye Sokoine na walevu wa madaraka.
 
Kuna Taifa kama China wakiwa wanasoma Sifa tunazomwagia Kiongozi Wetu kwa kupambana na ufisadi na hatua tulizochukua kwao ni kama comedy show na wanaburudika.

Chenge
Lowasa
Membe
Jiwe..list inaendelea..

Watu wa Kufanana na Sokoine huwezi kuwapata CCM.
Msimdhalilishe .
 
Kimiti ni mapambio kama wewe, after all ni spent force. katika historia yetu, hakuna awamu ya "upigaji" kama hii. hao wanaopelekwa kortini ni visa vya Jiwe na wao na si dhamira ya kupambana na uhujumu uchumi. Wapi Lugola, wapi kigwangala, wapi Mpina , wapi madudud ya jeshi toka CAG report. Rubbish!
 
Labda awafananishe kwa kutopenda watu wafanikiwe, maana wote Wana chuki na matajiri uwatamani kuwashusha chini, maana hata sokoine aliwachukia matajiri
 
Kuna Taifa kama China wakiwa wanasoma Sifa tunazomwagia Kiongozi Wetu kwa kupambana na ufisadi na hatua tulizochukua kwao ni kama comedy show na wanaburudika.

Chenge
Lowasa
Membe
Jiwe..list inaendelea..

Watu wa Kufanana na Sokoine huwezi kuwapata CCM.
Msimdhalilishe .

Siku ukiona maswaiba zake wako jela ndio tutaamini kweli dhamira ya kupambana na ufisadi ni ya kweli, huwezi ukapambana na ufisadi au uhujumu uchumi huku bashite,chenge,ngeleja nk wako nje.Mapapa yako nje ndani ni vibaka wa Mia mbili Mia mbili wengi ni watumishi sababu ya njaa ndo wamejaa ndani sababu hawana chapa.
 
  • Thanks
Reactions: prs
Mzee Paul Kimiti ambaye amewahi kushika nyadhifa mbalimbali nchini ikiwemo ubunge, ukuu wa mkoa na uwaziri kuanzia enzi za mwalimu Nyerere amemmwagia sifa za kutosha Rais Magufuli.

Mzee Kimiti anasema katika kupambana na wahujumu wa uchumi wa taifa letu Dr Magufuli anafanana sana na aliyekuwa Waziri mkuu awamu ya kwanza Edward Sokoine.

Sokoine hakumuogopa yoyote wala kumuonea aibu au kumpendelea yoyote na ndivyo alivyo Rais wetu mpendwa Dr Magufuli, amesisitiza.

Source magazetini.

Maendeleo hayana vyama!
Ripoti ya CAG inaonyesha kati ya awamu zote hii ya tano imeongoza kwa ubadhirifu. Kwa taarifa hii, Kimiti anamkosea sana Sokoine. Watu wakisha. Zeeka waache kutoa mawazo yasiyo na tafiti. Akae kimya alee wajukuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muulize Mzee Kimiti atuambie Kange Lugola amefungwa jela gani kwa kuhujumu uchumi. Mzee Kimiti ajitahidi kutenganisha wapambanaji na wahujumu uchumi, na watu wenye madaraka wenye chuki binafsi na wanaokomoa watu wasiowapenda kwa kisingizio cha kupambans na wahujumu uchumi. Kisha mwambie mzee Kimiti CAG haruhusiwi kukagua ujenzi wa SGR, SG na ununuzi wa ndege, ili asimchanganye Sokoine na walevu wa madaraka.
Kangi Lugola atapandishwa kizimbani soon!
 
Sokoine hakujilimbikizia mali. Mali zake karibia zote zilikuwa za urithi. Aliamini sana usawa!
 
Back
Top Bottom