Kubomolewa Jengo la TANU ni dhambi ya kihistoria

CCM ina vichwa makini hayo yote yamejadiliwa kwa muda mrefu katika vikao husika, hivyo uamuzi ulifikiwa ni huo! Nyie msiotakia mema CCM kwa nini kila uamuzi unaofikiwa na chama chetu unatilia mashaka? Umefika wakati wa kutumia raslimali kuingiza pesa na si vinginevyo. WEWE MBONA nyumbani kwenu hukuzuia kubomolewa kwa nyumba ya aliyezaliwa babu mzaa babu yako!!!!!
Sikiliza rafiki, hizi ni tunu za taifa, kwa nini kuna sheria ya Mambo ya Kale ya mwaka 1964, na marekebisho yake ya 1979 na na kuna kanuni zake kibao. Uamuzi huo wa chama chenu ni wa kiupuuzi na wakishetani, mmejaa mafisadadi, mmechanganyikiwa hamjuai hata lipi sahihi na lisilo sahihi kufanya. Na hii naomba kwa kuvunga jengo la hilo CCM ife kabisa, na iwe laana kabisa. Hiyo ilipaswa ndilo liwe hekalu la CCM. Ktaaalamu, hata katika business, kunakutu kinaitwa collections, hizi zinahistorical value na historical value haiozi wala kupungua. Kama heshma ya ukombozi nchini imepungua basi CCM imeshachanganyikiwa.
 
CCM ina vichwa makini hayo yote yamejadiliwa kwa muda mrefu katika vikao husika, hivyo uamuzi ulifikiwa ni huo! Nyie msiotakia mema CCM kwa nini kila uamuzi unaofikiwa na chama chetu unatilia mashaka? Umefika wakati wa kutumia raslimali kuingiza pesa na si vinginevyo. WEWE MBONA nyumbani kwenu hukuzuia kubomolewa kwa nyumba ya aliyezaliwa babu mzaa babu yako!!!!!
Sawa ni vichwa, vimejaa maji tu, hawazungushi ubongo! kama serikali yenyewe ya TANU kuheshimu tunu za kitaaifa, ni Idara ya kwanza kuundwa na wakoloni mwaka 1937 na wakoloni, Nyerere akaanzisha sheria Mwaka 1964, ukisoma marais wote waliiimarisha sheria ya Mambo ya Kale! Je Serikali ya Awamu 4 imefanya nini? Bomoa historia nzima ya nchi. Tanzania hatuna uchache wa maeneo?
 
Kamanda, nakushuruku kwa kuliona hili jambo. Lile jengo bado lilikuwa imara, tena lingeweza kuwapo kwa miaka mingine 100 au zaidi. Hapakuwa na sababu ya kubomoa jengo ambalo bado liko imara na si hatari kwa maisha ya binadamu. Hoja ya CCM, kama umefuatilia vema, ni kuliondoa ili kuweka 'Kitega Uchumi'! Kwa hiyo hoja si uzee, bali kuingia pesa! Unaweza kujiuliza, nchi hii imekuwa finyu kiasi kwamba uwanja pekee wa kuwekwa kitega uchumi cha chama ni kubomoa Jengo la TANU? Hakika uamuzi huu naulaani.
Kamanda kana ni hivyo, kuna uwezekano CCM imeanza kuona mbali, hilo jengo ndilo mali pekee ya halali ya CCM!, mali nyingine zote za CCM kabla ya 1992, ni mali za umma, hivyo tulipoanza vyama vingi, CCM, ilipaswa kurejesha serikali zime mali za umma, hivyo ilichofanya CCM ni kupora mali ya umma, in case upinzani unachukua nchi, kazi ya kwanza ni kuipurura CCM mali zote za umma ilizojimilikisha, hivyo hilo jengo ndilo pekee mali halali ya CCM, inawezekana hili wameliona, hivyo wameamua kujiandaa mapema kukitumia vema kidogo walichonacho kabla hawajapururwa!.

Ngoja tuisubirie taarifa rasmi ya CCM kutufafanulia!.

Pasco
 
Siamini kama ni wewe .....yaani piramid zinabomolewa sembuse hilo jengo la magamba?
labda lingekuwa "limetabarukiwa" kama yale majengo yetu hapo ninge kuunga mkono mkuu @manyerere
 
Manyerere Jackton
Mkuu Manyerere asante kwa hii, This is sad!, very sad indeed! kama ni kweli, Mzimu wa Babu yako, utawaibukia!.
Kuna uzi humu niliwahi kuuliza Jee Watanzania ni Ignorants? au Tumelogwa?!. Huu ni uthibitisho hata viongozi wetu ni ignorants mpaka basi!,

Japo mimi sijapita hapo Lumumba, naomba kutoa angalizo lenye some minimum reasonable doubt, kuwa kinachofanyika, sio lazima iwe ni kuvunja, bali wanaweza kuvunja baada ya kujiridhisha restoration haiwezi kulidumisha kwa sababu original structure ni udongo ambao hauwezi kudumu miaka milioni moja ijayo, hivyo kinachofanyika sasa ni ku demolish the old structure, kisha kujenga replica vile vile, halafu ile ample wastage space, ndio inakuwa put to more economical news ikiwemo kujenga ghorofa on top for investment!.
This is my assumption tuu!.

