Elly Corner
Member
- Sep 10, 2014
- 36
- 35
Niseme tu kuwa sasa nimeanza kumchukia Magufuli.
Sawa endelea kumpenda kubenea na umchukie magufuli...it wont change anything
Niseme tu kuwa sasa nimeanza kumchukia Magufuli.
Hii movie imetegenezwa maksudi na Makonda kwa nia ya kuhujumu uchaguzi wa meya wa Kinondoni, Makonda alitengeneza mazingira mabaya jana akijua moja kwa moja kuwa lazima Kubenea atakataa ndipo wakajibizana na yeye kutumia Udikiteta kumkamata Mbunge na polis pasipo kujali nani chanzo cha Tatizo wakaamua kuegemea kwa mkuu wa wilaya kunyanyasa Mbunge, hizi sheria mbovu zinazompa mamlaka mkuu wa wilaya kuweka watu ndani hata kama yeye ndiyo mchokozi lazima zifutwe haraka vinginevyo wakuu wa wilaya wenye Akili za Kazi kwanza fikiri baadae au kazi kwanza tafakari baadae watachomoza kwa kasi na kuendeleza unyanyasaji kwa wananchi.
Makonda hana hadhi ya kuwa kiongozi, labda akaimbe muziki
Kwani kubenea alimwita kibaka??? Aaah kama unamwita mkuu wa wilaya kibaka tena...hayo maneno wapi na wapi??
Ndio atambuwe kuwa mbunge hakumaanishi kuwa juu ya sheriaMbunge wa Ubungo, Saed Kubenea anafikishwa mahakamani Kisutu muda huu.
Huku ni kuiongezea mahakama mrundikano wa kesi zisizo na kichwa wala miguu.
Kwa mtindo huu lazima Makonda ajitafakari mara mbili mbili
=============
UPDATES;
Mbunge wa jimbo Ubungo kupitia Chadema, Saed Kubenea amepandishwa kizimbani kortini Kisutu, jijini Dar es Salaam leo na kusomewa shtaka la kutoa lugha chafu dhidi ya Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.Hata hivyo, Kubenea amekana kufanya kitendo hicho na kesi yake kuahirishwa hadi Desema 29, mwaka huu.
Aachiwa kwa dhamana.
Nasikia alimwambia kuwa ni kibaka baada ya yeye kuambiwa ni nani!
Inasemekana kuwa huyo DC Makonda ameframe charge ya kuwa Kubenea amemtukana kuwa yeye ni mjinga sana!
Duh................. kazi kweli kweli............. kama kila anayeitwa mjinga hapa jijini Dar angefungua mashitaka, basi ingekuwa balaa kubwa.............
Mbona Makonda alivyo mpiga Warioba hakukamatwa na polisi wala kupandishwa kizimbani?
Niseme tu kuwa sasa nimeanza kumchukia Magufuli.
Utajiju, sisi mbele kwa mbele.
Unauhakika gani kama Makonda alitukanwa??Kwanini atoe order polisi kunyang'anya kamera za waandishi wa habari??Nani asiyejua Makonda amepata ukuu wa wilaya baada ya kumpiga Mzee Warioba???Kwa hiyo wewe unasupport Kubenea kumtukana Makonda? Kubenea hana adabu na hajaanza leo. Ni swala la muda tu mtawajua vyema. Acha sheria ifuate mkondo wake.
Magu wala hana tatizo. Tatizo hapa ni kila kiongozi kutaka kuonekana mtendaji, kesho utasikia naye mwenyekiti wa kitongoji kaamurisha flani atiwe ndani, kesho kutwa napo utasikia balozi wa nyumba kumi, yaani bora tu nao waonekane watendaji.
Hivi ulishawahi kumpenda? Kwa mahaba uliyonayo kwa Edo!Niseme tu kuwa sasa nimeanza kumchukia Magufuli.