It is becoming more obvious day by day kwamba Mradi wa Makonda ulilenga kufanikisha mambo makuu yafuatayo:
1. Kuzima mvuto wa wagombea funali fulani - Urais CCM 2015.
2. Kurudisha imani ya vijana kwa chama cha mapinduzi kupitia ujumbe wake Bunge la Katiba.
Katika haya yote, hakufaulu. Lakini juhudi zake zikapelekea kupewa zawadi ya Ukuu wa Wilaya ya Kinondoni. Inaonekana kwamba uteuzi huo ulilenga kufanikisha jambo lingine - nalo ni kurudisha imani ya Vijana kwa CCM katika jiji la DSM, lakini hasa Kinondoni ambayo ndio wilaya namba moja Tanzania. Lakini tofauti na ilivyotarajiwa, katika mradi huu pia amefeli. Pamoja na jitihada za CCM kugawanya jimbo la ubungo na pia juhudi za Makonda kubuni njia mbalimbali za kushawishi wapiga kura vijana waiunge mkono CCM, Chini ya makonda, CCM imeingia hasara zaidi:
1. Jimbo pekee la CCM Wilaya ya Kinondoni (Jimbo la Kinondoni) limepokonywa na UKAWA chini ya Makonda.
2. CCM imeshindwa kurudisha majimbo iliyopoteza 2010 (Kawe na Ubungo).
3. Mbaya zaidi, hata jimbo jipya lililotengenezwa na CCM (Kibamba), nalo limeenda UKAWA.
Kwa hali hii, Makonda hana tena political legitimacy Kinondoni. Alichobakia nacho ni political authority kupitia. Mamlaka haya haijabadilika tangia ukuloni.
Makonda anatakiwa aelewe kwamba Political Authority pekee yake haiwezi kumsaidia kutatua changamoto husika bila ya kuwa pia na Political Legitimacy.
Alichokifanya kwa Mbunge wa Ubungo (Chadema) ni matumizi mabaya ya madaraka. Ni kitendo cha aibu na ni liability kisiasa kwa CCM.