Pasco
Pasco! hili suala si la kutetea hata kidogo! Huu ni usaliti wa historia ya nchi yetu! Historical value ya jengo hilo haiwezi kuondolewa na mtutu yeyote anayethamini harakati za ukombozi wa TANU. Nakushauri usome earthern architecture ambayo kuna wataalamu waliobobea! Suala, ni mtaalamu gani kawashauri? sababu sekta hii imeanza kudharauriwa na awamu ya nne! Rejea ubomoaji wa majengo ye kihistoria hapo Dar es salaam! Marais wote waliopita waliimarisha sheria hii! Na wakoloni walifanya kazi kumbwa hiyo ambayo inadharaurika na CCM ya miaka. Mfano wakoloni walianza miaka 1900's kuuuhifahdi mji wa Kilwa Kisiwani na Songo Mnara, hao ni wajerumani,Olduvai nk; mwingereza aktunga sheria mwaka 1937, Mwalimu Nyerere 1964/79, na mioongozo ya 82, mwinyi nae uhifadhi wa jiji la Dar es salaam, na Mkapa sheria za utafiri nk! Katafute awamu ya nne imevunja asilimia kubwa ya architectural heritage ya Dsm, historical life kama mahoteli ikiwemo salamander na ina mpango wa kuvunja Forodhani nk!, Kumbuka DSm cultural Centre etc.
Na ubomoaji uliasisiwa na Lowassa! hiyo ni hadithi nyingine! Lumumba ndiko kulianzia chuo kitivo cha Sheria nadhani?
Hii ni Laaana! Watu wa accounting na biashara nadhani wanakitu kinaitwa collections = these could be historical treasures or items may not decline in value! Japo kuna may, lakini kiutaalamu wangu haziwezi kutoka thamani.
Kuna mji kama roma, kuna gofu, wacha hilo jengo liabaki gofu, watalii na wanafunzi wangeelezwa hili gofu ndipo mahali harakati za kutafuta uhuru wa nchi zilianzia.
Hii ni dhambi kubwa Pasco! Wameamua kuzika mpaka historia yako! Wanataka viyoyozi vya kisasa. Aibu ya Mwaka. Nadhani watafuta hata somo la Archaeology na heritage Management ya Mlimani!
 
Siamini kama ni wewe .....yaani piramid zinabomolewa sembuse hilo jengo la magamba?
labda lingekuwa "limetabarukiwa" kama yale majengo yetu hapo ninge kuunga mkono mkuu @manyerere

Acha uwongo niandiki piramid la wapi lililovunjwa! No historia ya Tanu, si ya Magamba, kuwaita waaasisi wa nchi kama magamba ni kutofikiri vizuri kabla hujaandika ndugu yangu. Hao magamba wanaovunja, wangejua ingekuwa ni dini hilo ndilo hekalu la CCM, lingekuwa dogo na ni makuhani wakuuu tu na maamuzi makubwa ya kichama yangefanyika, badala ya Dodoma. Huu ni upuuzi tu.
 
Pasco! hili suala si la kutetea hata kidogo! Huu ni usaliti wa historia ya nchi yetu! Historical value ya jengo hilo haiwezi kuondolewa na mtutu yeyote anayethamini harakati za ukombozi wa TANU. Kuna mji kama roma, kuna gofu, wacha hilo jengo liabaki gofu, watalii na wanafunzi wangeelezwa hili gofu ndipo mahali harakati za kutafuta uhuru wa nchi zilianzia.
Hii ni dhambi kubwa Pasco! Wameamua kuzika mpaka historia yako! Wanataka viyoyozi vya kisasa. Aibu ya Mwaka. Nadhani watafuta hata somo la Archaeology na heritage Management ya Mlimani!
Mkuu Rare, asante, by the way, nilibahatika kulitembelea hilo jengo nilipokuwa Rome, tena sio jengo tuu, hata mavazi yale watu wanavaa na watalii wanapiga nao picha!.

Pasco.
 
CCM ina vichwa makini hayo yote yamejadiliwa kwa muda mrefu katika vikao husika, hivyo uamuzi ulifikiwa ni huo! Nyie msiotakia mema CCM kwa nini kila uamuzi unaofikiwa na chama chetu unatilia mashaka? Umefika wakati wa kutumia raslimali kuingiza pesa na si vinginevyo. WEWE MBONA nyumbani kwenu hukuzuia kubomolewa kwa nyumba ya aliyezaliwa babu mzaa babu yako!!!!!

Mwalimu Nyerere alipopingana na hoja nyembamba kama hizi alitunga utenzi huu:
Wengi wakichachamaa,
Watakalo watatwaa,
Ila si kweli kusema
Daima hutaka mema.

