johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,947
- 141,922
Kiukweli sisi wahenga tunakumbuka vizuri vita ya wahujumu uchumi miaka ile ya 1980s iliyosimamiwa na Waziri mkuu wa wakati ule rip Edward Moringe Sokoine.
Vita ile ilisomba wengi na kwa kuwa hapakuwepo fursa kama hii iliyotolewa na Rais Magufuli watuhumiwa wengi walikaa gerezani kwa muda mrefu na wengine kuonekana hawana hatia baada ya kuwa wamesota sana rumande.
Msamaha wa Rais Magufuli utasaidia kuwaondoa wakosaji wengi kwani watatubu na kurejesha fedha na wao kuachiwa.
Hii maana yake ni kuwa kesi za ufisadi zitapungua sana na wale wachache wanaoamini wameonewa hivyo hawajatubu kesi zao zitasikilizwa kwa haraka na watapata haki yao
Kwa mara ya kwanza Tanzania tunafaidi matunda ya kuongozwa na Rais ambaye ni mwanasayansi
Maendeleo hayana vyama!