Kubadilisha Avatar

Kubadilisha Avatar

SHIEKA

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
8,240
Reaction score
4,280
Halo Wanachitchat! Nawasalimu wote! Kabla ya kusoma hii thread, bila shaka utakuwa umeiona avatar yangu mpya.Usishangae, nimeichagua kwa kuipenda sana.

Unajua, inafika wakati unaichoka avatar - unaiona kama imechuja vile. Avatar niliyoiacha juzi ilianza kunichosha kwa kupoteza ladha. Nikaibadilisha lakini hiyo mpya nikaiona imekaa kitoto zaidi nikaiacha. Sasa nimekuja na hii asmbayo nimeipenda kwa sababu inaakisi maisha yangu kwa sasa hivi yaliyojaa mshangao, huzuni,kukata tamaa,kizunguzungu nk.

MSHANGAO: Yaani hii nchi kila kitu kinanishangaza. Kiongozi na akili zake timamu anasifia jeshi la polisi kwamba linafanya kazi nzuri sana huku tunajua wazi kwamba jeshi la polisi linanyanyasa wananchi kwa kuwabambikizia kesi, kuwaua na kuwanyang'anya mali zao. Ninajua ni baadhi ya mapolisi si wote - ila kwangu samaki mmoja akioza basi wote walio kwenye tenga wameoza! Mshangao umejaa kichwani mwangu ninapoona eti matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2012 yaandaliwe upya leo mwezi wa tano 2013!
Nina mshangao mkubwa kuona kwamba ni mpaka moto uwake na kuunguza watu ndo tunaanza kuulizana cheche zimetoka wapi ilhal muda wote tulikuwa tunaziona hizo cheche!
Tena mshangao wangu mkubwa ni kusikia viongozi tunaowaamini wakipayuka kwa sauti kubwa kwamba wana ushahidi wa video unaoonesha watu wenye mipango ya kufanya ugaidi humu nchini na mara hawa watu wanapofikishwa mahakamani
wanaambiwa hawana kesi ya kujibu! Je hao waheshimiwa sana walioona hiyo video akili zao ni timamu? Nashangaa mpaka macho yangu yanageuka makengeza!

HUZUNI: Nimejawa na huzuni nyingi wanachitchat kwa kujulishwa kwamba watanzania kadhaa huko Arusha wamepoteza maisha kwa namna ambayo ingeweza kabisa kuepukika.

KUKATA TAMAA: Mwenzenu mie nshakata tamaa na mambo ya nchi hii kitambo, sijui nyie. Viongozi kwenye wizara ya nishati wameapa kwamba hakuna mgao wa umeme lakini jana nililala kwenye giza! Hata ninapoandika thread hii umeme umekatika mara mbili. Mbali na hayo, nikimpa mke wangu sh 20,000 za kwenda sokoni ananiambia hazitoshi: mchele kilo sh 2,500 sukari kilo sh 2,200 nyama kilo sh 5,000. Familia yangu ni ya watu 5.

KIZUNGUZUNGU: Kichwa changu hakikai vizuri na huwa nahisi sauti kama kengele pale ninaposikia viongozi wa nchi hii
wanatumia maneno yafuatayo kutatua matatizo yetu: tumejenga barabara za lami, tupo kwenye mchakato, tunalifanyia kazi, tuna habari na hilo, nk.Maneno haya nimeyasikia sana kuanzia 2005 na mpaka sasa yameanza kuniletea kizunguzungu; sielewi yaani.

Nimeona wanachitchat kadhaa nao wamebadili avatar zao. Je sababu ni nini? Waliobadili avatar ni pamoja na best yangu Boflo, Preta, Mamdeny sakapal, Kipipi Smile Erickb52na wengineo.
 
Last edited by a moderator:
Nimeona wanachitchat kadhaa nao wamebadili avatar zao. Je sababu ni nini? Waliobadili avatar ni pamoja na best yangu Boflo, Preta, Mamdeny sakapal, Kipipi na wengineo.

Heeeh!! kumbe huwa unaona nnavobadili avatar!!! hehehehe thanks 4 that,mie huwa nabadili avatar kwa sababu napenda sana pictures na huwa napenda muonekano tofauti tofauti kwa mtizamo wangu mwenyewe. Those avatars ambazo umeziona nimekuwa nikiweka zina resemble who and how I am in front of others.
 
Siyo kosa lako kwani wamekupigia simu kuwa bomba la nyumbani maji yamerudi. Nipe ratiba yako ya weekend kwani mimi nitatoka na Arabela na shem wangu KOKUTONA. Nipe mwongozo wa maeneo.
Halo Arushaone! Huku bush ninakokaa hakuna maeneo yanayowafaa Arabela na KOKUTONA. Hakufai! Mvua zinanyesha na mabanda mengi yanavuja! Bakini hukohuko!
 
Last edited by a moderator:
Heeeh!! kumbe huwa unaona nnavobadili avatar!!! hehehehe thanks 4 that,mie huwa nabadili avatar kwa sababu napenda sana pictures na huwa napenda muonekano tofauti tofauti kwa mtizamo wangu mwenyewe. Those avatars ambazo umeziona nimekuwa nikiweka zina resemble who and how I am in front of others.
Nakufatilia sana sakapal tangu nilipokukuta kwenye jukwaa la jokes ukiifurahia joke moja ambayo hata mimi niliipenda sana. Halafu siku moja ukaleta thread ukisema kwamba ulikuwa hujisikii vizur ulitaka uchangamshwe. Nikakukumbushia hiyo joke ukafurahi sana na siku yako ikachangamka.Avatar ya wakati huo ni kweli ilikuwa ikireflect kicheko. Pamoja na hayo samahani sijapata muda wa kusign autograph yako!
 
