blea
JF-Expert Member
- Nov 14, 2011
- 379
- 114
Kwa kweli maamuzi yaliyofanywa na kamati ilyoundwa kufuatilia suala la matokeo mabovu ya kidato cha nne yalikuwa ni ya kukurupuka, na yalifanywa bila kufikiriwa sawasawa. Najaribu kuwaza concept ya kustandardize matokeo, ni kwa faida ya nani? Kujifurahisha kwa kuona tunarekodi za vijana wengi waliofaulu bila kuzingatia ubora wa elimu na uwezo wa hao wanafunzi wenyewe? Si haya aliyosema Richard Mabala kuwa ni sawa na kupanua goli ili mtu afunge!!! Haya ni Maamuzi yasiyo na tija. Nampongeza sana Prof. Mkandala kama kweli atasimamia msimamo huo.
Tatizo la matokeo mabaya haliko kwenye kustandardize wala hizo grades mpya, tatizo ni mfumo mbovu wa elimu nchini. Na matatizo haya si mageni, maana yalishazungumzwa sana. Matatizo ni kama kukosa nyenzo za kufundishia, uhaba wa walimu, uhaba wa vifaa vya maabara, maslahi duni ya walimu, mazingira magumu ya kufundishia, ukosefu wa majengo ya kutosha, ubovu na uchakavu wa madarasa na nyumba za walimu, nk nk
Serikali ilipaswa iyatatue haya na si kukimbilia kkwenye kufuta matokeo na kustandardize matokeo maana matokeo haya ni kuwa na WASOMI wasio wasomi ambao kimsingi NDIYO hao wanaotuletea MATATIZO kwenye hii SERIKALI yetu ya sasa. Baadhi ya viongozi wetu ni vihiyo wa kutupwa, wana PHD ama Masters za magumashi na matokeo yake ndiyo haya kukurupuka kutoa maamuzi ambayo hayana tija kwa watanzania.
Hii ndio shida ya kuchanganya taaluma na siasa. Wanasiasa wamezoea uongo kila kitu wanataka kudanganya na kujidanganya wenyewe. Kama walitaka kuona hayo matokeo ya kupeana pasipo taaluma kuzingatiwa bora wangetoa maagizo mapema ili waliosahihisha na kupanga hayo matokeo wafuate viwango vya hao wanasiasa na si viwango vya kitaaluma. Tatizo wanasiasa wa nchi hii kila kitu wao wanaweza tuwaachie wanataaluma wafanye yao nanyi mfanye siasa zenu