Kubenea apandishwa Mahakamani leo

Kubenea apandishwa Mahakamani leo

Nasikia sababu ni majibu mabaya kwa dc wake,ila kwa maneno ya shombo naye yumo kubenea,du awe makini nahisi kama ni asubuhi sana
 
sijaona kosa la makonda ..!

hajavunja sheria yoyote..

annayao haki ya kuamrisha kubena kukamatwa inapobidi....

nasikia kuna ushahidi wa mkanda wa video akitoa hayo maneno machafu .....

angenyimwa dhamana ...
 
huyo makondakta wenzake wanaangaika kukamata wakwepa kodi bandarini yeye anashindwa hata kukusanya uchafu wa uhuru anashupaa na siasa za mata.ko wazi! hiyo wilaya bora apewe lusinde over!
 
Hivi kuna mtu hata mmoja ambaye anampenda:
1. Nape
2. Makonda
Itabidi watu hawa wajitafakari.
 
kwani hujaona shitaka lake mpaka sasa?
KawashtAkini waliouza nyumba za serikali na wale wa Escrow.. Hii nchi ni yetu sote. Tunaumia sana mnapojiona Kua nyinyi ndio Watanzania zaidi.
 
Hii movie imetegenezwa maksudi na Makonda kwa nia ya kuhujumu uchaguzi wa meya wa Kinondoni, Makonda alitengeneza mazingira mabaya jana akijua moja kwa moja kuwa lazima Kubenea atakataa ndipo wakajibizana na yeye kutumia Udikiteta kumkamata Mbunge na polis pasipo kujali nani chanzo cha Tatizo wakaamua kuegemea kwa mkuu wa wilaya kunyanyasa Mbunge, hizi sheria mbovu zinazompa mamlaka mkuu wa wilaya kuweka watu ndani hata kama yeye ndiyo mchokozi lazima zifutwe haraka vinginevyo wakuu wa wilaya wenye Akili za Kazi kwanza fikiri baadae au kazi kwanza tafakari baadae watachomoza kwa kasi na kuendeleza unyanyasaji kwa wananchi.

Kwa hiyo unataka kumaanisha Makonda alijua Kubenea atatoa matusi? Ifike mahala watu mjenge uzalendo na kukemea mabaya hata kama ni ya watu mnaowapenda. Si ustaarabu kutukana, na wala sheria zetu haziruhusu matusi. Mtu kama mbunge kutukana hadharani tena mbele ya kadamnasi ni aibu na ujinga usioelezeka. Mnataka sheria zibadilishwe ili tu ziwalinde wabunge wenye tabia ya kutukana kama alivyofanya Kubenea?
 
Wana bifu la siku nyingi. Acha atakayeshindwa atamheshimu mwenzake
 
Avoid power showoff by all cost. It is not beneficial to both of you two neither to public by large.
 
Kinondoni wilaya kubwa sana kwa huyu dogo,angepewa liwale huko
 
Kwa hiyo wewe unasupport Kubenea kumtukana Makonda? Kubenea hana adabu na hajaanza leo. Ni swala la muda tu mtawajua vyema. Acha sheria ifuate mkondo wake.

Kila kitu kina mwanzo na mwisho. Kubenea amekuwa akitumia kalamu yake, kama mwandishi, kutukana na kukashfu watu. Kwenye majukwaa ya siasa, amefanya hivyo hivyo. Sasa anasahau kuwa ni mbunge (heshima, busara na hekima hutawala maneno na matendo) na hayuko kwenye ulingo wa siasa tena wala bungeni, kuwa makini na vitendo na maneno yake. Kagusa himaya nyingine mahala pasipo pake, anaisoma namba.

Tusishabikie utovu wa nidhamu.

TAFAKARI CHUKUA HATUA.
 
Vile makonda kumpiga warioba c utovu wa nidham?
 
Mkapa alitoa lugha chafu pia!! Aliwaita watu malofa na wapumbavu
 
Kila kitu kina mwanzo na mwisho. Kubenea amekuwa akitumia kalamu yake, kama mwandishi, kutukana na kukashfu watu. Kwenye majukwaa ya siasa, amefanya hivyo hivyo. Sasa anasahau kuwa ni mbunge (heshima, busara na hekima hutawala maneno na matendo) na hayuko kwenye ulingo wa siasa tena wala bungeni, kuwa makini na vitendo na maneno yake. Kagusa himaya nyingine mahala pasipo pake, anaisoma namba.

Tusishabikie utovu wa nidhamu.

TAFAKARI CHUKUA HATUA.

Alipomzaba kibao Warioba Mahakama zipi zilimfunga? Kalamu ya Kubenea si ndo inamsaisia Magufuli kumulika TRA?TPA na kwingineko Mkuu? tumia bongo kufikiri, achana na mambo ya ccm mbele kwa mbele!
 
Back
Top Bottom