Halo Wanachitchat! Nawasalimu wote! Kabla ya kusoma hii thread, bila shaka utakuwa umeiona avatar yangu mpya.Usishangae, nimeichagua kwa kuipenda sana.

Unajua, inafika wakati unaichoka avatar - unaiona kama imechuja vile. Avatar niliyoiacha juzi ilianza kunichosha kwa kupoteza ladha. Nikaibadilisha lakini hiyo mpya nikaiona imekaa kitoto zaidi nikaiacha. Sasa nimekuja na hii asmbayo nimeipenda kwa sababu inaakisi maisha yangu kwa sasa hivi yaliyojaa mshangao, huzuni,kukata tamaa,kizunguzungu nk.

MSHANGAO: Yaani hii nchi kila kitu kinanishangaza. Kiongozi na akili zake timamu anasifia jeshi la polisi kwamba linafanya kazi nzuri sana huku tunajua wazi kwamba jeshi la polisi linanyanyasa wananchi kwa kuwabambikizia kesi, kuwaua na kuwanyang'anya mali zao. Ninajua ni baadhi ya mapolisi si wote - ila kwangu samaki mmoja akioza basi wote walio kwenye tenga wameoza! Mshangao umejaa kichwani mwangu ninapoona eti matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2012 yaandaliwe upya leo mwezi wa tano 2013!
Nina mshangao mkubwa kuona kwamba ni mpaka moto uwake na kuunguza watu ndo tunaanza kuulizana cheche zimetoka wapi ilhal muda wote tulikuwa tunaziona hizo cheche!
Tena mshangao wangu mkubwa ni kusikia viongozi tunaowaamini wakipayuka kwa sauti kubwa kwamba wana ushahidi wa video unaoonesha watu wenye mipango ya kufanya ugaidi humu nchini na mara hawa watu wanapofikishwa mahakamani
wanaambiwa hawana kesi ya kujibu! Je hao waheshimiwa sana walioona hiyo video akili zao ni timamu? Nashangaa mpaka macho yangu yanageuka makengeza!

HUZUNI: Nimejawa na huzuni nyingi wanachitchat kwa kujulishwa kwamba watanzania kadhaa huko Arusha wamepoteza maisha kwa namna ambayo ingeweza kabisa kuepukika.

KUKATA TAMAA: Mwenzenu mie nshakata tamaa na mambo ya nchi hii kitambo, sijui nyie. Viongozi kwenye wizara ya nishati wameapa kwamba hakuna mgao wa umeme lakini jana nililala kwenye giza! Hata ninapoandika thread hii umeme umekatika mara mbili. Mbali na hayo, nikimpa mke wangu sh 20,000 za kwenda sokoni ananiambia hazitoshi: mchele kilo sh 2,500 sukari kilo sh 2,200 nyama kilo sh 5,000. Familia yangu ni ya watu 5.

KIZUNGUZUNGU: Kichwa changu hakikai vizuri na huwa nahisi sauti kama kengele pale ninaposikia viongozi wa nchi hii
wanatumia maneno yafuatayo kutatua matatizo yetu: tumejenga barabara za lami, tupo kwenye mchakato, tunalifanyia kazi, tuna habari na hilo, nk.Maneno haya nimeyasikia sana kuanzia 2005 na mpaka sasa yameanza kuniletea kizunguzungu; sielewi yaani.

Kwahiyo mkuu mambo yakikaa sawa utabadili tena avatar?
 
mimi nimebadili mara moja tu, ya kwanza ilikuwa
profilepic19087_1.gif

nikabadili maana mara nyingi watu walikuwa hawakosi kuuliza jinsia.....
hii niliyonayo sitaki kuibadilisha sababu inawasaidia watu wakiona avatar tu wanajua ni fp
 
Nakufatilia sana sakapal tangu nilipokukuta kwenye jukwaa la jokes ukiifurahia joke moja ambayo hata mimi niliipenda sana. Halafu siku moja ukaleta thread ukisema kwamba ulikuwa hujisikii vizur ulitaka uchangamshwe. Nikakukumbushia hiyo joke ukafurahi sana na siku yako ikachangamka.Avatar ya wakati huo ni kweli ilikuwa ikireflect kicheko. Pamoja na hayo samahani sijapata muda wa kusign autograph yako!

oooh thats nice, thanks buddy. Would love if u,ll sign my auto ili huku niliko nikisoma nawakumbuka. U have the memory daaah!! hadi waikumbuka ile siku niliyokuwa nimeboreka na kunisaida kuniondoa ile hali ya kuwa down....., I appreciate u much HYGEIA
 
You are welcome Madam sakapal! Autograph nitasign dear. Naomba kuuliza:Uko wapi?
 
mimi nimebadili mara moja tu, ya kwanza ilikuwa
profilepic19087_1.gif

nikabadili maana mara nyingi watu walikuwa hawakosi kuuliza jinsia.....
hii niliyonayo sitaki kuibadilisha sababu inawasaidia watu wakiona avatar tu wanajua ni fp
Ni kweli @FP. Avatar yajo ya sasa ni tops!
 
Back
Top Bottom