Wengi wakisha amua
Mama yako kumuua,
Kwa kuwa wao ni wengi,
Utashiriki, hupingi?

Kitabu hicho kinachoitwa "Tanzania! Tanzania!", Mwalimu alikiandika Novemba 16, 1993.
 
Unashangaa hilo...! profesa kasema anawashukuru Ujerumani kwa kuitawala Tanganyika maana walituletea maendeleo.
 
Acha uwongo niandiki piramid la wapi lililovunjwa! No historia ya Tanu, si ya Magamba, kuwaita waaasisi wa nchi kama magamba ni kutofikiri vizuri kabla hujaandika ndugu yangu. Hao magamba wanaovunja, wangejua ingekuwa ni dini hilo ndilo hekalu la CCM, lingekuwa dogo na ni makuhani wakuuu tu na maamuzi makubwa ya kichama yangefanyika, badala ya Dodoma. Huu ni upuuzi tu.

BELIZE CITY -- A construction company has essentially destroyed one of Belize's largest Mayan pyramids with backhoes and bulldozers to extract crushed rock for a road-building project, authorities announced on Monday.
The head of the Belize Institute of Archaeology, Jaime Awe, said the destruction at the Nohmul complex in northern Belize was detected late last week. The ceremonial center dates back at least 2,300 years and is the most important site in northern Belize, near the border with Mexic
o-MAYAN-PYRAMID-DESTROYED-570.jpg


belize-mayan-pyramid.png
 
KIm-JOng-Un, nadhani tunachopaswa kufanya ni kujifunza yaliyo mema, tena yenye faida. Kubomoa historia yetu kwa sababu wapo wengine wapuuzi wamefanya hivyo, ni kuonyesha kuwa sisi ni wapuuzi zaidi.
 
Kweli kabisa, mimi ningewaelewa wanaopinga kubomolewa kwa jengo hilo kama wangependekeza lisiwe la CCM kwanza ili historia yenyewe iwe na maana wakati ambao nchi inafuata mfumo wa vyama vingi, lakini kama wanakubaliana ni jengonla CCM sioni tabu kama wameamua kulivunja.

Tatizo lenu ni hilo. Hamtafakuri kwa kina hoja mnakurupuka kujibu matokea yake mnakuwa na hoja dhaifu kuliko. Ni ukweli usiopingika kuwa TANU ina historia ambayo haitokaa ifutike katika nchi hii. Vivyo hivyo CCM. Yapo amabayo tutaendelea kuyakumbuka ingawa hatutasahau pia jinsi mlivyobadilika kama kinyonga na kuanza kuitafuna nchi.
 
Nina uhakika jibu ni hapana. Kumbuka kwa wakati huo watu walipenda kwa dhati vyama vyao. Kila mtu alijitolea kukiinua chama. Sasa hivi hali ni tofauti maana baadala ya kukisaidia chama wengi wetu tunavitafuna au tunavitumia vyama kwa manufaa yetu wenyewe. Hili ni kwa kila chama TZ.
 
IMG_4947.JP


Wananchi wakiangalia jengo la ofisi ndogo ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) la Lumumba, ambapo kilizaliwa chama cha Tanu lililobomolewa kupisha ujenzi wa jengo jipya la chama hicho Dar es Salaam jana



JENGO
la ofisi ndogo la Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Mtaa wa Lumumba Dar es Salaam ambako ndiko kilizaliwa Chama cha Tanu limebomolewa ili kupisha ujenzi wa jengo jipya la chama hicho.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema jengo hilo limebomolewa kwa ajili ya matengenezo ya kawaida.

"Tunachokifanya katika jengo hili ni ukarabati wa kawaida,"alisema Nape wakati akielezea jengo hilo ambalo limebomolewa jana kwa kutumia tingatinga.

Kutokana na kubolewa kwa jengo hilo , viongozi wa ngazi mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu wa CCM,Abdulrhaman Kinana , watakuwa katika Jengo la Umoja wa Vijana wa chama lililopo barabara ya Morogoro, wakati ukarabati wa jengo hilo lililobomolewa ukiendelea.

Awali baadhi ya makada wa chama hicho waliokuwa eneo hilo, walidai kuwa jengo hilo la Tanu limebolewa ili kupisha ujenzi wa jengo la kisasa ambalo litatumika kwa ajili ya kitega uchumi.

Makada hao walisema jengo hilo litakapokamilika litakuwa la kisasa zaidi tofauti na jengo ambalo lilikuwepo eneo hilo.


Chanzo: Globalpublishers
 
Ukarabati ???
Tingatinga limeangusha chini sasa ukarabati wapi? Au sielewi maana ya neno "ukarabati"?
 
Ujue hapo ndio laana inapoanzia. Lile jengo lilistahili kubakia lilivyokuwa karne na karne! Vizazi vijavyo vifunge safari kutoka mikoan kuja kuona TANU (UKOMBOZI) ilipoanzia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom